» » MCHUNGAJI SIJI TENA KANISANI!


Na, Ev. Zachary John Bequeker

  • Mwanamke mmoja alimwendea mchungaji wake akimwambia kuwa hatokuja tena kanisani. Mazungumzo yao yalikuwa hivi:
Mwanamke: sitakuja tena kanisani
Mchungaji: Kwanini?
Mwanamke: watu wapo kanisani wanachati, wanapiga umbeya, ni wanafiki na waongo sana wala hawaishi sawa na mafundisho ya neno la Mungu.
Kisha mchungaji akakaa kimya kwa muda kisha akaendelea……
Mchungaji: Nakuomba ufanye jambo moja kabla ya uamuzi wako wa kuacha kuja kanisani. Uko tayari?
Mwanamke: Jambo gani mchungaji?
Mchungaji: chukua glass iliyojaa maji, nenda nayo kanisani na kurudi mara mbili, hakikisha maji yake hayapungui.
Mwanamke: Sawa, naweza kufanya!
Mchungaji: Sawa, fanya ukimaliza rudi.
Baadaye yule mwanamke akarudi………….
Mwanamke: Mchungaji, tayari nimerudi.
Mchungaji: Ulipoenda, ulimwona mtu yeyote anachati? Ulimwona mtu yeyote akipiga umbeya? Ulimwona mtu yeyote mavazi yake na Matendo yake hayako sawa na neno la Mungu?
Mwanamke: Hapana, sikuona chochote kwa sababu akili yangu yote na macho yangu yalikuwa yakiiangalia glass ili maji yasimwagike.
Mchungaji: Umenena vyema kabisa, unapokuja kanisani unapaswa umwangalie Mungu pekee na kwa namna hiyo hautaanguka. Kwa sababu hiyo Yesu Kristo alisema ‘NIFUATE’ wala hakusema tumfuate mkristo mwenzako, mchungaji wako, nabii fulani, askofu fulani, Mwinjilisti fulsni au mtume fulani. Usiruhusu uhusiano wako na Mungu ukawa kwa namna wengine wanavyoishi bali ishi kama jinsi Mungu anavyotaka uishi. Tunamfuata mtu kama anaenenda sawasawa na neno la Mungu, Paulo akasema “Nifuateni mimi kama mimi ninavyomfuata Kristo”. Maana yake hata kama ni mimi mchungaji wako sienendi sawa na neno la Mungu, hupaswi kunifuata. Kumbuka wanadamu hawana mbingu, mwenye mbingu ni Mungu pekee na ndiye aliyeweka vigezo vya kuingia mbinguni ambavyo ni utakatifu(Waebrania 12:14) na huo utakatifu unapatikana katika neno la Mungu(Yohana 17:17). Lifuate neno, usiwafuate waitwao wakristo.
Ukweli wa Biblia
Zaburi 37:37 “Umwangalie sana mtu mkamilifu, Umtazame mtu mnyofu, Maana mwisho wake mtu huyo ni amani”
Isaya 45:22 “Niangalieni mimi, mkaokolewe, enyi ncha zote za dunia; maana mimi ni Mungu; hapana mwingine.”
Waebrania 12:14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;”
Yohana 17:17 “Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli.”
Yohana 1:1 “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.”
1 Petro 1:15 “bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;”
Yohana 15:3 "Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia."
...............................................

Je, unataka kuokoka?
Tuma neno "NATAKA KUOKOKA" kwa SMS au WhatsApp kwa +255625966236

Facebook Group: Inili Halisi Ministry

KWA MAFUNDISHO TEMELEA:
🔗zakachekainjili.blogspot.com
💕 Sharing is Caring💓

Pakua App Ya Injili Halisi -Bofya Hapa Flower
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295

About INJILI HALISI MINISTRY

Zachary, most known as Zakacheka is the founder of the Injili Halisi Ministry. He is a member of Full Gospel Bible Fellowship Church.. He lives in Mwanza,Tanzania. 0621261295.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

1 Post a Comment:

  1. Slot machine games - JTM Hub
    If you like playing online 안양 출장안마 slots, you should be interested in getting the 광주광역 출장마사지 best experience. You can 진주 출장안마 also 공주 출장안마 use the free demo mode and the software Mar 24, 2019 안산 출장안마 · Uploaded by SlotmachineGames

    ReplyDelete