Katika somo hili tutajifunza mambo yafuatayo:
Ø
Nini Maana ya ahadi na nadhiri?
Ø
Mifano wa walioahidi na kuweka nadhiri katika
biblia
Ø
Madhara yatokanayo na kuvunja ahadi na kutoondoa
nadhiri
NINI MAANA YA AHADI NA NADHIRI
AHADI ni sharti alilojipa mtu kulitimiza;
agano, mapatano. Ahadi inapotamkwa ni lazima itimizwe.
NADHIRI ni ahadi au kauli rasmi kabisa ya
kufanya ya kutofanya jambo fulani kwa Mungu.
Mungu huwaadhibu wale washindwao kutimiza
ahadi hiyo(nadhiri)
MIFANO WA WATU WALIOAHIDI NA KUWEKA NADHIRI
ZAO MBELE ZA MUNGU
Katika biblia kuna watu wengi walioweka
nadhiri zao mbele za Bwana. Hapa tutawaangalia baadhi yao tu:
Wa kwanza ni Hana alikuwa ni mke wa Elkana
na alipendwa sana na mmewe lakini kwa sababu hakuwa na mtoto, mke mwenzio
Penina alikuwa akimnyanyasa sana. Kitendo hiki kilimfadhaisha sana Hana akawa
ni mtu mwenye huzuni wakati wote, alilia sana. Hatimaye akaona kulia tu
haisaidii kitu ndipo akaona amwendee Muumba wa vyote, aliye mwisho wa fedheha,
Bwana wa mabwana. Kwa jinsi alivyokuwa akiomba alionekana kana kwamba amelewa
kumbe la bali ni kwa sababu alivyokuwa amezama katika maombi. Alimuomba Mungu
na akaweka nadhiri kwamba akipewa mtoto atamtoa mtoto huyo awe ni wa Bwana
miaka yote na ndivyo alivyofanya “Naliomba nipewe mtoto huyu; Bwana akanipa dua
yangu niliyomwomba;kwa sababu hiyo mimi nami nimempa Bwana mtoto
huyu; wakati wote atakaokuwa hai amepewa Bwana. Naye akamwabudu Bwana huko.” (1
SAMWELI 1:9-28)
Wa pili ni Yeftha alikuwa akienda kupigana
vitani ndipo akamwekea Bwana nadhiri, akasema, “Kwamba wewe utawatia wana wa
Amoni mkononi mwangu kweli,ndipo itakuwa ya kwamba, kile kitakachotoka katika
milango ya nyumba yangu kunilaki, hapo nitakaporudi na amani kutoka kwa hao
wana wa Amoni, kitu hicho kitakuwa ni cha Bwana, nami nitakisongeza kiwe sadaka
ya kuteketezwa”. Bwana alimsaidia akawapiga adui zake wote, pindi anarudi
aliyetoka wa kwanza kumlaki alikuwa ni binti yake na mtoto wake wa pekee, na
kumbuka katika ahadi yake alisema kitakachotoka katika malango ya nyumba yake
kumlaki atakaporudi salama atakitoa sadaka ya kuteketezwa;. Yeftha alisononeka
sana moyoni lakini kwa sababu alijua madhara ya kutotimiza ahadi ili mlazimu
amtoe mwanae wa pekee sadaka na hivyo akabaki bila mtoto. (WAAMUZI 11:30-40)
Wa tatu ni Yakobo aliweka nadhiri kwa Mungu
wakati wa safari yake akielekea Padan-aramu, katika nyumba ya babu yake
Bethueli (baba yake na mama yeke) akajitwalie huko mke katika binti za Labani, ambaye
alikuwa ni kaka yake na mama yake yaani mjomba wake. Isaka baba yake,
hakupenedelea kumuona Yakobo akioa wanawake wa Kikanaani ndipo akamuagiza
huko(MWANZO 28:20-22).
MADHARA YA KUVUNJA AHADI NA KUTOTIMIZA
NADHIRI
Kuvunja ahadi ni dhambi kama ilivyo dhambi
ya uongo (HOSEA 4:2-3), Kwa sababu unapovunja ahadi unadhihirisha kwamba kile
ulichokisema kilikuwa si cha kweli bali ni uongo na biblia inakataza kusema
uongo(WAKOLOSAI 3:9). Kuna watu wanatabia yakuwaahidi watu kuwatendea jambo
fulani na wala hawatendi, hiyo ni dhambi kama dhambi zingine na inatosha kabisa
kukupeleka motoni. Kama ulimahidi mtu na hukutimiza nakushauri utimize ahadi
yako la sivyo laana inakukalia pamoja na kwamba vitu ni vya kwako lakini
unakuwa mdaiwa kwa sababu wasawahili husema ahadi ni deni. Kumbe unapomuahidi
mtu wala hutimizi unakuwa unadaiwa na biblia inatuambia akopaye ni mtumwa wa Yeye
amkopeshaye (MITHALI 22:7), ooooh kumbe wewe ni mtumwa tayari. Hebu kataa
utumwa huo, fahamu wewe ni mtumwa wa Kristo pekee na si mtumwa wa mwanadamu,
timiza ahadi. Kama Mungu hutimiza ahadi zake kwetu kwanini wewe usitimize? Je,
wewe ni bora kuliko Mungu?
Unapoweka nadhiri mbele za Bwana kumbuka
kuziondoa (ZABURI 76:11, ZABURI 116:14)
Kumbuka ulimwomba Mungu akupe kazi, mke,
mme, watoto, nyumba, gari na ukaweka nadhiri kwamba akikupa utafanya hiki au
hautafanya kile naye akakupa, ulimwomba akufanikishe katika mambo yako na sasa
ametenda na umesahau kwamba ulimuahidia nini Bwana (AYUBU 22:27) Anayeiondoa
nadhiri anabarikiwa na asiyeiondoa analaaniwa ubarikiwe (MAMBO YA WALAWI 22:21).
Madhara ya kutoondoa nadhiri zetu ni kifo.
Anania na Safira waliahidi watauza kiwanja chao na kumtolea Bwana fedha yote ya
mauzo ya kiwanja hicho. Baada ya kuuza hawakupeleka fedha yote na badala yake
walificha na kupeleka kiasi fulani tu wakidhani Mungu hawaoni kumbe looo!
Walijidanganya nafsi zao wenyewe. Mungu aliwaua wote wawili, mke na mme
(MATENDO YA MITUME 5:1-11). Unaweza
kujisifu kwa ubingwa wako wa kuweka nadhiri na kuingia mitini wala
hawakufuatilia, nakupa pole! Unaweza sema ‘mbona mimi sijafa’, kumbe Mungu
ameshaua mambo mengine; inaweza kuwa ni kazi zako, biashara zako hazifanikiwi
kwa sasa kumbe chanzo ni ile nadhiri, ndoa yako au masomo yako kuyumba kumbe
chanzo ni ile nadhiri uliyoweka wala hukuiondoa. Mungu anaweza kukuua kimwili
yaani afya, kikazi, kibiashara, kielimu au kwa namna yoyote ile. Kuna watu
mmekuwa mkilalamika na kulalamika na kumlaumu Mungu bure kumbe tatizo ni ninyi
wenyewe mnamfanyia Mungu uhuni eeee? Kumbuka Mungu hadhihakiwi. Mkumbuke
Samsoni pamoja na kutembea na Mungu kwa miaka mingi lakini kosa moja tu
lililomfanya kutiwa chini ya mikono ya Wafilisti haikuwa ni kulala na Delila
bali ni kwa sababu alishindwa kuitunza nadhiri (WAAMUZI 13 na 16).
Kuna watu mnatabia ya kuwka nadhiri
kanisani kwamba utatoa hiki au utafanya jambo fulani hali unaona uwezo wa
kutimiza ahadi hiyo huna, unafanya ili watu wengine wakuone upigiwe na makofi
mengi halafu mwishoni unaingia mitini, nawaambia dhambi hiyo ni mbaya bora hata
kahaba neema ya Mungu inamvutavuta ili ampokee Kristo lakini kwako wewe si
umemuona Mungu ni kauchunguro? Nakupa pole ndugu yangu. Nakushauri utubu na
uziondoe nadhiri hizo ndipo utakuwa salama vinginevyo utazunguka mno kuombewa
na kuombewa pasipo mafanikio.
Kama ni mtu anaomba umsaidie jambo fulani
na unaona uwezo huna kuwa tu muwazi kuliko kumwambia ‘sawa nitakupa’ halafu
usifanye hivyo. Nakuambia hapo hakuna namna, dawa ni kutoa tu.
MHUBIRI 5:4-5 “4 Wewe ukimwekea Mungu
nadhiri, usikawie kuiondoa; kwa kuwa yeye hawi radhi na wapumbavu; basi, uiondoe
hiyo uliyoiweka nadhiri.5 Ni afadhali usiweke nadhiri, Kuliko kuiweka
usiiondoe.”
GROUP LA FACEBOOK: INJILI HALISI MINISTRY
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295
No comments: