» »Unlabelled » MPUMBAVU NI MTU GANI? ZIFAHAMU AINA TATU ZA WAPUMBAVU KIBIBLIA

 


Mtu wa kwanza anayeitwa Mpumbavu ni ambaye anasema Mungu hayupo. Katika ZABURI 14:1 Tunaona maneno haya "Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; ".


Mtu wa pili anayeitwa Mpumbavu ni yule asiyetenda mema bali hutenda matendo yanayomchukiza Mungu.

Mtu huyo hamwogopi Mungu hivyo hawezi kuyatenda yaliyo mapenzi yake yaani matendo mema bali matendo maovu. Tunaliona hilo katika ZABURI 14:1 " .......Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema."

Mtu wa tatu anayetajwa kuwa ni Mpumbavu ni mtu asiyefikiri maisha baada ya kufa; yeye huwaza utajiri na mali za dunia hii tu. Mtu huyu hawazi kuweka akiba kwa ajili ya Roho yake bali nafsi yake tu. Mtu anayewaza juu ya maisha ya dunia hii tu wala hafikirii ya Mbinguni huyo ni Mpumbavu. 
Tunaona hiyo katika LUKA 12:16-21 "...Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani?.....Ndivyo alivyo mtu ajiwekeaye nafsi yake akiba, asijitajirishe kwa Mungu."

Ni mimi Mwinjilisti Zachary John Bequeker 
+255-625-966-236
+255-758-590-489
 INJILI HALISI MINISTRY

Pakua App Ya Injili Halisi -Bofya Hapa Flower
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295

About INJILI HALISI MINISTRY

Zachary, most known as Zakacheka is the founder of the Injili Halisi Ministry. He is a member of Full Gospel Bible Fellowship Church.. He lives in Mwanza,Tanzania. 0621261295.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply