SOMO: INJILI NI NINI? | INJILI LAZIMA IWE NA NINI?
Alhamisi 02042020, CHATO-GEITA
Ev. Zachary John Bequeker(Zakacheka)
》Injili ni habari njema.
Habari njema kwa mwanadamu ni kusamehewa dhambi zake.
■Tunapozungumzia injili tunakuwa tunamzungumzia Yesu Kristo.
》Fahamu kwamba, baada ya Adamu kuasi, kukawa na habari mbaya za kugofya ambazo ni laana tupu na utumwa, lakini Yesu akaleta habari njema za mwanadamu kutolewa katika laana na kufanywa wana wa Mungu. Hii ndio habari njema.
■Kuna vitabu katika Biblia vinaitwa vitabu vya Injili, vitabu hivi vya Injili vinamzungumzia Yesu Kristo. Kumbe tunaona Injili lazima imzungumzie Yesu Kristo aokoaye watu kutoka katika utumwa wa dhambi kwa maana Injili ni uwezo wa Mungu uletao wokovu.
WARUMI 1:16 " Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia."
☆Habari mbaya ni kwamba sisi tulikuwa tumepotea, habari njema ni kwamba Yesu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.
LUKA 19:10 " Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea."
》Palipo na Injili pana Wokovu na palipo na Wokovu pana Injili.
》Mafundisho yote yenye vitisho hayo si Injili. Injili inafunua peupe uovu wa mtu kisha inamuelekeza ni nini anapaswa afanye ili asalimike.
Mfano 1: Mama mmoja aliambiwa na mhubiri fulani kuwa atakufa la sivyo atoe pesa kiasi cha $10,000 ambayo ni kama zaidi ya milioni 23 za Kitanzania, hebu waza hii ni habari njema kweli? Mtu umempa habari mbaya kwamba atakufa, tena unamwambia akupatie pesa zote hizo ili asife ilhali maisha yake mwenyewe ni ya kawaida, mshahara wake ni kidogo sana! Hapa utakuwa unampa habari njema au ndio unamuongezea habari mbaya? Hizo zote ni habari mbaya. Kwa kuogopa kufa anaweza kukopa fedha hizo ili alipe lakini kumbuka atakuwa bado yuko katika habari mbaya kubwa zaidi ya madeni. Kumbuka madeni ni utumwa, Yesu alikuja kututoa katika utumwa.
☆Kwanini umuogopeshe mtu kwa kusema ni injili? Hapana! Hiyo si injili bali hiyo ni Injili ya namna nyingine, na mlaaniwe katika jina ya Bwana(Wagalatia 1:6,9).
Mfano 2: Nikimwambia mtu "wewe ni mzinzi utaenda motoni" hapa hakuna nilichohubiri. Ilipaswa nimwambie hivi "wewe ni mzinzi, unatakiwa utubu ili usiende motoni"
☆Kuna mifano mingi sana ya mafundisho ya vitisho ambayo yamekuwa yakihubiriwa na kudaiwa kuwa ni injili.
■Injili inaeleza kosa la mtu na kile alichostahili kukipata kwa kosa lile kisha inampa njia ya kufanya ili aepukane na hicho kilichomstahili kwa makosa yake.
Mfano unaweza kusema "Wewe utendaye dhambi, Mungu anachukizwa na dhambi, na mshahara wa dhambi ni mauti, yaani mauti ya milele(Warumi 6:23). Okoka leo Bwana Yesu anaweza kukuokoa na kukubadilisha kabisa. Mpokee Yesu leo, tubu dhambi zako kwa kumaanisha kuziacha kabisa nawe utapata msamaha wa dhambi na kuepukana na adhabu ya moto wa milele(Mithali 28:13)" - hapa umeeleza habari mbaya alizonazo kisha ukamwambia habari njema ulizonazo ili asalimike.
HITIMISHO: Injili ni habari njema. Habari njema ni watu kusamehewa dhambi zao. Anayesamehe dhambi ni Yesu Kristo mwenyewe.
1 Yohana 2:1-2 " Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki, naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote."
Sharing is Caring
Share ujumbe huu na wengine.
By Mwinjilisti Zachary John Bequeker
INJILI HALISI MINISTRY(Online Ministry)
+255625966236
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295
No comments: