Na Mwinjilisti Zachary John Bequeker(zakacheka)
+255 625 966 236/ +255 758 590 489
Email: zacharybequeker@gmail.com
Kumekuwa na utata mkubwa sana juu ya wanawake kufunika kichwa wakati wa ibada.
+255 625 966 236/ +255 758 590 489
Email: zacharybequeker@gmail.com
Kumekuwa na utata mkubwa sana juu ya wanawake kufunika kichwa wakati wa ibada.
Nataka leo tuangalie andiko hilo kwa undani zaidi ili
tuufahamu ukweli.
Neno la Mungu linasema katika YOHANA 8:32 “32
tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.” Watu wengi
wamekuwa watumwa katika jambo hili kwa sababu ya kushindwa kuifahamu kweli na
pia neno la Mungu linasema katika HOSEA 4:6 kwamba tunaangamizwa kwa sababu ya kukosa
maarifa. Maarifa hayo ni yapi basi? Maaarifa hayo ni neno la Mungu na ndiyo
haya tunayoenda kuyaangalia siku ya leo.
Biblia iko wazi kwamba, mwanamke asalipo (anapoomba,
anapohubiri,anapofundisha,anapomwimbia Mungu n.k) lazima afunike kichwa(1 WAKORINTHO 11:5)
Kumekuwa na watu wakisema kuwa kufunikwa kwa kichwa kunakoongelewa
ni kuwa na nywele ndefu (1 WAKORINTHO
11:15). Napenda kusema kuwa huu ni upotofu tena upotofu mkubwa kabisa.
Hebu tusome mistari hiyo katika 1 WAKORINTHO 11:4-15 “4 Kila mwanamume, asalipo, au anapohutubu, naye amefunikwa kichwa,
yuaaibisha kichwa chake. 5 Bali kila mwanamke
asalipo, au anapohutubu, bila kufunika kichwa, yuaaibisha kichwa chake; kwa
maana ni sawasawa na yule aliyenyolewa. 6 Maana mwanamke asipofunikwa na akatwe
nywele. Au ikiwa ni aibu mwanamke kukatwa nywele zake au kunyolewa, na
afunikwe. 7 Kwa maana kweli haimpasi mwanamume kufunikwa kichwa, kwa sababu
yeye ni mfano na utukufu wa Mungu. Lakini mwanamke ni utukufu wa mwanamume. 8
Maana mwanamume hakutoka katika mwanamke, bali mwanamke katika mwanamume. 9
Wala mwanamume hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke, bali mwanamke kwa ajili ya
mwanamume.10 Kwa hiyo imempasa mwanamke awe na dalili ya kumilikiwa kichwani,
kwa ajili ya malaika.11 Walakini si mwanamke pasipo mwanamume, wala mwanamume
pasipo mwanamke, katika Bwana.12 Maana kama mwanamke alitoka katika mwanamume,
vile vile mwanamume naye huzaliwa na mwanamke; na vitu vyote asili yake hutoka
kwa Mungu. Hukumuni ninyi wenyewe katika nafsi zenu. 13 Je! Inapendeza mwanamke
amwombe Mungu asipofunikwa kichwa? 14 Je! Hayo maumbile yenyewe hayawafundishi
ya kwamba mwanamume akiwa na nywele ndefu ni aibu kwake?15 Lakini mwanamke
akiwa na nywele ndefu ni fahari kwake.
Kwa sababu amepewa zile nywele ndefu ili ziwe badala ya mavazi.”
Katika mistari hii kuna mambo matano makuu ya kujifunza. Mambo
hayo ni kama yafuatayo:-
1. Haimpasi mwanaume kufunika kichwa asalipo
(anapoomba, anapohubiri,anapofundisha,anapomwimbia Mungu n.k) soma mstari wa 7
2. Inampasa mwanamke afunike kichwa asalipo
(anapoomba, anapohubiri,anapofundisha,anapomwimbia Mungu n.k). mwanamke
asipofunika kichwa anakuwa anaaibisha kichwa chake kama jinsi ilivyoaibu kwa
mwanamke kunyoa kipara (soma mstari wa 5 na 10)
3. Haimpasi mwanamke kunyoa nywele zake yaaani kuwa
na kipara kwani ni aibu (mstari wa 5)
4. Ni fahari kwa mwanamke kuwa na nywele ndefu.(soma
mstari wa 15)
5 5. Ni aibu kwa mwanaume kuwa na nywele ndefu. (soma
mstari wa 14)
Hitimisho: Pamoja na mwanamke kuwa na
nywele ndefu, ni lazima afunike kichwa anaposali au anapohutubu.
JE, UNATAKA KUUPOKEA WOKOVU?
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295
No comments: