» » BABA WA KIROHO


Waefeso 6:1-3.
BibliĆ  imeweka wazi juu ya wazazi wawili. Tuna baba wa kimwili na baba wa kiroho. Waefeso 6:2-3 inasema, " Waheshimu baba yako na mama yako; Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia." Hii inazungumzia baba zetu wa kimwili. Halafu kuna sehemu inasema kwamba, "Watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana...." Hapa anaongelea wazazi wa kiroho. Katika 2 Wafalme 2:11-12, Elisha alimuita Eliya, "baba yangu, baba yangu..."
Mtume, mchungaji na nabii wanatambulika kama mababa. Soma 1 Wakorintho 4:15-16.
Kuna wazazi wa kiroho na una paswa kuwaheshimu ili kuepuka laana ya kutowatii wazazi katika Bwana. Ukisoma atika Wafalme wa Kwanza sura ya 19, utaona Elisha alikuwa na wazazi wake wa kimwili lakini baadaye alishikamana na Eliya akawa baba yake wa kiroho.
Paulo hakuwa na watoto wa kuzaa kimwili lakini hapa anajitambulisha kama baba. Maana yake kuna kuzaa kimwili na kuzaa kiroho kwa njia ya injili.
1 Wakorintho 4:15 "Kwa kuwa ijapokuwa mna waalimu kumi elfu katika Kristo, walakini hamna baba wengi. Maana mimi ndimi niliyewazaa katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili."
Hitimisho: Ni vyema kuwatambua wale waliowekwa na Mungu kama wachungaji wetu kuwa ni wazazi Wetu, hivyo tunapaswa tuwaheshimu.
Je, unataka kuokoka?
Tuma neno "NATAKA KUOKOKA" kwa SMS au WhatsApp kwa +255625966236
KWA MAFUNDISHO TEMBELEA;
šŸ”—zakachekainjili.blogspot.com
šŸ’• Sharing is CaringšŸ’“

Pakua App Ya Injili Halisi -Bofya Hapa Flower
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295

About INJILI HALISI MINISTRY

Zachary, most known as Zakacheka is the founder of the Injili Halisi Ministry. He is a member of Full Gospel Bible Fellowship Church.. He lives in Mwanza,Tanzania. 0621261295.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply