» » CHUKUA VYOTE NIACHIE YESU



Unapoimba wimbo wa ‘’chukua vyote niachie Yesu” si kwamba unamruhusu shetani kufanya lolote juu ya maisha yako bali unamtangazia kwamba lolote atakalolifanya hawezi kukuondoa katika imani, lolote analolifanya haliwezi kukufanya uondoe imani yako kwa Yesu, lolote analolifanya ili umkane Yesu huwezi kumkana kamwe.

Shedraki, Meshaki na Abednego walijua kwamba pamoja na magumu yanayoenda kuwapata, pamoja na kutupwa katika tanuru la moto, hawatamkana Bwana. Walipotupwa Bwana alionekana akiwa anatembea nao katika moto ule.

Danieli alikuwa tayari kufa kwa ajili ya kusimamia kile alichokuwa akikiamini, hakuwa tayri kumwabudu mfalme, hakuwa tayari kuendeshwa na kanuni na taratibu zilizo kinyume na mapenzi ya Mungu. Kwa jinsi hiyo, Mungu aliingilia kati na hata kupitia yeye, Mfalme na watu wake wakamkubali Mungu wa Danieli.

 Ayubu pia, pamoja na mazito yaliyompata hakuwa tayari kumkana Bwana. Shetani alichukua watoto wake na mali zake zote lakini hakuwa tayari kumkana Bwana bali alisema ‘pamoja na mwili huu nitamwona Bwana’ alijua pamoja na magumu anayoyapitia, pamoja na afya yake kuwa mbaya, pamoja na mwili wake kuharibiwa na kukonda, hawezi kumuacha Bwana kwa maana hata akifa ataishi milele na milele Mbinguni ambako ndiko atamuona Bwana uso kwa uso.

Yusufu naye pia hakuwa tayari kumuudhi Mungu kwa ajaili ya kumfurahisha mke wa bosi wake. Yusufu alikuwa tayari kukimbia akiwa uchi, alikuwa tayari kuachishwa kazi, alikuwa tayari kufungwa, kuliko kufanya uchafu na kahaba yule mkewe Potifa. Yusufu pamoja na hayo yote hakumuacha Bwana na mwisho wake ulikuwa mkuu.

Kumbuka Mungu anaweza kumruhusu Shetani akujaribu au shetani mwenyewe anaweza akakujaribu bila kujali unaimba wimbo huu au la!

Kukataa wimbo huu ni kumtangazia shetani kwamba wewe unategemea vitu na endapo ataviondoa utamuacha Bwana, kwa jinsi hii lazima upigwe.

Kumbuka unapoimba wimbo huu unamtangazia shetani kwamba huwezi kumuacha Bwana pamoja na changamoto za maisha unazozipitia.

Hitimisho: Unapoimba wimbo huu unamtangazia shetani kwamba pamoja na changamoto za maisha unazozipitia hauwezi kumkana Yesu kamwe. Ulikuwa umechumbiwa baadaye mchumba akakuacha usimwache Yesu, mwambie pamoja na kumnyakua mchumba wangu sitamuacha Yesu. Umeoa/umeolewa mwezi wako kakuacha, nawe vivyo hivyo mtangazie shetani kuwa hauwezi kumkana Yesu. Ni biashara imeyumba, mali kupukutika, nawe pia mdhihirishie shetani kwamba pamoja na hayo bado utaendelea na Yesu. Na kwa jinsi hii mwishoni utaibuka mshindi kama Shedraki, Meshaki, Danieli na Yusufu katika jina la Yesu.

Pakua App Ya Injili Halisi -Bofya Hapa Flower
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295

About INJILI HALISI MINISTRY

Zachary, most known as Zakacheka is the founder of the Injili Halisi Ministry. He is a member of Full Gospel Bible Fellowship Church.. He lives in Mwanza,Tanzania. 0621261295.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply