✍️Kuna kifaa hupendelewa sana kuchezewa na watoto bila shaka unalijua; kifaa hicho ni mdoli. Mtoto huweza kucheza na mdoli kwa namna yoyote ile awezavyo. Akitaka aubebe mgongoni au aukanyage ni yeye mwenyewe. Biblia siyo mdoli,hivyo hatuwezi kucheza nayo na kuipinduapindua ili kuifanya ifanye chochote tunachotaka ifanye.
✍️Biblia ni NENO LA MUNGU lililokusudiwa kumbadilisha binadamu na kumfanya kufanana na Kristo, sio binadamu aibadilishe yenyewe.
✍️Kuna njia mbili za kufasiri maandiko.
(1) Eisegesis
(2) Exegesis
✍️EISEGESIS inamaanisha kuwa unaifasiri Biblia katika muktadha wowote ambao wewe binafsi unataka, kutokana na mtazamo wowote unaotaka imaanishe.
✍️Hii ni njia ya utafsiri ISIYOFAA, ISIYOPENDEZA, ICHUKIZAYO, POTOFU, na HATARI.
✍️EXEGESIS maana yake unaifasiri Biblia katika muktadha wake ufaao, kwa mtazamo sahihi, ili kufikisha ujumbe ambao Mungu aliukusudia alipowavuvia watu wake.
✍️Hii ndiyo njia ya utafsiri SAHIHI, INAYOFAA, INAYOPENDEZA, na SALAMA.
✍️Tunapofasri kwa njia ya EISEGESIS tunapotosha maandiko na ukweli wa Neno la Mungu, yaani tunapotosha YESU maana yeye ndiye Neno.
Kwa maneno mengine, tunauonyesha ulimwengu picha tofauti ya Yesu ambayo si ya kweli kwa uhalisia, lakini ulimwengu unafikiri ni ndivyo alivyo kwa jinsi tunavyoiwasilisha kwao.
✍️Rafiki yangu upendwaye na Yesu Kristo fahamu kwamba, HATUWEZI kuifanya Biblia iseme chochote tunachotaka; HATUWEZI kuifanya Biblia ipotoshe maana yake kwa kuridhisha nafsi zetu zilizojaa tamaa.
✍️Biblia ni Neno la Mungu na ilikusudiwa kufasiriwa ili kudhihirisha maana ya MUNGU aliyoikusudia,na sio maana uliyoikusudia wewe au mtu fulani.
🍞Somo hili linaendelea sehemu ya pili...Endelea kufuatilia hadi mwisho. katika sehemu zifuatazo nitakuonesha mifano ya maandiko yanavyotafsiriwa tofauti na maana iliyokusudiwa.
🤝Ni mimi Mwinjilisti Zachary (Zakacheka Mtanzania)
Facebook: INJILI HALISI MINISTRY
💕Sharing is Caring💕
No comments: