Jiulize, Kama ungekufa
leo, Ungeenda wapi?
Uamuzi Sahihi Utakaoufurahia Milele
www.zakachekainjili.blogspot.com
KWANINI?
Utakapokufa, hautapotea tu. Utaingia katika
maisha mengine ya umilele mahali Fulani. Mbingu ipo na Motoni kupo pia. Watu
hawapendi kuzungumzia kuhusu motoni au kufikiri
kuhusu huko. Lakini ni kweli kabisa Jehanum ipo. Na tunapaswa
kuizungumzia ili kila mmoja ajue na aweze kufanya maamuzi sahihi.
Mbinguni ni mahali kwa wale waliosamehewa
makosa yao na Mungu. Na motoni ni kwa wale ambao hawajapata msamaha huo.
Mungu ni mwema, Mungu Baba anataka uwe na
uhusiano mzuri nay eye na hatimaye uurithi uzima wa milele Mbinguni ambako kila
kitu ni chema.
Unawezaje kupata msamaha kutoka kwa Mungu?
YESU
Njia pekee ya kupata msamaha wa dhambi zako ni
Yesu. Yesu ni mwana wa Mungu. Aliyatoa maisha yake na kuwa tayari kufa msalabani
kwa ajili ya dhambi zetu wanadamu. Yesu
aliipa deni la maovu yetu na kwa jinsi
hiyo tunapata msamaha wa maovu yetu kwa Mungu.
Lakini msamaha hauji tu wenyewe. Unapaswa
umkiri Yesu kuwa Mwokozi wa Maisha yako ndipo upate msamaha.
Unawezaje kumkiri Yesu kuwa Mwokozi wako?
SASA
Unaweza Kumkiri Yesu kuwa Mwokozi wa Maisha
yako sasa hivi kwa kuomba sala ifuatayo. Tamka kwa sauti, sema maneno yote kwa
moyo wako wote.
Sala ya Msamaha wa
Dhambi
“Mungu, nisamehe kwa
makosa niliyoyatenda. Nakuomba unisamehe. Yesu, Wewe ni Mwana wa Mungu. Ahsante
kwa kulipa deni la dhambi zangu kwa kifo chako msalabani. Naamini ulifufuka
kutoka mautini na sasa uko Mbinguni. Nakukubali uwe Bwana na Mwokozi wa
Maaaisha yangu. Yesu, Nakualika ukae name maishani mwangu sasa katika jina la
Yesu Amen!”
Kama umeomba sala hii kwa kumaanisha,
umesamehewa na uhusiano wako na Mungu umerejea upya tena. Na kupitia uhusiano
huu sahihi na Mungu utaenda Mbinguni na Kuishi Maisha ya Umilele huko. Hongera!
Hakikisha unabonyeza maneno meusi hapa chini yaliyoandika HATUA YA 2 kwa msaada zaidi wa kiroho ili uzidi kukua na kumjua
Yesu zaidi.
Kama umemkubali Yesu
kuwa Mwokozi wako baada ya kusoma ujumbe huu, tunapenda kusikia kutoka kwako!
Pia kila mmoja anakaribishwa kuchangia maoni yake pamoja nasi. Unaweza
kutufikia kwa kutumia email ifuatayo: zacharybequeker@gmail.com
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295
No comments: