Na, Ev. Zachary John Bequeker
Ni muhimu kuelewa kuwa kuna kitabu kimoja cha uzima na kuna vitabu vingi vya hukumu.UFUNUO 20:11-12 “…Vitabu vikafunguliwa na kitabu kingine kikafunguliwa ambacho ni cha uzima….”
KWA NINI KUNA KITABU KIMOJA TU CHA UZIMA NA VITABU VYA HUKUMU NIVINGI?
Ni vyema kufahamu kwamba wanao pata nafasi ya kuokoka niwachache, na wanao ishi sawasawa na mapenzi ya Mungu ni wachache MATHAYO 7:13-14 “…..na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache” , LUKA 13:23-24 “23 Mtu mmoja akamwuliza, Je! Bwana, watu wanaookolewa ni wachache? Akawaambia, 24 Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.”
NB: Kuna mafundisho ya Uongo,wakisema eti mtu akiamini Yesu yupo na akiokoka hata akifanya dhambi hamna shida Mbinguni anaingia tu,huku wakitumia maandiko na kutafsiri visivyo kama YOHANA 3:16,18,36 “…….kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele…Amwaminiye yeye hahukumiwi;....... Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele…”
Na kusema hakuna hukumu juu ya wanaoenda kanisani hata kama ni watenda dhambi WARUMI 8:1 “ hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.” .
Suala la kwenda kanisani si sababu, Je, unayaishi yale unayojifunza?kwa maana neno ni sauti ya MUNGU isemayo nawe na mtu hahesabiwi haki kwa kusikia sheria bali huhesabiwa haki kwa kuitenda WARUMI 2:13 “…sio wale waisikiao sheria walio wenye haki mbele za Mungu, bali ni wale waitendao sheria watakaohesabiwa haki.” Hivyo basi wanao pata uzima wa milele ni wale wanalisikia neno la Mungu na kulitenda YOHANA 10:27-28 “Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata. 28 Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea….”. Kumwamini Yesu tu hakutoshi wala si kwa kumwamini kama sisi tujuavyo neno “AMINI’’ Hapana hapa lina maana anayeamini ni yule anayempenda na kumfuata kwa yote asemayo kwasababu anamwamini 1 YOHANA 5:3-5 “Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito. 4 Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu. 5 Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, isipokuwa ni yeye aaminiye ya kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu?”.
YOHANA 5:38 “Wala neno lake hamnalo likikaa ndani yenu, kwa kuwa ninyi hammwamini yule aliyetumwa na yeye”
Na tunaweza kusema tunampenda Yesu kama tunazishika amri zake YOHANA 14:15,23-24 “Mkinipenda, mtazishika amri zangu…Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.24 Mtu asiyenipenda, yeye hayashiki maneno yangu; nalo neno mnalolisikia silo langu, ila ni lake Baba aliyenipeleka..”
1 YOHANA 2:3-6 “3 Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake. 4 Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake. 5 Lakini yeye alishikaye neno lake, katika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli. Katika hili twajua ya kuwa tumo ndani yake.6 Yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani yake, imempasa kuenenda mwenyewe vile vile kama yeye alivyoenenda.”
JE, NI AKINA NANI WALIO KATIKA KITABU CHA UZIMA?
Mtu anapookoka jina lake hufutwa katika vitabu vya hukumu na huwa linaandikwa katika kitabu cha uzima kwa maana hiyo walio katika kitabu cha uzima ni wale waliotubu dhambi zao na kumaanisha kuziacha (MITHALI 28:13) na ni wale wanao dumu katika utakatifu bila kukengeuka (WAFILIPI 4:3, WAEBRANIA 12:23, LUKA 10: 20) Wanafunzi wa Yesu majina yao yalikuwa yameandikwa Mbinguni.
NB:Mtu aliye okoka akitenda dhambi jina lake hufutwa na kuandikwa tena katika vitabu vya hukumu, Musa alilijua hilo KUTOKA 32:33 “32 Walakini sasa, ikiwa utawasamehe dhambi yao - na kama sivyo, unifute, nakusihi, katika kitabu chako ulichoandika.33 Bwana akamwambia Musa, Mtu ye yote aliyenitenda dhambi ndiye nitakayemfuta katika kitabu changu.”Adumuye katika wokovu bila yeye kukengeuka jina lake halifutwi bali hubaki katika kitabu cha uzima UFUNUO 3:5 “5 Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitalikiri jina lake mbele za Baba yangu, na mbele ya malaika zake.”
JE, NI AKINA NANI WALIO KATIKA VITABU VYA HUKUMU?
Wote watendao dhambi majina yao huwa katika vitabu vya hukumu. Kwa sababu watendao dhambi wastahili hukumu.hata kama anasema kuwa ameokoka lakini anatenda dhambi hataingia na hata kama anajiita yeye ni mtumishi wa Mungu , kwani majina yao hayataandikwa katika kitabu cha uzima wala hawataingia. Hata kama walitenda mema mengi lakini wakatenda dhambi moja tu hufutwa yale mema yote na kufanya majina yao kuandikwa katika vitabu vya hukumu EZEKIELI 18:4,24 "4 Tazama, roho zote ni mali yangu; kama vile roho ya baba ni mali yangu, ndivyo ilivyo roho ya mwana mali yangu; roho ile itendayo dhambi itakufa. 24 Bali mwenye haki atakapoghairi, na kuiacha haki yake, na kutenda uovu, na kufanya machukizo yote kama yale afanyayo mtu mwovu, je, ataishi? Katika matendo yake yote ya haki aliyoyatenda halitakumbukwa hata mojawapo. Katika kosa lile alilolikosa, naam, katika dhambi yake aliyoitenda, atakufa." WAEBRANIA 10:26-27 “26 Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi; 27 bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao.”.
Lakini mwenye dhambi hata kama ni nyingi kiasi gani akighairi na kutubu, husamehewa na jina lake hufutwa katika vitabu vya hukumu na huandikwa katika kitabu cha uzima EZEKIELI 18: 21-22 “21 Lakini mtu mbaya akighairi, na kuacha dhambi zake zote alizozitenda, na kuzishika amri zangu zote, na kutenda yaliyo halali na haki, hakika ataishi, hatakufa.22 Dhambi zake zote alizozitenda hazitakumbukwa juu yake hata mojawapo; katika haki yake aliyoitenda ataishi.”
JE, NINI CHA KUFANYA?
Kama bado hujaokoka, tubu dhambi zako kwa kumaanisha kuziacha ili jina lako lifutwe katika vitabu vya hukumu na liandikwe katika kitabu cha uzima wa milele. Na hata kama umeokoka ni vyema kujijengea tabia ya kutubu mara kwa mara, hata pale wewe unapoona hujatenda dhambi , kwa sababu pasipo kujua wakati mwingine tunatenda dhambi, wala tusijihesabie haki na kuona kuwa tumekwisha kuwa wakamilifu (WAFILIPI 3: 12-16). Tusiwe kama hawa waliojihesabia haki kwa kutoa pepo na kuponya wagonjwa hali majina yao yakiwa yameshafutwa katika kitabu cha uzima pasipo wao kujua. Ni muhimu kujua hata kwa mawazo yetu tu twaweza kumtenda Mungu dhambi (MATHAYO 7:21-22). Kutotenda mapenzi ya Mungu ni dhambi (YAKOBO 4:17). Tusifanye dhambi kwa lengo la kutubu baadae, hivyo twafanya dhambi kusudi na matokeo yake ni hukumu (WAEBRANIA 10: 26-27, 1YOHANA 3:8-9). Kwa hiyo tunapo gundua kuwa tumetenda dhambi lazima kutubu saa hiyo hiyo hakuna cha kusema kesho. Tuwe tayari kutubu kama Daudi alivyokuwa tayari kutubu (ZABURI 50:1-12).
HITIMISHO
Tunapata wokovu kwa kukiri kw kinywa (WARUMI 10:9-10) na Yesu Kristo ndio ondoleo la dhambi zetu (MATENDO 10:43, 1YOHANA2:1-2).
Unataka kutubu dhambi zakao kwa kumaaanisha kuziacha na kupata ondoleo la dhambi, tuma neno nataka kuokoka kwenda namba 0625966236 tumia whatsapp au sms za kawaida.
+255 625 966 236
+255 758 590 489
Kwa mafundisho Zaidi tembelea www.zakachekainjili.blogspot.com
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295
No comments: