+255625966236/+255758590489
zacharybequeker@gmail.com
Malaika ni neno la Kigiriki ἄγγελος au "angelos" lenye maana ya messenger (mjumbe) au angel kwa kiingereza. Malaika hufanya yaliyo matakwa ya Mungu (ZABURI 103:20, MATHAYO 26:53).
Malaika ni viumbe wenye nguvu kubwa na uwezo kuliko binadamu
(2 PETRO 2:11). Malaika walitokea mbinguni, au katika ulimwengu wa Kiroho , ambao uko juu sana kuliko ulimwengu wa kimwili (1 WAFALME 8:27; YOHANA 6:38) Kwa namna hiyo tunawaita ni roho (1 WAFALME 22:21; ZABURI 18:10).
Mungu aliwaumba malaika kupia Yesu, ambaye biblià inamtaja kuwa ni mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote. Biblià inasema katika WAKOLOSAI 1:13-17 " naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote. Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake. Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye."
Malaika ni jeshi la mbinguni (NEHEMIA 9:6). Malaika waliumbwa kabla ya dunia kuwako. Wakati Mungu anaumba dunia malaika walikuwa wakiimba na kupiga kelele kwa furaha (AYUBU 38:4-7).
Biblià haijatuambia idadi kamili ya malaika, lakini inaonesha kwamba idadi yao ni kubwa sana. Kwa mfano, maono aliyopewa Mtume Yohana yanaonesha mamia ya mamilioni ya malaika (UFUNUO 5:11).
Malaika wana majina yao. Biblia inatupatia majina ya malaika wawili : Mikaeli na Gabrieli (DANIELI 12:1; LUKA 1:26) . Malaika wengine walitajwa kuwa wana majina lakini hawakutaka kuyataja (MWANZO 32:29; WAAMUZI 13:17, 18).
Kazi moja wapo ya malaika ni kwalinda na kuwahudumia wale wamwaminio Mungu (ZABURI 34:7;91:10, 11; WAEBRANIA 1:7, 14).
Malaika mkuu kwa Kiingereza ni archangel /ˌɑːrkˈeɪndʒəl/ . Huyu ni malaika mwenye cheo cha juu.Neno hili linaonekana mara mbili katika Agano jipya katika 1 THESSALONIKE 4:16 na YUDA 9 . "Michael, one of the chief princes" (DANIELI 10:13) na "Michael, the great prince" (DANIELI 12:1).
Neno la kiingereza archangel limetokana na neno la Kigiriki ἀρχάγγελος (arch- +angel, literally "chief angel" or "angel of origin").
Mikaeli anatajwa katika DANIELI 10:13 kama "one of the chief princes" na si "chief prince" maana yake ni malaika wengi walio na mamlaka ya juu. Mikaeli wakati wote cheo chake kinakuwa na herufi ndogo ambazo ni tofauti na kwa Yesu ambapo huanza na herufi kubwa, angalia ISAYA 9:6, pia katika DANIELI 10:21 inasema Mikaeli ni "mkuu wenu" hapo napo imetumia herufi ndogo.
YESU ni MUNGU ,UFUNUO WA YOHANA 21:1, 3, 4, inatuonesha kwamba kuna kiti cha enzi kimoja cha Mungu na Mwana Kondoo, ukiendelea kwa biblia ya Kiingereza ya KJV inasema the servants (wingi!) will worship HIM (umoja!) and, will have on their faces HIS Name (umoja tena!)
I YOHANA 5:20 Inasema "YESU NI MUNGU WA KWELI"
Mtazamo wa Yesu kuwa ni Mikaeli, ulifundishwa na Russell, Ellen White, Joseph Smith yakihusiana na mafundisho ya Waislam kwamba Yesu ni nabii tu.
Yesu na Mikaeli ni tofauti. Hapa tunaona Bwana atashuka na sauti ya malaika mkuu (1 WATHESALONIKE 4:16) na katika MATHAYO 24:30-31 anasema "ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi. Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu."
MATHAYO 25:31 "Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake;"
Yesu anatumikiwa na malaika, MATHAYO 4:10-11 "Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake. Kisha Ibilisi akamwacha; na tazama, wakaja malaika wakamtumikia."
Yesu ni:-Zaidi ,tafadhali soma YOHANA 12:37-41 na linganisha na ISAYA 6:1-10.Yeye ni Mungu kama alivyosema katika YOHANA 10:30.
- Muumbaji (creator)
- Yuko mahali popote (Omnipresent)
- Aonaye sirini (Omniscient)
- Mwenye nguvu (Omnipotent)
YESU NI BWANA, YEYE NI MUNGU!
JE, UNATAKA WOKOVU?
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295
No comments: