» » JE, ADAMU NA EVA WALIFANYA DHAMBI YA UZINZI?

Na Kaka Zachary +255 625 966 236

Jibu ni kwamba, Adamu na Hawa hawakufanya dhambi ya uzinzi wala uasherati. Mungu aliwaumba Adamu na Hawa na si tu kwamba aliwapa uwezo na uhuru wa  kufanya tendo la ndoa bali Mungu mwenyewe ndiye aliyewaagiza wafanye tendo la ndoa.

Mwanzo 1:27-28Mungu akaumba mtu kwa mfano wake,……. mwanamume na mwanamke aliwaumba. Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.”

Mungu mwenyewe aliwabarikia akawaambia wazae ili waongezeke na kuijaza nchi na wote tunafahamu kwamba viumbe hai huongezeka kwa kuzaliana. Binadamu hawawezi kuzaliana bila tendo la ndoa tena mwanamke na mwanamume. Mwanamume kwa mwanamume au mwanamke kwa mwanamke hapo hakuna kuzaliana, ndio maana Adamu alipewa Hawa mwenye jinsia tofauti na yeye ili tendo la ndoa lifanyike na watu waongezeke kwa kuzaliwa.

Adamu na Hawa walipata mtoto wao wa kwanza baada ya tendo la ndoa.                                         Mwanzo 4:1 “ Adamu akamjua Hawa mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Kaini”
Kosa walilolifanya Adamu na Hawa ni kutotii kile walichoagizwa na Mungu na badala yake wakamtii shetani. Mungu aliwapa uhuru wa kula matunda yoooote katika bustani isipokuwa mmoja tu. Na aliyepewa agizo hilo alikuwa ni Adamu kabla Hawa hajaumbwa. Ndio maana shetani aliona njia rahisi ni kumtumia Hawa ambaye hakulipokea agizo hilo moja kwa moja kutoka kwa Mungu bali aliambiwa na mmewe, Adamu. Kumbuka pia kwamba aliyeanza kula alikuwa ni Hawa ndipo akampelekea na Adamu akala. Hapa inaonesha kipindi Hawa akidanganywa na shetani Adamu hakuwa karibu na Hawa.

 Mwanzo 2:15-17 “Bwana Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza. Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.”
Kumbuka walipokuwa katika bustani ya Edeni hawakuwa wamevaa mavazi, walikuwa uchi lakini hawakuona kuwa ni tatizo pamoja na kwamba Mungu alikuwa akiwatembelea kila siku (Mwanzo 2:25).

Kwanini walijiona wako uchi? 
Walijiona wako uchi baada ya kutenda dhambi. Biblia inamtaja mtu mwenye dhambi kuwa ni mtu aliye uchi.

Mwanzo 2:4-7 “……..Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.”

Tangia hapo wakawa wametengwa na Mungu kiroho na ndipo Mungu alipowaondoa katika bustani ya Edeni. Kabla ya kuondolewa katika bustani ya Edeni hakukuwa na kifo bali kifo kilikuja baada tu ya kutenda dhambi Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti (Warumi 6:23).

Hitimisho: Adamu na Hawa hawakufanya uasherati wa uzinzi kwa sababu walikuwa ni mke na mume. Na Mungu mwenyewe ndiye aliyewaagiza wazaliane na ili kuzaliana lazima kufanya tendo la ndoa. Tendo la ndoa hufanywa na wana ndoa wote wawili kwa wakati mmoja na si kama hapo tulipoona Hawa alianza kula kisha akampatia na Adamu. Adamu na Hawa walikula tunda halisi kutoka katika mmea wa mti.                                                                                                   
Adamu na Hawa walikuwa ni mke na mme, yaani walikuwa ni wana ndoa na tendo la ndoa ni halali kwa wana ndoa Mwanzo 3:17 “Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale…”      

INJILI HALISI MINISTRY:    
    images-8.jpg+255625966236     youtube-512.png Zachary John Bequeker

KWA MAFUNDISHO ZAIDI BOFYA HAPA è zakachekainjili.blogspot.com 


Pakua App Ya Injili Halisi -Bofya Hapa Flower
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295

About INJILI HALISI MINISTRY

Zachary, most known as Zakacheka is the founder of the Injili Halisi Ministry. He is a member of Full Gospel Bible Fellowship Church.. He lives in Mwanza,Tanzania. 0621261295.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply