Kitabu cha uzima ni kimoja kama tunavyoona katika UFUNUO WA YOHANA 20:11-12 “11 Kisha nikaona kiti cha enzi,
kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso
wake, na mahali pao hapakuonekana. 12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo,
wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na
kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu
wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na
matendo yao.”
Walio katika kitabu cha Uzima ni watakatifu kama tunavyoona
katika maandiko yafuatayo.
WAFILIPI 4:3 “3 Naam, nataka na wewe pia,
mjoli wa kweli, uwasaidie wanawake hao; kwa maana waliishindania Injili pamoja
nami, na Klementi naye, na wale wengine waliotenda kazi pamoja nami, ambao
majina yao yamo katika kitabu cha uzima.”
LUKA 10:20 “20 Lakini, msifurahi kwa vile
pepo wanavyowatii; bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni.” Yesu aliwaambia Wanafunzi wake wanapaswa
wafurahi si kwa sababu wanaupako wa kukemea pepo wakatoka bali kwa sababu
majina yao yameandikwa mbinguni katika kitabu cha uzima. Kumbe, kuna uwezekano
wa kufanya miujiza hali majina yetu hayako katika kitabu cha uzima kwani hata
shetani mwenyewe anaweza kufanya miujiza. Pamoja na kuona kuwa tunatumiwa kwa
namna ya ajabu katika kutenda miujiza vile vile ni lazima kuhakikisha majina
yetu yameandikwa katika kitabu cha uzima Mnvinguni.
WAEBRANIA 12:23 “23 mkutano mkuu na kanisa
la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu
wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika”
UFUNUO WA YOHANA 3:5
“5 Yeye ashindaye atavikwa
hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima, nami
nitalikiri jina lake mbele za Baba yangu, na mbele ya malaika zake”
Watu wasioandikwa katika kitabu cha uzima hawataingia Mbinguni.
Inavyokuwa ni kwamba mtu anapokufa ni hukumu moja kwa moja kama tunavyoona
katika WAEBRANIA 9:27 “27 Na kama vile watu
wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu” Mtu ambaye
alikuwa akitenda dhambi jina lake halikuwa katika kitabu cha uzima bali vitabu
vya hukumu. Anapokufa moja kwa moja anaenda Jehanamu au motoni. Na watenda
dhambi waliopo duniani watapitia katika kipindi cha dhiki kuu baada ya Yesu
Kristo kulinyakua kanisa lake. UFUNUO WA
YOHANA 13:8 “8 Na watu
wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika
kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi
ya dunia.”
UFUNUO WA YOHANA 17:8
“8 Yule mnyama uliyemwona
alikuwako, naye hayuko, naye yu tayari kupanda kutoka kuzimu na kwenda kwenye
uharibifu. Na hao wakaao juu ya nchi, wasioandikwa majina yao katika kitabu cha
uzima tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, watastaajabu wamwonapo yule
mnyama, ya kwamba alikuwako, naye hayuko, naye atakuwako.”
Baada ya dhiki kuu wale wote waliokuwa wamekufa katika
dhambi na wale wote waliokuwa wakipitia dhiki kuu watatupwa katika ziwa la moto.
UFUNUO WA YOHANA 20:11-15 “15 Na iwapo mtu ye yote
hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa
la moto.”
Kama umeokoka jina lako linakuwa katika kitabu cha uzima na
ukitenda dhambi jina lako linafutwa katika kitabu cha uzima na kuandikwa katika
vitabu vya hukumu.
KUTOKA 32:32-33 “32 Walakini sasa, ikiwa
utawasamehe dhambi yao - na kama sivyo, unifute, nakusihi, katika kitabu chako
ulichoandika. 33 Bwana akamwambia Musa, Mtu ye yote aliyenitenda dhambi ndiye
nitakayemfuta katika kitabu changu.” Musa alimuomba Mungu
awasamehe wana wa Israeli na kama hawasamehi basi amfute katika kitabu cha
uzima ndipo Mungu akamwambia wanaofutwa katika kitabu cha uzima ni wale
walionitenda dhambi maana yake ni kwamba Musa asingewezwa kufutwa kwa sababu
hakuwa maetenda dhambi kwa wakati huo.
Tujitahidi kutenda mema ili majina yetu yaandikwe mbinguni. MATHAYO 7:21-22 “21 Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana,
atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba
yangu aliye mbinguni. 22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya
unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya
miujiza mingi?”
Tuwe tayari kutubu wakati wote wala tusijihesabie haki kwa
sababu dhambi si mpaka uibe, uzini, useme uongo n.k bali dhambi ni kutotenda
uliyoagizwa kutenda na kutenda uliyokatazwa kutenda. Kutenda mema ni kuomba,
kutoa, kuwahubiri wengine, kuhudhuria ibada, kuwapenda wengine n.k na kutotenda
tuliyoagizwa ni kwenda kinyume na neno la Mungu, Mungu anatuambia tusiibe tunaiba,
tusiue tunaua, tusizini tunazini hizo zote ni dhambi. Umeambiwa usiue unaua ni
dhambi, pia Mungu anatuagiza kuyafanya mapenzi yake yote na huyafanyi hiyo nayo
ni dhambi.
YAKOBO 4:17 “17 Basi yeye ajuaye kutenda
mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi.”
WAFILIPI 3:12-16 “12 Si kwamba nimekwisha kufika,
au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! Bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile
ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu. 13 Ndugu, sijidhanii nafsi
yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo
nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele; 14 nakaza mwendo, niifikilie mede ya
thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.”
Tunapogundua kuwa tumetenda dhambi basin a tutubu mara moja
kwake Yesu kristo ambaye ni ondoleo la dhambi zetu MATENDO YA MITUME 10:43 “43 Huyo manabii wote humshuhudia, ya kwamba kwa jina lake kila
amwaminiye atapata ondoleo la dhambi.”
1 YOHANA 2:1-2 “1 Watoto wangu wadogo,
nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye
Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki, 2 naye ndiye kipatanisho
kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu
wote.”
JE, UNATAKA ONDOLEO LA DHAMBI?
BONYEZA HAPA>>>>> NATAKA MSAMAHA WA DHAMBI
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295
No comments: