Ulimwenguni kuna
mambo mengi yanayoweza kumkosesha mtu au kuwakosesha watu.
Pamoja na kwamba
hayana budi kuja lakini ni ole kwake ayaletaye.
MATHAYO 18:7 “7
Ole ni wa ulimwengu kwa sababu ya mambo
ya kukosesha! Maana hayana budi kuja mambo ya kukosesha; lakini ole wake mtu
yule aliletaye jambo la kukosesha!”
Mfano wa mambo
yanayoweza kukosesha ni mafundisho potofu, mavazi, malezi mabaya, mazungumzo mabaya na hata chakula pia. Hebu
tuanze na moja baada ya jingine.
1. Mafundisho
potofu humfanya mtu
aamini uongo na kuufata na hatima yake huishia kupotea kwa sababu ni uongo.
Biblia inatoa onyo juu ya wahubiri au walimu wafundishao upotofu kwa tamaa zao
wenyewe.
2. Mavazi wanayovaa hasa wanawake wa leo ni
mavazi yanayowavuta vijana kufanya uzinzi/uasherati. Wanawake inawapasa mvae
mavazi yatakayowaokoa wanaume kuvutwa na tama kisha kutenda dhambi na hatimaye
kupata hukumu.
3. Malezi
mabaya: Biblia inasema
katika MITHALI
22:6 “Mlee mtoto katika njia
impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.” Kumbe mzazi au mlezi unanafasi
kubwa ya kumpoteza mwanao. Mlee katika misingi sahihi ili asipotee.
4. Maneno yako yanaweza kuwakosesha wengine wakajikuta wamefanya mambo yasiyo
stahili. Maneno ya uongo yanaleta hasira, chuki, kinyongo, fitina na hata
visasi. Kwa mtu uliyemsababishia kinyongo au hasira maana yake umemkwaza,
umemkosesha na kwa namna hiyo anahesabiwa katenda dhambi na kama mtu huyo
atakufa katika dhambi hiyo damu yake itatakwa kwako.
5. Chakula: unaweza kuwakwaza watu kwa chakula.
Mathalani wewe unapenda nyama fulani na mkeo au mmeo hapendi kabisa kuiona au
kuigusa nyama hiyo jambo la kufanya ni kwamba, kwa kuwa wewe unaipenda sana
nyama hiyo au chakula hicho nenda mahali wanapouza nunua, tumia kisha rejea
nyumbani na usitumie mbele ya mmeo/mkeo asiyekula nyama/chakula hicho kwani kwa
kufanya hivyo unaleta makwazo bila sababu ya msingi. Biblia imeweka wazi kabisa
suala hili. Ukisoma katika WARUMI
14:14-23 inasema “14 Najua, tena nimehakikishwa sana katika Bwana Yesu, ya kuwa
hakuna kitu kilicho najisi kwa asili yake, lakini kwake yeye akionaye kitu kuwa
najisi, kwake huyo kitu kile ni najisi. 15 Na ndugu yako akiingia huzuni kwa sababu ya chakula,
umeacha kwenda katika upendo. Kwa chakula chako usimharibu mtu yule ambaye
Kristo alikufa kwa ajili yake.16 Basi, huo wema wenu usitajwe kwa ubaya.17 Maana ufalme wa Mungu si
kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu.18 Kwa kuwa yeye
amtumikiaye Kristo katika mambo hayo humpendeza Mungu, tena hukubaliwa na
wanadamu.19
Basi kama ni hivyo, na mfuate mambo ya amani na mambo yafaayo kwa kujengana. 20 Kwa ajili ya chakula
usiiharibu kazi ya Mungu. Kweli, vyote ni safi; bali ni vibaya kwa mtu alaye na
kujikwaza. 21
Ni vyema kutokula nyama wala kunywa divai wala kutenda neno lo lote ambalo kwa
hilo ndugu yako hukwazwa. 22 Ile imani uliyo nayo uwe nayo nafsini mwako mbele za
Mungu. Heri mtu yule asiyejihukumu nafsi yake katika neno lile analolikubali.23 Lakini aliye na shaka,
kama akila, amehukumiwa kuwa ana hatia, kwa maana hakula kwa imani. Na kila
tendo lisilotoka katika imani ni dhambi.”
Pia 1 WAKORINTHO 10:31-32
inafafanua zaidi “31 Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni
yote kwa utukufu wa Mungu. 32 Msiwakoseshe
Wayahudi wala Wayunani wala kanisa la Mungu,” Kumbe
hatupaswi kuwakosesha wengine kwa chakula hata vinywaji wasivyovitumia.
LUKA 17:1 “1
Akawaambia wanafunzi wake, Makwazo
hayana budi kuja, lakini ole wake mtu yule ambaye yaja kwa sababu yake!“
NB: Pamoja na
kuwako mambo yakoseshayo, ewe kaka ewe baba usikubali kuvutwa kwenye uasherati
au uzinzi. Ewe dada ewe mama usikubali mazingira kukufanya umuache Mungu, iwe
ni kazini boss wako anataka kufanya uasherati au uzizinzi na wewe ili upate
kazi, cheo n.k……. Usikubali jambo lolote
likutenge na upendo wa Kristo. (WARUMI 8:35)
Ni ole kwako wewe
uletaye makwazo/mambo ya kukosesha.
GROUP LA FACEBOOK: INJILI HALISI MINISTRY
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295
No comments: