» » JE, KUNA MAISHA BAADA YA KIFO?

                                                  Mwinjilisti Zachary John Bequeker

»Swali hili limekuwa likihojiwa kila mahali tangu nyakati za mababu. Ayubu alijiuliza swali hili ".........mtu akifa je! atakuwa hai tena?...." (AYUBU 14:1-2).

»Katika swali hilo kuna maswali hayo madogo yafuatayo:-
1. Nini hutokea baada ya mtu kufa?
2. Je, Maisha ni mtindo wa Kutoka na kurudi duniani?
3. Je, Watu wote huenda sehemu moja au kila mtu huenda mahali pake?
4. Je, ni kweli kuna mbinguni na Motoni?

»Biblia inatuambia si tu kwamba kuna maisha baada ya kufa bali ni maisha ya milele ambayo " Macho hayajawahi Ona, masikio hayajawahi sikia wala akili zetu hazijawahi fikiria ambacho Mungu ameandaa kwa ajili ya wale tu wampendae" (1 WAKORINTHO 2:9).

»Yesu Kristo, Mungu katika mwili alikuja ulimwenguni kutupatia zawadi ya maisha ya milele kwa sababu hiyo akawa tayari kuteswa kwa ajili ya dhambi zetu(ISAYA 53:5). Yesu kristo aliteswa( alisulubishwa)na kuwa tayari kuutoa uhai wake kuwa fidia ya dhambi zetu.
Siku ya tatu alijidhihirisha yeye mwenyewe kuwa ni mshindi juu
ya kifo na akafufuka kutoka kaburini. Baada ya kufufuka alikaa ulimwenguni kwa siku arobaini na alikuwa amekwisha shuhudiwa na mamia Kabla ya kwenda Mbinguni. WARUMI 4:25 inasema"....alitolewa kwa ajili ya makosa yetu , na kufufuliwa ili tupate kuhesabiwa haki".

»Ufufuo wa Yesu Kristo lilikuwa ni tukio lenye uthibitisho ulio dhahiri. Ufufuo wa Yesu kristo ni jiwekuu la pembeni katika Ukristo. Kama Yesu asingefufuka , Ukristo usingekuwepo kwani angeonekana Yeye mwenyewe kuwa ni mwongo kwa kusema kuwa atafufuka na asifufuke. Kwa sababu Yesu  Kristo alifufuka Kutoka katika mauti, tunaamini kuwa nasi tutafufuliwa . Ufufuo wa Yesu ni uthibitisho mkubwa kuwa kuna maisha baada ya kifo. Kristo pekee ndiye wa kwanza katika wale watakao fufuliwa na kuishi tena.

»Kifo kilikuja kupitia mtu mmoja Adamu, ambaye kwa yeye wote tunakufa. Lakini kwa wale walio katika familia ya Mungu kwa njia ya Imanikupitia Kristo (YOHANA 1:12) watapata maisha mapya(1 WAKORINTHO 15:20-22). Kama Mungu alivyoufufuamwili wa Yesu, ndivyo tutakavyofufuliwa Yesu Kristo akija kulinyakua Kanisa lake (1 WAKORINTHO 6:14).

»Biblia inasema kuwa tunakufa mara moja na baada ya kifo ni hukumu (WAEBRANIA 9:27). Walioishi maisha yanayompendeza Mungu wataenda kuishi maisha ya milele Mbinguni lakini ambao walimkataa Bwana Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yao watatupwa katika moto wa milele, vivyo hivyo nao watateseka milele (MATHAYO 25:46).

»Motoni, kama ilivyo Mbinguni si rahisi kueleza jinsi kulivyo lakini ni mahali panapotisha sana. Ni mahali ambapo wasio haki huishi maisha yao milele yote kwa hukumu ya milele Kutoka kwa Mungu mwenyewe. Motoni kunaelezwa ni kama Shimo refu lisilo na ukomo( bottomless pit) (LUKA 8:31, UFUNUO WA YOHANA 9:1) mahali hapo mtu mwovu huenda mara tu baada ya kukata roho, na baada ya hukumu ya siku ya mwisho watatupwa katika ziwa la moto unaowashwa kwa sulfur mchana na Usiku, milele na milele (UFUNUO WA YOHANA 20:10). Motoni kutakuwa na kilio na kusaga meno (MATHAYO 13:42).

»Mungu hafurahishwi na kifo cha mwenye dhambi lakini hutaka watubu ili waepukane na adhabu ya milele (EZEKIELI 33:11) Lakini hawezi kutulazimisha kama tukimkataa huheshimu maamuzi yetu yapo hafurahii. 

»Maisha ya hapa duniani ni mtihani na maandalizi ya maisha ya baadaye baada ya kufa. Kwa wanaomwamini Yesu maisha yao baada ya kufa  ni Mbinguni. Kwa wasiomwamini Kristo maisha yao ya milele yatakuwa katika ziwa la moto.

»Namna gani tunaweza kuepukana na ziwa la moto? Kuna njia moja pekee - kupitia kumwamini Yesu Kristo. Yesu alisema "...mimi ndimi huo Ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi; naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele.." (YOHANA 11:25-26).

»Zawadi ya bure ya uzima wa milele inapatikana kwa wote  kwa kumwamini Bwana Yesu YOHANA 3:36 " Amwaminiye mwana(Yesu) yuna Uzima wa milele; asiyemwamini Mwana(Yesu) hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia".

»Hakuna nafasi ya kutubu baada ya kufa. Hatima  ya maisha yetu ya mileleinafanyika hapa hapa duniani kwa kumkubali au kumkataa Bwana Yesu Kristo. "Wakati uliokubalika ni sasa....siku ya wokovu ndiyo sasa" (2 WAKORINTHO 6:2).

»Kama tukiamini kifo cha Yesu Kristo kuwa ni malipo halali ya dhambi zetu , tunaishi maisha ya milele Mbinguni baada ya kufa .

NI MIMI MWINJILISTI ZACHARY JOHN BEQUEKER WA MWANZA TANZANIA. WASILIANA NAMI FACEBOOK KWA JINA HILO, WHATSAPP/ CALL/SMS/ TELEGRAM/IMO 0625966236

Kwa Masomo zaidi tembelea: 
www.zakachekainjili.blogspot.com

Kwa msaada wowote, usisite kuwasiliana nami.

Pakua App Ya Injili Halisi -Bofya Hapa Flower
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295

About INJILI HALISI MINISTRY

Zachary, most known as Zakacheka is the founder of the Injili Halisi Ministry. He is a member of Full Gospel Bible Fellowship Church.. He lives in Mwanza,Tanzania. 0621261295.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply