» » NINI MAANA YA NENO “HOSANA”?



Na, Ev. Zachary John Bequeker (+255625966236)
Hosana ni neno litumikalo katika nyimbo za kusifu, mara nyingi katika Jumapili ya Mitende. 
Asili ya neno “Hosana” ni Kiebrania na ni moja ya neno lililotamkwa na kundi la watu pindi Yesu akiingia Yerusalemu.
“9 Na makutano waliotangulia, na wale waliofuata, wakapaza sauti, wakisema, Hosana, Mwana wa Daudi; ndiye mbarikiwa, yeye ajaye kwa jina la Bwana; Hosana juu mbinguni!” (Mathayo 21:9).

Hosana ni neno linalohamasisha wokovu. Neno hili linapatikana katika Zaburi 118:25 “25 Ee Bwana, utuokoe, twakusihi; Ee Bwana, utufanikishe, twakusihi.” Katika biblia ya kiingereza Psalm 118:25, inasomeka, “Save us, we pray, O LORD!” (ESV). Neno la Kiebrania yasha (“deliver, save”) na anna (“beg, beseech”) muunganiko wa maneno hayo tunapata neno la Kiingereza “hosanna.” Neno Hosana linamaanisha “twakuomba utuokoe” au "utuokoe twakusihi".

Wakati Yesu akiingia Yerusalem akiwa amempanda punda, watu walipaza sauti wakisema “Hosana!” walimtambua kama Masihi wao. Waliamini kuwa Yesu anaweza kuokoa.
Baadaye, Yesu alikuwa hekaluni, watoto waliokuwepo wakaanza kupaza sauti wakisema “Hosana Mwana wa Daudi!” (Mathayo 21:15). Lakini wakuu wa makuhani na waandishi walikasirika, wakamuuliza Yesu “Unasikia watoto hawa wasemavyo?” Yesu akawajibu, akawaambia “Hamkupata kusoma, Kwa vinywa vya watoto wachanga na wanyonyao umekamilisha sifa?” (Mathayo 21:16).

Hivyo watu walisema “Hosana!” wakihitaji wokovu na ndio sababu kuu iliyomleta Yesu yaani “Kutafuta na kuokoa kile kilichopotea”. Katika juma hilo ndilo Yesu alipoangikwa msalabani.
Ni mimi Ev. Zachary John Bequeker
INJILI HALISI MINISTRY
www.zakachekainjili.blogspot.com
+255625966236
+255758590489

Pakua App Ya Injili Halisi -Bofya Hapa Flower
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295

About INJILI HALISI MINISTRY

Zachary, most known as Zakacheka is the founder of the Injili Halisi Ministry. He is a member of Full Gospel Bible Fellowship Church.. He lives in Mwanza,Tanzania. 0621261295.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply