» » SOMO: JE, HUNA LA KUMSHUKURU MUNGU?


Sasa tunatoka mwaka 2018 na kuingia mwaka 2019 na kila mmoja anatazamia kufanya mambo mengi sana kwa mwaka wa 2019. Ni muhimu kujiuliza kwamba tunapopanga ni nani anayetuwezesha kufanikisha mipango yetu na tumewezeshwa mangapi 2018 na je, tumshukuru Mungu kwa kiasi gani 2018 kwa hayo aliyotutendea?

Kuna mambo mengi mno ya kushukuru Mungu kama:-
1. Afya au uzima
2. Biashara
3. Elimu
4. Familia
5. Kazi
6. Miujiza n.k

Nebkadreza aliona kuwa yote aliyoyafanya ni kwa nguvu zake na si kwa uwezo wa Mungu, akasahau kuwa Mungu ndiye aliyemuwezesha kuwa vile na pia anaweza kuviondoa (DANIELI 4:28-31).

Shukrani ina nguvu kwani shukurani humfanya Mungu atukumbuke kwa mwaka mwingine.
Wale wenye ukoma waliomba na baada ya kupokea muujiza yule mmoja tu ndiye aliyejua umuhimu wa kushukuru akarudi kushukuru Yesu (LUKA 17: 11-19) Hapa aliyekuwa na moyo wa kushukuru ni mmoja tu na wale tisa hawakuona umuhimu wa kushukuru.
Shukurani ina nguvu kuliko kuomba. 
Yesu alishukuru Lazaro akafufuka. Pia Yesu alishukuru kwa ile mikate mitano na samaki wawili watu wakala na kusaza.

Tusiwe wagumu wa kushukuru kwani hakuna mtu miongoni mwetu anayeishi kwa nguvu zake wenyewe bali kwa nguvu za Mungu, hivyo yeye huweza kutuondoa wakati wowote.

Hakuna kitu kikubwa kama uzima hivyo hata kama hatukutendewa mambo makuu mwaka 2018 lakini kwa uhai tu tunastahili kushukuru Mungu. Jaribu kuwaza watu wanaokufa kila baada ya saa, siku na mwaka. Kutokana na takwimu zinazo aminika za shirika la Ecology Global Network inaonesha idadi ya watu wanaokufa duniani kwa saa, siku na mwaka. Kila baada ya saa moja  watu 6,316 hufa, kwa siku ni watu 151,600 na kwa mwaka ni 55,300,000 (Milioni hamsini na tano na laki tatu). Jaribu kuwaza katika orodha ya majina ya watu elfu sita, mia tatu kumi na sita ambao wanakufa kila saa wewe umeshindwa kuwamo na zaidi sana kwa orodha ya majina ya watu zaidi ya milioni hamsini na tano kwa mwaka wewe jina lako halikuwemo Je, wewe ni bora   kuliko hao waliokufa? Je, wewe ni Mtakatifu sana? Jibu ni la! Bali ni huruma tu za Mungu (MAOMBOLEZO 3:22).

Tunafanikisha yote kama Mungu akitufanikisha hivyo basi hata kuwa wazima tu ni kwa sababu Mungu amependa tuwe hai. Hivyo si vyema kujisifu kuwa ni kwa uwezo wetu ndiyo tuko hai (YAKOBO 4:13-16) Hata kama tumepitia au tuko kwenye mabaya tunapaswa kushukuru Mungu kwa hali hii ili kuona kwamba anatutetea kwa hayo kama Paulo na Sila gerezani pamoja na mabaya yaliyowapata hawakulia na kuanza kumlalamikia Mungu bali walianza kumtukuza pamoja na kufungwa.

Tunamshukuru Mungu kwa vinywa vyetu na kutoa sadaka(dhabihu) za kushukuru (ZABURI 107:21-22)

SHUKURU SHUKURU SHUKURU

HERI YA MWAKA MPYA 2019
Ni mimi Mwinjilisti Zachary John Bequeker
INJILI HALISI MINISTRY
+255625966236
+255758590489
zacharybequeker@gmail.com

Pakua App Ya Injili Halisi -Bofya Hapa Flower
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295

About INJILI HALISI MINISTRY

Zachary, most known as Zakacheka is the founder of the Injili Halisi Ministry. He is a member of Full Gospel Bible Fellowship Church.. He lives in Mwanza,Tanzania. 0621261295.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply