Moja
ya swali linaloulizwa na wakristo wengi ni, Je, Yuda alienda Mbinguni au
Jehanum?
Biblia
imeweka wazi kwamba Yuda Iskariote aliyemsaliti Yesu sasa yuko motoni. Yuda
Iskariote hakuwa ameokoka ingawa alihuzunika kabla ya kwenda kujinyonga lakini
hakutubu.
Mungu hakumuumba Yuda
ili aje kumsaliti Yesu, lakini alijua kwamba atafanya hivyo. Kumbuka hata leo
kuna baadhi ya watu wasio wakristo halisi wa leo hii wanalitumia jina la Mungu ili kujipatia pesa
na naamini hata Yuda pia alimtumia Yesu ili kujipatia pesa pekee wala hakuwa na
mpango naye (Yohana 10:28).
Zifuatazo ni sababu
zinazothibitisha kwamba Yuda hakwenda Mbinguni:-
1. Yuda alikuwa ni mwizi
mwenye tamaa, alimsaliti Yesu kwa ajili ya pesa!
Yohana 12:4-6 “Basi Yuda Iskariote, mmojawapo wa
wanafunzi wake, ambaye ndiye atakaye kumsaliti, akasema, Mbona marhamu hii
haikuuzwa kwa dinari mia tatu, wakapewa maskini? Naye aliyasema hayo, si kwa
kuwahurumia maskini; bali kwa kuwa ni mwivi, naye
ndiye aliyeshika mfuko, akavichukua vilivyotiwa humo.
1 Wakorintho 6:9-10 “Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi
ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala
waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala
wanyang'anyi.”
Mathayo 26:14-16 “Wakati huo mmoja wa wale Thenashara, jina
lake Yuda Iskariote, aliwaendea wakuu wa makuhani, akasema, Ni nini mtakachonipa, nami nitamsaliti kwenu? Wakampimia vipande thelathini vya fedha.Tokea wakati huo akawa akitafuta nafasi apate
kumsaliti.”
Luka 16:13 “Hakuna mtumishi awezaye kutumikia mabwana wawili…..Hamwezi
kumtumikia Mungu na mali.”
2. Yuda alikuwa ameokoka?
Hapana, Shetani alimuingia. Mkristo halisi hawezi kuvamiwa na mapepo!
Yohana 13:27-30 “Na baada ya hilo tonge Shetani alimwingia. Basi Yesu akamwambia, Uyatendayo yatende upesi. Wala hakuna mtu katika wale walioketi chakulani aliyeijua
sababu ya kumwambia hivyo. Kwa maana wengine walidhania, kwa kuwa Yuda huchukua
mfuko, ya kwamba Yesu alimwambia kama, Nunua mnavyovihitaji kwa sikukuu; au
kwamba awape maskini kitu. Basi huyo, akiisha kulipokea lile tonge, akatoka mara hiyo. Nako kulikuwa ni
usiku.”
1
Yohana 5:18 “Twajua ya kuwa kila
mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi; bali yeye aliyezaliwa na Mungu hujilinda, wala yule mwovu
hamgusi.”
3. Yesu alimuita Yuda kuwa
amemchagua akiwa ni ‘Shetani’!
Yohana 6:70 “Yesu akawajibu, Je! Mimi sikuwachagua ninyi Thenashara, na mmoja wenu ni shetani?”
4.Yesu alitambua kuwapo
kwa Yuda duniani ilikuwa ni hasara kawke Yuda mwenyewe
Mathayo 26:20-24 “Basi kulipokuwa jioni aliketi
chakulani pamoja na wale Thenashara. Nao
walipokuwa wakila, alisema, Amin, nawaambia, Mmoja wenu atanisaliti. Wakahuzunika sana, wakaanza kumwuliza mmoja
mmoja, Ni mimi, Bwana? Akajibu akasema, Yeye aliyetia mkono wake pamoja nami
katika kombe, ndiye atakayenisaliti. Mwana wa Adamu aenda zake, kama
alivyoandikiwa; lakini ole wake mtu yule
ambaye amsaliti Mwana wa Adamu! Ingekuwa heri kwake mtu yule kama
asingalizaliwa.”
5. Yuda alikuwa ndiye
mchafu kati ya wanafunzi wa Yesu. Hakuwa amesamehewa dhambi zake.
Yohana 13:8-11 “Petro akamwambia, Wewe
hutanitawadha miguu kamwe. Yesu akamwambia, Kama nisipokutawadha, huna shirika
nami. Simoni Petro akamwambia, Bwana, si miguu yangu tu, hata na mikono yangu
na kichwa changu pia. Yesu akamwambia, Yeye aliyekwisha kuoga hana haja ila ya
kutawadha miguu, bali yu safi mwili wote; nanyi mmekuwa safi, lakini si
nyote. Kwa maana alimjua yeye atakayemsaliti; ndiyo maana alisema, Si nyote
mlio safi.”
6. Yuda hakumwamini wala hakumjua
Yesu kuwa ni nani
Ingawa Yuda
alihuzunika kwa kumsaliti Yesu, hakuamini kuwa Yesu alikuwa ni nani hasa.
Yohana 6:64-65 " Lakini kuna
wengine miongoni mwenu wasioamini. Kwa maana Yesu alijua
tangu mwanzo ni nani wasioamini, naye ni nani atakayemsaliti.
Akasema, Kwa sababu hiyo nimewaambia ya kwamba hakuna mtu awezaye kuja kwangu
isipokuwa amejaliwa na Baba yangu.”
HITIMISHO: Kutokana na maandiko,
tunahitimisha kwamba, Yuda hakuwa mwamini wa kweli katika Kristo (Yohana 6:64), kwa sababu hiyo aliingiwa na Shetani na hali hii inaonesha ni jinsi
gani hali yake ya kiroho ilivyokuwa mbaya (Yohana 13:27), pamoja na kujuta
baada ya kumsaliti Yesu lakini hakutubu na Yesu alisema heri asingezaliwa mtu
aakaye msaliti, maana yake kuzaliwa kwake hakukuwa na faida (Mathayo
26:24; Marko 14:21).
Kwa hiyo, tunahitimisha kwa kusema Yuda
alienda Jehanum.
GROUP LA FACEBOOK: INJILI HALISI MINISTRY
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295
No comments: