ISAYA 7:14 “14 Kwa hiyo Bwana mwenyewe
atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye
atamwita jina lake Imanueli.”
ISAYA 9:6 “6 Maana kwa ajili yetu mtoto
amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake;
Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele,
Mfalme wa amani.”
Yesu Kristo alizaliwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, mbegu ya
mwanamume haikuwa na nafasi juu yake naye alizaliwa kwa ajili ya kuokoa.
MATHAYO 1:18-25 “18 Kuzaliwa kwake Yesu Kristo
kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla
hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu. 19 Naye
Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu
kumwacha kwa siri. 20 Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana
alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua
Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa
uweza wa Roho Mtakatifu. 21 Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake
Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao. 22 Hayo yote
yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii akisema, 23
Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli;
Yaani, Mungu pamoja nasi. 24 Naye Yusufu alipoamka katika usingizi, alifanya
kama malaika wa Bwana alivyomwagiza; akamchukua mkewe; 25 asimjue kamwe hata
alipomzaa mwanawe; akamwita jina lake
YESU.”
Yesu Kristo alizaliwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, mbegu ya
mwanamume haikuwa na nafasi juu yake naye alizaliwa kwa ajili ya kuokoa na ndio
maana aliishi pamoja na wanadamu bila kufanya dhambi. Dhambi ile ya asili itokanayo
na Adamu haikuwa na nguvu kwake kwa sababu alizaliwa kwa uweza wa Roho
Mtakatifu.
WAEBRANI 4:15 “15 Kwa kuwa hamna kuhani mkuu
asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo
yote, bila kufanya dhambi.”
Sisi nasi tuliozaliwa mara ya pili kwa uwezo wa Roho
Mtakatifu yaani tuliookolewa, tukimkaribia anatupa huo uwezo wa kushinda
dhambi.WAEBRANI 4:15-16 “15 Kwa kuwa hamna kuhani mkuu
asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa
sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi.16 Basi na tukikaribie
kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia
wakati wa mahitaji.”
Yesu Kristo alizaliwa katika mazingira duni lengo ni
kutuonesha jinsi ilivyo muhimu kuanzia chini na ndipo tunapandishwa juu kama
yeye alivyozaliwa katika hori ya kulia ng’ombe Bethlehemu, akaingia Nazareti
kisha Yerusalemu na hatimaye akaingia Mbinguni.
LUKA 2:1-7 “4 Yusufu naye aliondoka Galilaya, toka mji wa Nazareti,
akapanda kwenda Uyahudi mpaka mji wa Daudi, uitwao Bethlehemu, kwa kuwa yeye ni wa mbari na jamaa ya Daudi; 5 ili
aandikwe pamoja na Mariamu mkewe, ambaye amemposa, naye ana mimba. 6 Ikawa,
katika kukaa huko, siku zake za kuzaa zikatimia, 7 akamzaa mwanawe, kifungua
mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng'ombe, kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba
ya wageni.”
JINSI YA KUSHEHEREKEA KUZALIWA KWA YESU
Kusudi la Yesu Kristo kuzaliwa ni ili aje kuokoa watu na
dhambi zao.
YOHANA 3:16 “16 Kwa maana jinsi hii Mungu
aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye
asipotee, bali awe na uzima wa milele.”
Hivyo basi ili kuhakikisha tunasheherekea vizuri sikukuu ya
Krismas ni lazima tuwe tumezaliwa mara ya pili yaani tumeokoka.
Kama wewe bado hujaokoka hakikisha unafanyika mtoto wa Mungu
kwa kutubu dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha kabisa.
YOHANA 1:12 “12 Bali wote waliompokea
aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;”
Tunasheherekea kuzaliwa kwa Yesu kwa toba. Tubu kwa wazazi,
watoto ndugu, jamaa, marafiki, na watu
wote ambao unahisi uliwakosea kwa namna moja au nyingine.
Hatusherekei kuzaliwa kwa Yesu Kristo kwa uzinzi, uasherati,
ulevi, ukahaba na uovu wa kila namna bali tunasheherekea tukiwa na furaha kwa
watu wote kwa maana siku Yesu Kristo alipozaliwa furaha ilitanda kila mahali.
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295
No comments: