» » SOMO: NGUVU YA MAOMBI YA KUSHUKURU



Na Zachary John Bequeker

Facebook: www.facebook.com/Zachary.bequeker 

✍ Watu Wengi tumekuwa na maombi ya kulalamika na kumnung'unikia Mungu pasipo kujua manung'uniko ni dhambi.

✍ Shukurani  humgusa Mungu moja kwa moja.

✍Neno la Mungu linatuhimiza tushukuru kwa kila jambo (1 WATHESALONIKE 5:18) Pia ni Vyema tukafahamu kwamba Mungu hupendezwa na shukurani zetu.

✍ Tusimshukuru Mungu pale tu tunapopata mambo mema tu au pale tu anapojibu Maombi yetu tu bali tuwe tayari na tuwe wepesi kumshukuru Mungu pale tunapopatwa na mabaya na kwa kufanya hivyo Mungu huguswa na hivyo kutenda jambo jema (WAFILIPI 4:6)

✍ Je, unajua kilichomfanya Lazaro afufuke?   ni Shukurani. YOHANA 11:41-43 "Basi wakaliondoa lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia....Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje.
Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende zake."

Hapo tunaona *Yesu alishukuru* na muujiza mkubwa ukatendeka.

✍Kumbe maombi ya kushukuru yanaweza kufufua ndoa yako, elimu yako, kazi yako, biashara yako, familia yako n.k

Je, umeomba mchumba kwa muda mrefu na bado hujapata?  Usiseme *"kwa nini Mungu hunisikii"?* Sema *"Ahsante Mungu kwa maana Mke/Mme wangu anakuja."*

SHUKURU SHUKURU SHUKURU

Kwa Masomo zaidi tembelea: www.zakachekainjili.blogspot.com

Ni mimi Ev. Zachary John Bequeker Kutoka Mwanza Tanzania wa INJILI HALISI.

Pakua App Ya Injili Halisi -Bofya Hapa Flower
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295

About INJILI HALISI MINISTRY

Zachary, most known as Zakacheka is the founder of the Injili Halisi Ministry. He is a member of Full Gospel Bible Fellowship Church.. He lives in Mwanza,Tanzania. 0621261295.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply