Fahamu kwamba Mungu anakupenda!
Biblia inatuambia
kwamba, “Kwa maana
jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu
amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.” – YOHANA 3:16
Tatizo ni kwamba…………
Wote tumetenda, tumewaza au kuzungumza maovu. Hii inaitwa
dhambi, na dhambi zetu hututenganisha na Mungu wetu.
Biblia inasema katika WARUMI 3:23 “kwa sababu
wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.”
Mungu ni mkamilifu na mtakatifu, na dhambi zetu hututenga
sisi na Mungu milele. Biblia inasema “Mshahara wa dhambi ni mauti.” – WARUMI 6:23
Habari njema ni kwamba, miaka 2,000 iliyopita,
Mungu alimtuma mwanae wa pekee Yesu Kristo ili afe kwa ajili
ya dhambi zetu.
Yesu ni mwana wa Mungu. Aliishi maisha yasiyo ya dhambi hapa
duniani kasha akafa msalabani ili kulipa deni za dhambi zetu.
“Bali
Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa
ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.” –WARUMI 5:8
Yesu alifufuka kutoka katika mauti na sasa yu hai mbinguni
pamoja na Mungu Baba. Alitupatia zawadi ya Uzima wa Milele – wa kuishi milele
pamoja na Yeye mbinguni kama tukimkubali yeye kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha
yetu.
Yesu alisema “Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa
Baba, ila kwa njia ya mimi.” – YOHANA 14:6
Mungu hudhihirisha pendo lake kwako na anakutaka wewe uwe mtoto
Wake. “Bali wote
waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio
jina lake.” – YOHANA 1:12. Unaweza kumuomba Yesu kristo akusamehe dhambi
zako na awe katika maisha yako kama Bwana na Mwokozi.
Kama unataka kumpokea Kristo kama Bwana na Mwokozi na
akuondoe katika dhambi zako, unaweza kumwomba kwa kufuatisha sala hii:
“Bwana Yesu,
naamini wewe ni Mwana wa Mungu. Ahsante kwa kufa msalabani kwa ajili ya dhambi
zangu. Nakuomba unisamehe dhambi zangu zote na unipe zawadi ya uzima wa milele.
Ninakuhitaji katika maisha yangu na moyo
wangu uwe Bwana na Mwokozi wangu. Nahitaji niyatenda matendo yako mema wakati
wote katika jina lako Yesu Kristo Amen”
“Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa
milele; na uzima huu umo katika Mwanawe” – 1 YOHANA 5:11
Je, umefuatisha sala hii? Kama ni ndiyo bonyeza neno hili<<<NDIYO>>>
Je, umefuatisha sala hii? Kama ni ndiyo bonyeza neno hili<<<NDIYO>>>
© 2018 INJILI HALISI MINISTRY
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295
No comments: