Goliathi na Daudi |
I Samweli 17:31-40 inasema kwamba Daudi mwana wa Yese
hakutaka kuvaa mavazi ya kivita na badala yake alichukua mawe matano ili kumuua
Goliathi.
Kwanini Daudi alitumia mawe matano ili kumuua Goliathi? Je, Daudi alimuogopa Goliathi? Jibu ni Hapana!
Kumbuka Daudi alikuwa tayari alishaua dubu na simba kwa mikono yake mwenyewe.
Kwa hiyo kama alikuwa anauwezo huo basi alikuwa ni mzoefu sana na mtu mwenye
mbinu nyingi kwa habari ya kukabiliana na adui.
Daudi alikuwa akitokea katika ukoo wa Yuda. Alikuwa ameandaliwa
vyema katika utumiaji wa kombeo wala hakuhitaji mawe mengi.
Waamuzi 20: 15-16 ‘’Hao wana wa
Benyamini walihesabiwa siku ile kutoka hiyo miji, watu waume ishirini na sita
elfu waliotumia upanga, zaidi ya hao waliokaa Gibea, ambao walihesabiwa watu
wateule mia saba. Katika watu hao wote walikuwako watu waume mia saba
waliochaguliwa, wenye shoto; kila mmoja alikuwa anaweza kuutupia unywele mawe
kwa teo, wala asikose.’’
Unaposoma katika 2 Samweli 21:15-22 na 1 Mambo ya
Nyakati 20:1-8 Tunaweza kukwambia kwamba Goliathi alikuwa na ndugu wanne, (Yeye
alikuwa wa tano) Ishbi-Benobu, Safu, Lahmi, na jitu “Huge
man”. Wote hawa walikuwa ni
majitu(giants) ambao walikuwa ni wana wa jitu lililoitwa Mrefai lililoishi Gathi.
Mrefai kwa biblia
ya kiingereza inaandikwa Rapha
ambayo kwa kiebrania inamaanisha GIANT yaani
jitu kubwa, pandikizi (2 Samweli 21:22), Mrefai aliishi Gathi akiwa na vijana
watano (1 Nyakati 20:8): Goliathi (1 Samweli 17:23), Ishbi-Benobu(2 Samweli
21:16), Safu (1 Mambo ya Nyakati 20:4), Lahmi (1 Mambo ya Nyakati 20:5), na “jitu kubwa”,
Ambaye aliuliwa na askari wa Daudi huko Gathi (2 Samweli 21:20, 1 Mambo ya
Nyakati 20:6). Mtu huyu alikuwa ni hatari kwa sababu alikuwa ana vidole
sita miguuni na mikononi.
Kulingana na kanuni na sheria za Israeli, sheria ya vita ilitaka wapiganaji
vita hodari wote kuingia katika vita na kulinda mipaka yao. Hii inadhihirisha kwamba si Goliathi pekee
aliyekuwa akiliwakilisha jeshi la Wafilisti katika bonde la Ela siku ya
mapigano dhidi ya wapinzani wao bali pia na ndugu zake wane walikuwa pamoja
naye.
Goliathi hakuwa ametahiriwa. Goliathi alikuwa na ndugu wanne
ambao hawakutahiriwa pia.
Inaonesha kwamba Daudi hakuwa pale ili kumuua Goliathi pekee bali na ndugu zake wanne pia.
Hitimisho: " Naye Daudi akajifunga upanga juu ya mavazi yake, akajaribu
kwenda; maana alikuwa hajavijaribu. Daudi akamwambia Sauli, Siwezi kwenda na
vitu hivi, maana sikuvijaribu. Basi Daudi akavivua. Akaichukua fimbo yake
mkononi, akajichagulia mawe laini matano katika kijito cha maji, akayatia
katika mfuko wa kichungaji aliokuwa nao, maana ni mkoba wake, na kombeo lake
alikuwa nalo mkononi mwake, akamkaribia yule Mfilisti." (1 Samweli
17:39-40).
Labda Daudi alichukua mawe matano kumuua Goliathi kwa sababu alikuwa na
ndugu zake watano. Katika tamaduni za kale, kulikuwa na tabia iliyoitwa
malipizo ya damu "blood revenge." Kama mtu alimjeruhi mtu
fulani, baadaye ndugu wa mtu yule aliyejeruhiwa walikuja kufanya malipizo kwa
adui. Hivyo Daudi alijua kama atamuua Goliathi na lazima ndugu zake wataingilia
kati ili kulipiza kisasi, hivyo alijiandaa pia kupambana nao.
" Kulikuwa na vita tena huko Gathi; ambako
kulikuwa na mtu mrefu sana, mwenye vidole sita katika kila mkono, na vidole
sita katika kila mguu, jumla yake ishirini na vinne; yeye naye alizaliwa kwa
Mrefai. Naye huyo alipowatukana Israeli, ndipo Yonathani, mwana wa Shama,
nduguye Daudi, akamwua. Hao wanne walizaliwa kwake huyo Mrefai wa Gathi;
wakaanguka kwa mkono wa Daudi, na kwa mikono ya watumishi wake." (2 Samweli 21:20-22).
Je, unataka kuokoka?
Tuma neno "NATAKA KUOKOKA" kwa SMS au WhatsApp kwa +255625966236
Tuma neno "NATAKA KUOKOKA" kwa SMS au WhatsApp kwa +255625966236
Facebook Group: Injili Halisi Ministry
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295
No comments: