» » MAMBO YA MUHIMU KUHUSU KUOA NA KUOLEWA

Kaka Joseph M. Marwa

»Kuna vitu vitatu ambavyo biblia inatuagiza kuwa navyo ili tuwe na sifa ya kuoa mke.
Vitu hivyo ni:-

1. Uwezo wa kumhudumia kwa CHAKULA
 2. Uwezo wa kumhudumia kwa MAVAZI
3. Uwezo wa kumhudumia kwa UNYUMBA

Soma: KUTOKA 21:10 "Kwamba ajitwalia mke mwingine; CHAKULA chake huyo, na NGUO zake, na NGONO yake, hatampunguzia."

1 WAKORINTHO 7:9 "Lakini ikiwa hawawezi kujizuia, na waoe; maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka TAMAA."

Biblia inaainisha mambo ya mhimu matatu hapo mwanzo, ya kumfanyia mke utakaye muoa. Lakini kama hilo la tatu hauwezi,yaani una upungufu wa nguvu za kiume (maana yake jogoo hawiki) basi unapoteza sifa  hata kama una V8 Lexus au MAGHOROFA😁😁😁Itakubidi usubiri uendelee kumuomba MUNGU akuondolee kwanza hilo tatizo kabla ya kuamua kuoa. Msingi wa kuoa na kuolewa ni ili kuishinda ZINAA 1 WAKORINTHO 7:2 "Lakini kwasababu ya ZINAA kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe.

Kuoa mke wakati bado unatatizo (yaani jogoo hawiki) ni kuongeza matatizo. Ukimuoa ninani atakayempa hitaji hilo la tatu? Maana kama ni chakula na nguo hata WAZAZI au NDUGU zake wanaweza kumpa, kwa ufupi hata yeye mwenyewe anaweza akafanya kazi na kujilisha na kujivisha, hilo la tatu ndiyo linaloleta tofauti na ndiyo msingi na sababu ya ndoa yenyewe wala siyo watoto.

Kuna watu linapokuja suala hili hutoa visingizio chungu mzima na wakati mwingine kufikiri kuwa wataonekana watu wa MWILINI wakionekana wanamlingana BWANA kwa bidii kwaajili ya NDOA. Hauhitaji TV, Sofa, Gari na Furniture za gharama ili uoe. Kama unauwezo wa kuhudumia familia kwa chakula, mavazi/malazi na kutimiza wajibu wako kwa mkeo yaani kumtendea kama ilivyo desturi umemaliza.

Kulingana na ripoti maalum za kitaalam zinaonesha kijana huanza kuwa na michocheo ya hormone kuanzia miaka 12,13 na wakati mwingi 14. Kulingana na tafiti hizo kijana huyo huzalisha mbegu 1500 kwa sekunde MOJA, sawa na mbegu 64,800,000 kwa siku. Ni katika umri huu vijana huona mabadiriko katika miili yao kwa kasi ya ajabu.

Ikitokea wamekosa ushauri na kufundishwa, wengi wao huanza KUJICHUA au PUNYETO na kuvutwa katika uchafu mwingi ikiwemo ULAWITI, kunajisi VITOTO na wengine UASHERATI. Wakati mwingine unaweza ukakuta kijana mstaarabu hana habari kabisa na UASHERATI lakini kwa kiasi kikubwa ANAJICHUA au KUNAJISI vitoto.Jambo ambalo linaweza kumgharimu mtu JEHANUM ya moto🔥🔥🔥

Ni umri upi ni sahihi kuoa na  kwanini? 18+ sheria za nchi yetu zinaruhusu kabisa kufanya maamuzi ya busara. Japo wengi hupendekeza angalau miaka 21 kwa kijana na 18 kwa binti ijapokuwa siyo sheria. Katika taifa la Israel kwa mfano vijana wa miaka 14 waliruhusiwa kuoa na mabinti wa miaka 12 hadi 13 waliluhusiwa kuolewa (Google marriage in ancient Israel). Kwanini ilifanyika hivyo, ilikuwa ndiyo muda ambao binti alikuwa anastawi au kupevuka kwa kasi na ili kulinda aibu isitokee akaolewa akiwa hana alama za UBIKIRA; jambo ambalo lingemgharimu kifo

UZURI WA MKE/MUME HAUKO KATIKA KITU KIMOJA
Kuna watu wanapoteza muda mwingi sana kwa kuhangaika na FRAME za nje. Ukweli ni kwamba kila kitu cha THAMANI kimefichwa (Hii ni SIRI kubwa ambayo wengi hawaijui kwa habari ya kuoa na kuolewa). Wengi wao hata ukiwatazama hivi unaweza kuwadharau kama Sauli kwa Daudi; lakini wamebeba HAZINA nzito nzito.

Anaweza akawa ni kijana au binti mzuri sana wa umbo na sura akawa siyo saizi yako, au akawa na kilema kilichofichwa na nguo, au akawa mvivu sana, au akawa mchafu, au akawa na udhaifu kwa habari ya magonjwa kiasi kwamba anahitaji UVUMILIE, au ni mjeuri na hasira za kupita kawaida au kama mwanadamu akawa na mapungufu mengi tu yanayohitajika kuvumiliwa.

Unachohitaji wewe ni kumlingana BWANA akupe wa kufanana na wewe na si vinginevyo. Unaweza ukakuta binti au kijana anavutia sana kimaumbile na uzuri wa nje lakini ni DHAIFU sana kwa habari ya ajenda kuu ya ndoa. Wengine kutokana na historia zao huko nyuma katika UKAHABA labda binti ana maumbile makubwa, ambayo yakiwa yamefichwa kwenye nguo hauwezi kujua lolote na wewe umekimbilia umbo wakati yupo saizi yake kabisa. Ukimlazimisha MUNGU akupe huyo sawa sawa na tamaa za moyo wako lazima ukubaliane na MATOKEO ya uamzi wako. Wakati mwingine utaambulia fedheha na MAJUTO kwasababu ulifuata hisia zako wala haukumsikiliza BWANA!

Nguo zinaficha mengi, ndiyo maana unahitaji kuomba MUNGU ili akupe HAZINA zilizositirika na kisima cha maji yatakayokuburudisha badala ya kuwa KERO. Ni hekima ya MUNGU kuficha mambo hayo kwa utukufu wake. Kimsingi mambo mengi unayoyahitaji kwa mke au mume unaweza kuyapata vizuri kabisa kwa msaada wa Roho Mtakatifu. kama ukiwa mjinga kwa ajili hili endelea kuwa mjinga lakini nakukumbusha kuwa HAZINA za THAMANI zote zimesitirika wala haziko nje kama unavyofikiri.

Uzinzi au uasherati: Shetani anajua vizuri kuwa hakuna dhambi inayomuondoa KRISTO ndani ya mtu haraka sana kama matendo yote ya zinaa, 1 WAKORINTHO 6:16-20, hivyo atakushawishi kwa kila njia hadi uingiwe na mawazo hayo machafu. Endapo utadanganyika na kufanya huo uovu, atakufanya kama alivyofanya kwa Samson na Daudi. Baada tu ya kukubali ushawishi huo tunajua vizuri yaliyofuata; Samson alitobolewa macho na kusagishwa ngano, wakati Daudi akapigwa sana katika ufalme wake hadi mtoto wake jina lake Absalom akatembea na mama zake wadogo mbele ya Israel. Chukua tahadhari tafadhali, kwa kuzingatia uhusiano wa KAKA na DADA katika WOKOVU, usipuuze ni vitu vidogo vidogo ndivyo vinavyowaangusha MASHUJAA kijinga tu

2 WAKORINTHO 12:21 "Nami nitakapo kuja tena, Mungu wangu asije akanidhili kwenu, nami nikawasikitikia wengi waliokosa tangu hapo, wasiutubie uchafu, na uasherati, na ufisadi (kufanyiza uchafu kwa kutamani, kwa kutumia mapicha ya uchi na video za ngono) walioufanya."

 ANGALIZO
Acha tabia ya KUJICHUA (Masturbation) na badala yake amua kuoa (me) kuliko kuwadanganya waokuzunguka kuwa haufanyi UASHERATI. Jambo hili linaweza kuua mishipa yako na kukufanya uangaike siku ya uhitaji kwa kuvuruga mfumo wa uzazi, kwa wanaume itapelekea kuwa na maumbile dhaifu na kushindwa kumudu tendo la ndoa kwa muda mrefu kwasababu kujichua huko ulikuwa unafanya haraka haraka sirini ili usikutilizwe na tabia hiyo ikijengeka ikaota mizizi basi ndivyo maisha yako ya ndoa yatakumbwa na changamoto na kumpa ibilisi nafasi wakati wa ndoa kwasababu ulikwisha liharibu hekalu hilo.

Kwa wamama itapelekea maumbile mapana ya uzazi yaliyozoezwa kwa vitu vigumu visivyo rasmi na kupelekea hali mbaya wakati wa ndoa. Tubia uchafu huo kisha omba rehema za MUNGU kuishinda, maana ni tatizo la kisaikolojia huwezi kushinda kwa nguvu na akili zako. Wafundishe vijana na binti zako juu ya madhara ya punyeto kujichua na uchafu mwingine kwa msisitizo na kwa upendo ili wao nao wasiende MOTONI.

☑Kama haujaoa (me) au haujaolewa (ke) usijihusishe kwa namna yeyote na mambo ya ndoa ni uasherati (WAEFESO 5:3).

☑Kwa wavulana na watoto wa shule, hakuna neno boyfriend wala girlfriend kibiblia ni ubunifu wa kuzimu wala usijaribu

☑Saizi ya mke au mume uliyeandaliwa haipimwi kwakumuingilia kimwili bali magotini katika maombi, ukifanya hivyo umedanganywa ni laana mbele za MUNGU

☑Upendo kwa mke au mume wako haumaanishi kutoka nae nje(out) mkiwa mmeshikana mikono au viuono mbele za watu wakati ndani mnaishi kama mapaka, bali uwezo wa kusameheana na kuvumiliana pindi udhaifu unapoonekana

 ☑Ndoa yenye amani ni ya watu walioridhika na vitu walivyo navyo, hivyo usiiondoe furaha katika ndoa yako kwa kujilinganisha na vitu wanavyomiliki wengine, kufanya hivyo ni kunia makuu na kuleta mafarakano na mashindano huo ni ushamba na ulimbukeni (Kumbuka kidogo alichonachomwenye haki ni bora kuliko vingi walivyo navyo wenye dhambi wengi)

☑Gari, nyumba, vyeo, elimu, nguo na uwezo wa kula unachotaka haimanishi ni msingi wa ndoa imara, hivyo acha tabia za kivulana na kisichana wala usimvunje moyo mume wako kama hana vitu hivyo badala yake muitengeneze amani na furaha isiyokoma. Mheshimu mume wako kwa nafasi aliyokupa kukuchagua wewe miongoni mwa wanawake wengi, akona wewe kuwa wa thamani kuliko wote.

YESU ANARUDI TUENDELEE KUWA ROHONI; KWAMBA ATATUKUTA TUMEKWISHA OA/KUOLEWA  VEMA, KWAMBA ATATUKUTA BADO NAPO VEMA LAKINI KATIKA MAMBO YOTE TUMPENDEZE YEYE ALIYE BWANA WETU; MAANA MBINGUNI NA KATIKA UFALME UJAO HAKUNA KUOA WALA KUOLEWA. JAMBO HILO LAFAA KATIKA MWILI HUU ILI KUISHINDA MICHOCHEO!
                   NI MIMI KAKA JOSEPH M. MARWA


Written by Zachary John Bequeker, Mwanza-Tanzania
+255625966236

Pakua App Ya Injili Halisi -Bofya Hapa Flower
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295

About INJILI HALISI MINISTRY

Zachary, most known as Zakacheka is the founder of the Injili Halisi Ministry. He is a member of Full Gospel Bible Fellowship Church.. He lives in Mwanza,Tanzania. 0621261295.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply