» » KUTOFAUTIANA MAJINA YA WANAFUNZI WA YESU



Kuna aina nne tofauti za orodha ya wanafunzi wa Yesu zinazotajwa katika biblia. Wakati mwingine majina yao yanatofautiana katika 
mpangilio, lakini hili si tatizo kwa sababu bado majina hayo 
yanabaki yanaonesha kuwa ni wanafunzi 12. Katika Mathayo, Marko na Luka majina ya wanafunzi yako 12 isipokuwa kitabu cha Matendo ya Mitume kina jumla ya wanafunzi 11 tu. Hii ni kwa sababu Yuda Iskariote aliyemsaliti Yesu alikuwa amekwisha kufa hivyo hakuorodheshwa. Matendo 1:21-26 inaonesha jinsi Mathiya alivyowekwa kukamata nafasi ya Yuda Iskariote na wakawa wanafunzi 12 tena.

Kama unavyoona katika orodha hapo chini, wanafunzi wa Yesu waliorodheshwa kwa kufanana isipokuwa mmoja tu ndio analeta mkanganyiko kwa wengi, ambaye anaonekana sehemu moja na sehemu nyingine haonekani. Katika Mathayo na Marko tunamuona Thadayo lakini katika Luka na Matendo hatumuoni. Pia katika Luka na Matendo tunamuona Yuda mwana wa Yakobo ambapo haonekani katika Mathayo na Marko.

Thadayo na Yuda mwana wa Yakobo ni jina la mtu mmoja. Kwa kuwa Yuda mwana wa Yakobo alikuwa akichangia jina moja na Yuda Iskariote aliyemsaliti Yesu, kuna uwezekano mkubwa aliitwa Thadayo ili kuwatofautisha.

Ni kawaida katika biblia kukuta mtu ana majina mawili au zaidi. Kwa mfano katika Matendo 1:23 tunamuona mtu mmoja aliyeitwa Yusufu aitwaye Barsaba, aliyekuwa na jina la pili Yusto.

Hii hapa ni orodha ya wanafunzi wa Yesu 

Mathayo 10:2-4
Marko 3:13-19
Luka 6:12-16            
Matendo 1:13-14
1.      Simoni  (Petro)
Simoni  (Petro)

Simoni  (Petro)
Simoni  (Petro)
                                                               
2.        Yakobo wa Zebedayo

 


3.      Yohana nduguye Yakobo


  Yakobo wa Zebedayo



Yohana nduguye Yakobo

Yakobo wa Zebedayo




Yohana nduguye Yakobo

Yakobo wa Zebedayo




Yohana nduguye Yakobo


4.      Andrea


Andrea


Andrea

Andrea
5.      Filipo

Filipo

Filipo

Filipo

6.      Bartholomayo

 


7.      Mathayo

Bartholomayo


Mathayo
Bartholomayo


Mathayo
Bartholomayo


Mathayo
8.      Tomaso

Tomaso

Tomaso

Tomaso

9.      Yakobo wa Alfayo

Yakobo wa Alfayo

Yakobo wa Alfayo
Yakobo wa Alfayo
10.  Thadayo

Thadayo


-------------------

-------------------
11.  Simoni Mkananayo

Simoni Mkananayo

Simoni Mkananayo

Simoni Mkananayo

12.  Yuda Iskariote

Yuda Iskariote

Yuda Iskariote

Nafasi hii ilikamatwa na Mathiya baada ya Yuda Iskariote kufariki


--------------------

        --------------------
 Yuda wa Yakobo
Yuda wa Yakobo

Pakua App Ya Injili Halisi -Bofya Hapa Flower
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295

About INJILI HALISI MINISTRY

Zachary, most known as Zakacheka is the founder of the Injili Halisi Ministry. He is a member of Full Gospel Bible Fellowship Church.. He lives in Mwanza,Tanzania. 0621261295.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply