Kaini alikuwa ni mtoto wa kwanza MWANZO 4:1 “1 Adamu akamjua Hawa mkewe;
naye akapata mimba, akamzaa Kaini,
akasema, Nimepata mtoto mwanamume kwa Bwana.”, akifuatiwa na ndugu
zake Habili na Sethi MWANZO 4:2,25 “2 Akaongeza akamzaa ndugu yake, Habili….
25 Adamu akamjua mke wake tena; akazaa mwana mwanamume, akamwita jina lake Sethi...” Hawa walikuwa ni
kizazi cha kwanza, ingawa watoto waliotajwa ni watatu tu, Adamu alikuwa na watoto
wengine wake na waume MWANZO 5:4 “4 Siku za Adamu
baada ya kumzaa Sethi zilikuwa miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake.” . Mwanahistoria wa Kiyahudi
aliandika kuwa kama walivyosema wazee wa kale Adamu alikuwa na watoto 56, wa
kiume 33 na wa kike 23. Biblia haituambii walikuwa watoto wangapi
lakini kwa kuangalia umri wa maisha ya Adamu miaka 930 tunakubaliana kuwa walikuwa
ni watoto wengi. MWANZO 5:5 “5 Siku zote za Adamu alizoishi ni miaka
mia kenda na thelathini, naye akafa.”
Kumbuka kuwa Adamu na
Hawa waliambiwa wazae wakaongezeke MWANZO
1:28 “28 Mungu akawabarikia, Mungu
akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze
nchi….”
Adamu alimzaa Sethi akiwa na miaka 130 akaishi miaka 800
mingine ndipo akafa (MWANZO 5:4).
Mwanamke aliambiwa atazidishiwa uchungu MWANZO
3:16 “16 Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto;
na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.”
JE! KAINI ALIMUOA
NANI?
»Kuna madai kuwa Kaini baada ya kumuua ndugu yake Habili
alitoka na kwenda Nodi na ndiko alikompata mwanamke/mke wake (MWANZO 4:17) na kusema kuwa kipindi
hicho Nodi ilikuwa na watu walioishi tangu zamani (pre adamic human/pre adamiam)kabla
ya Adamu kuwepo na kudai kuwa aliyeolewa na Kaini ni moja ya watu hao(Pre
adamic human / pre adamism). Wengine husema alikuwa ni moja ya malaika
walioasi.
»Biblia iko wazi sana kuwa mtu wa kwanza ni Adamu(MWANZO 1:26), Adamu anaitwa mtu wa
kwanza ( 1 WAKORINTHO 15:45). Kabla ya Adamu kuumbwa hakukuwa na mtu
duniani(MWANZO 2:5-8) Mungu
alipomuumba Adamu akaona yuko peke yake, Mungu akamfanyia wanyama na ndege
lakini hawakufanana naye (MWANZO
2:18-20) ndipo akamfanyia Hawa"Eve" yaani mama wa viumbe
vyote (MWANZO 3:20).
Hivyo ni vyema tukatambua kuwa hao watu wanaodaiwa kuwepo "
pre adamic humans" hawakuwepo kwa sababu hata kabla Mungu kuumba
dunia inaoneaha hakukuwa na watu (MWANZO
1:1-2).
Ukisoma katika MWANZO
6:1-2 “1 Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na
wana wa kike walizaliwa kwao,2 wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya
kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua.” Hawa
wanaoitwa wana wa Mungu ni Malaika walioasi wakatupwa hapa duniani ndipo
wakawapenda binti za wanadamu wakawaoa maana yake ni kwamba hao Malaika walikuwa
ni wa kiume, kwa hiyo kwa sababu hii bado inagoma kusema kuwa Kaini alioa moja
ya malaika hawa kwa sababu wao walikuwa ni wa kiume. Sababu ya pili
inayodhihirisha kuwa hakuoa miongoni mwa malaika hawa ni kwamba hawa walikuja
kuonekana miaka mingi kupita ambapo tayari ulimwengu ukiwa na watu wengi ambapo
tayari Kaini alikuwa ameshaoa miaka mingi sana iliyopita.
»Tunaposoma neno "
MKE" kwa lugha ya kiebrania ni "ishshah"
linamaanisha WOMAN/ WIFE /FEMALE yaani
MWANAMKE/MKE.
Mwanamke ni yule aliyetokana na Adamu MWANZO
2:23 “23 Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi
ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume.”
»Kumbe tunaona kuwa Kaini Hakuna pre adamic human / pre
adamism bali alioa mwanamke aliyetokana na Adamu mwenyewe.
»Hivyo nasi, bila shaka Kaini alimuoa dada yake au mtoto wa
ndugu yake.
Zamani ilikuwa si kosa kaka na dada kuoana. Abraham alimuoa
dada yake, Sara (MWANZO 20:12),
Amramu, baba yake Musa alimuoa shangazi yake(KUTOKA 6:20), Yakobo alioa binti za mjomba wake (MWANZO 29:1-35). Miaka 400 baadaye
Mungu akabadili utaratibu, akazuia dada na kaka kuona (MAMBO YA WALAWI 18:6-18).
»NOTE: Biblia
inaposema " akamjua MKE" haimaanishi "akaoa" bali ni
kushiriki
tendo la ndoa MWANZO 4:17 “17 Kaini akamjua mkewe; naye
akapata mimba, akamzaa Henoko...” . Mariamu alikuwa hajamjua mume lakini
tayari alikuwa ameposwa na Yusufu LUKA
1:34 “34 Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili, maana sijui mume?”
»Hivyo basi , Kaini alipoondoka kuelekea Nodi alikuwa na MKE
wake na alipoondoka aliwaacha ndugu wengine wengi waliotaka kumpiga baada ya
yeye kumuua Habili.
MWANZO 4:15 “15 Bwana akamwambia, Kwa sababu hiyo ye yote atakayemwua Kaini
atalipizwa kisasi mara saba. Bwana akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije
akampiga.”
NAAMINI UNABARIKIWA SANA NA MASOMO HAYA.
NI MIMI EV. ZACHARY
JOHN BEQUEKER
INJILI HALISI MINISTRY
MWANZA – TANZANIA
+255625966236 /+255 758 590 489
NIFUATE FACEBOOK KWA JINA HILOHILO
KAINI ALIMUOA NANI?
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295
No comments: