» »Unlabelled » TOFAUTI KATI YA RUSHWA NA SHUKRANI


»Kumekuwa na mkanganyiko mkubwa katika matendo haya mawili katika jamii ya sasa. Watu wamekuwa wakitafsiri tofauti rushwa na Shukurani. Watu wengi wameifanya Shukurani kuwa rushwa na rushwa kuwa Shukurani kitu ambacho ni kinyume kabisa.
»Kumbuka Neno la Mungu linasema "Shukuruni kwa kila jambo" tena sehemu nyingine inasema "Iweni watu wa Shukurani" Lakini pia Neno la Mungu linasema waziwazi kuwa rushwa ni dhambi. Kwanini ni dhambi? Ni dhambi kwa sababu inapotosha haki. Kuna msemo wa kiswahili unasema "rushwa ni adui wa haki".
»Sasa hebu tuone maana ya rushwa na Shukurani ili iwe rahisi kwetu kutofautisha.
RUSHWA ni fedha au kitu cha thamani kinachotolewa na kupewa mtu mwenye madaraka ya jambo fulani ili mtoaji apatiwe upendeleo.
SHUKURANI ni neno, kitu, fedha au ishara inayoonyesha kuridhika na wema aliotendewa mtu.
TOFAUTI kubwa ya rushwa na Shukurani ni kwamba; Rushwa hutolewa kwa lengo la kumshawishi mtu akutendee jambo fulani. Mara nyingi Rushwa hutolewa kabla ya kupatiwa huduma. Ambapo Shukurani hutolewa kwa lengo la kushukuru kwa jambo ulilotendewa.

|Ukweli wa Biblià
1 Wathesalonike 5:18 "shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu."
1 Nyakati 16:34 "Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema; Kwa maana fadhili zake ni za milele."
Zaburi 118:21 "Nitakushukuru kwa maana umenijibu, Nawe umekuwa wokovu wangu."
Kutoka 23:8 "Nawe usipokee rushwa; kwani hiyo rushwa huwapofusha macho hao waonao, na kuyapotoa maneno ya wenye haki."
1 Samweli 8:3 "Ila wanawe hawakuenda katika njia zake, bali waliziacha, ili wapate faida; wakapokea rushwa, na kupotosha hukumu."
Mithali 17:24 "Asiye haki hutoa rushwa kifuani, Ili kuzipotosha njia za hukumu."
Mithali 29:4 "Mfalme huithibitisha nchi kwa hukumu; Bali yeye apokeaye rushwa huipindua."
Muhubiri 7:7 "…rushwa huuharibu ufahamu."
…………••••••••••………
Heri ya Mwaka Mpya 2020
zakachekainjili.blogspot.com

Pakua App Ya Injili Halisi -Bofya Hapa Flower
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295

About INJILI HALISI MINISTRY

Zachary, most known as Zakacheka is the founder of the Injili Halisi Ministry. He is a member of Full Gospel Bible Fellowship Church.. He lives in Mwanza,Tanzania. 0621261295.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply