» » SOMO:NINI MAANA YA KUMJUA YESU?




Na Ev. Zachary John Bequeker
+255 625 966 236 / +255 758 590 489
INJILI HALISI MINISTRY
Watu wengi tumekuwa tukisema kuwa tunamjua Yesu. Je, ni kweli tunamjua Yesu?
Je, kumjua Yesu ni kuitwa Mkristo? Je, kumjua Yesu ni kullitaja jina la Yesu?
Kumjua Yesu ni kuzishika amri zake .

1 YOHANA 2:3-4 “3 Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake. 4 Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake.”
Anayesema kuwa anamjua Yesu wala hazishiki amri zake huyo anaitwa ni mwongo wala kweli haimo ndani yake. Kweli ni neno la Mungu kama tunavyoona katika YOHANA 17:17 “17 Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli.”  Neno la Mungu huyu ndiye Yesu Kristo mwenyewe. YOHANA 1:1 “1 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.

Amri hizo ni zipi basi? Amri hizo ni neno lake lote. Amri zake ni zaidi tu ya zile anazozitaja katika MATHAYO 19:18-19 “18 Akamwambia, Zipi? Yesu akasema, Ni hizi, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo, 19 Waheshimu baba yako na mama yako, na, Mpende jirani yako kama nafsi yako.”

Kwa sababu hiyo basi ili kuzijua zaidi ni lazima kusoma biblia. Mfano wa amri ambayo Yesu anaitaja kuwa ni mpya haipo hapo tunaiona katika YOHANA 13:34 “34 Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.”

Kama tulivyosoma katika 1 YOHANA 2:3-4 tukaona kuwa KWELI ni NENO la Mungu na NENO la Mungu ndiye YESU mwenyewe. Kumbe basi tunapolisoma neno lake na kulishika ndilo linalo tufanya tumjue yeye (Yesu) zaidi na zaidi.

Ili kumjua Yesu ni lazima kwanza uokoke, ukishaokoka ndiyo huyo Yesu ambaye ni neno anaingia ndani yako na kwa namna hiyo utamjua yeye.  Na kwa namna hiyo tunakuwa na ujasiri wa kuomba lolote tutakalo nay eye(Yesu) atatenda. YOHANA 15:7 “7 Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.”

JE, UNATAKA KUUPOKEA WOKOVU?
 BONYEZA HILO NENO NDIYO UJIFUNZE ZAIDI


Pakua App Ya Injili Halisi -Bofya Hapa Flower
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295

About INJILI HALISI MINISTRY

Zachary, most known as Zakacheka is the founder of the Injili Halisi Ministry. He is a member of Full Gospel Bible Fellowship Church.. He lives in Mwanza,Tanzania. 0621261295.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply