» »Unlabelled » CHAPA YA MNYAMA "666"


CHAPA YA MNYAMA "666"
Jumanne 07042020,
Ev. Zachary John Bequeker(Zakacheka)
www.zakachekainjili.blogspot.com
》Yesu alisema dalili za kuja kwake kuwa ni vita, magonjwa yasiyokuwa na tiba, njaa,matetemeko ya nchi mahali mahali, manabii wa uongo, mambo ya kutisha na ishara kutoka Mbinguni (Mathayo 24:7-14, Marko 13:7-8, Luka 21:10-11). Lakini pia akasema hayo yote yatatokea lakini ule mwisho bado (Marko 13:7).

》Unyakuo hautatokea mpaka habari njema itakapohubiriwa ulimwenguni kote na vilevile dhiki kuu haitatokea mpaka unyakuo utokee. Tunasubiria injili ihubiriwe ulimwenguni kote ndipo unyakuo utafuatia ambapo Watakatifu watakuwa wamenyakuliwa hapa duniani kwenda Mbinguni.

☆Angalia mtirirko wa matukio haya: 👇
 Unyakuo -> Sherehe Mbinguni (miaka 7) -> Dhiki kuu duniani (miaka 7) -> Ujio wa Yesu Kristo mara ya pili duniani -> Vita vya Harmagedoni -> Utawala wa miaka 1000 duniani pamoja na Yesu Kristo -> Vita vya Gogu na Magogu -> Hukumu ya mwisho -> Umilele (Mbinguni au Motoni)

■CHAPA YA MNYAMA
》 Chapa ya mnyama itakuwa ni katika kipindi cha dhiki kuu ambayo itadumu kwa kipindi cha nusu ya miaka saba ya dhiki kuu, yaani miaka mitatu na nusu.

》Katika kipindi hiki cha dhiki kuu, wanyama wawili wenye mamlaka watapata nguvu za ajabu kutoka kwa shetani mwenyewe. Mnyama wa kwanza atakuwa ni kiongozi wa kisiasa (2 Wathesalonike 2:1-4, Ufunuo 13:1-10) ambaye anaitwa Mpinga Kristo. Huyu atakuwa ni kiongozi wa serikali ya dunia nzima ijayo. Mpinga Kristo atakaa katika hekalu huko Yerusalemu na kujitangaza kama Mungu (Mathayo 24:15, 2 Wathesalonike 2:4). Mnyama wa pili ni Nabii wa uongo (Ufunuo 13:11-18, 19:20-21). Huyu atakuwa ni kiongozi wa dini. Nabii wa uongo ndiye atakayelazimisha watu kupokea chapa ya mnyama "666" ili kuweza kuuza na kununua (Ufunuo 13:16-17).

》 Baada ya Mpinga Kristo na Nabii wa uongo kupata nguvu ndipo chapa ya mnyama itahitajika kwa kila mmoja ili aweze kununua au kuuza. Wale wote watakao kataa chapa hii watatishiwa kuuawa.

■HITIMISHO: Unyakuo utaanza kwanza na baadaye katika kipindi cha dhiki kuu chapa ya mnyama "666" itatokea. Watakatifu wote hawatakuwepo katika kipindi hiki. Kumbuka Nabii wa uongo ndiye atakayetenda kazi ya chapa ya 666 kwa miaka mitatu na nusu, ukiangalia unaona ni kama kazi zake zinaonekana, yaani ishara na madanganyo ya kishetani, lakini ukweli ni kwamba yeye bado hajadhihirishwa. Nabii wa uongo atadhihirishwa mara tu baada ya kanisa kunyakuliwa anaanza Mpinga Kristo kisha Nabii wa uongo. Kanisa yaani Watakatifu ndio kizuizi cha yeye kutenda kazi, kanisa likiondolewa ndipo ataweza kujidhihirisha kwelikweli (2Wathesalonike 2:7-10)


❤Sharing is Caring❤
Share ujumbe huu na wengine.
By Mwinjilisti Zachary John Bequeker
INJILI HALISI MINISTRY(Online Ministry)
www.zakachekainjili.blogspot.com
+255625966236
Fb group: https://www.facebook.com/groups/281957879249363/

Pakua App Ya Injili Halisi -Bofya Hapa Flower
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295

About INJILI HALISI MINISTRY

Zachary, most known as Zakacheka is the founder of the Injili Halisi Ministry. He is a member of Full Gospel Bible Fellowship Church.. He lives in Mwanza,Tanzania. 0621261295.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply