Mwezi DESEMBA
katika biblia zetu unasomwa kama mwezi wa Kenda/tisa ambao kwa Kiebrania
unaitwa KISLEV(KISLEU) na wakati
mwingine katika biblia zetu utakuta umeandikwa Kisleu.
KISLEV ni mwezi wa tatu wa Serikali na ni mwezi wa tisa wa
mwaka wa Kiyahudi katika kalenda ya Kiebrania. KISLEU ni mwezi wa majira ya
VULI ambao ni kati ya mwezi Novemba na
Desemba kwa kalenda ya Gregorian.
Tunaona katika NEHEMIA
1:1 “1 Habari za
Nehemia, mwana wa Hakalia. Ikawa katika mwezi wa Kisleu, mwaka wa ishirini,
nilipokuwapo Shushani ngomeni,”
Pia katika ZEKARIA
7:1 “1 Ikawa katika
mwaka wa nne wa mfalme Dario, neno la Bwana lilimjia Zekaria, siku ya nne ya mwezi
wa kenda, yaani, Kisleu.”
Huu
ni mwezi wa kubarikiwa na Mungu kama
tunavyoona katika HAGAI 2:18-19 “18
Tafakarini, nawaomba; tangu siku hii ya leo na siku zijazo; tangu siku ya
ishirini na nne ya mwezi wa kenda, naam, tangu siku hiyo ulipowekwa msingi wa hekalu
la Bwana tafakarini haya. 19 Je! Mbegu ingali ghalani? Naam, huo mzabibu, wala
mtini, wala mkomamanga, wala mzeituni, haikuzaa kitu; tangu siku hii ya leo
nitawabariki.”
Huu ni mwezi wa ndoto kutimia na huu ni mwezi wa maono
chanya.
Ni vyema tukafahamu ili Mungu awabariki watu wake kuna
kuwa na mambo aliyoagiza. Mambo hayo tunayaona katika ZEKARIA 8:9 “9
Bwana wa majeshi asema hivi, Mikono yenu na iwe hodari, ninyi mnaosikia siku
hizi maneno haya kwa vinywa vya manabii, waliokuwapo siku hiyo ulipowekwa
msingi wa nyumba ya Bwana wa majeshi; yaani, hekalu hilo; ili lijengwe.”
Hapo tumeona mikono inakuwa hodari kwa wanaoisikia sauti
ya Mungu yaani neno la Mungu kupitia vinywa vya watumishi wake. Hivyo basi mwezi huu ukijiweka vizuri na Mungu kwa kulisikia neno lake na kulitenda hakika
ndoto zako ulizokuwa nazo kwa muda mrefu huu ndio mwezi wa kupokea kutoka kwa
Bwana.
Pia katika NEHEMIA
1:1,9 inasema “1
Habari za Nehemia, mwana wa Hakalia. Ikawa katika mwezi wa Kisleu, mwaka wa
ishirini, nilipokuwapo Shushani ngomeni, 9 bali mkinirudia mimi, na kuzishika amri
zangu na kuzitenda, watu wako waliofukuzwa wajapokuwa katika pande za
mwisho za mbingu, hata hivyo nitawakusanya kutoka huko, na kuwaleta mpaka
mahali pale nilipopachagua ili kuliweka jina langu hapo.”
Huu ni mwezi hatari kwa kila atendaye mambo haya
tunayoyaona katika ZEKARIA 7:8-12 “8 Kisha neno la Bwana likamjia
Zekaria, kusema, 9 Bwana wa majeshi amesema hivi, ya kwamba, Fanyeni hukumu za
kweli, kila mtu na amwonee ndugu yake rehema na huruma; 10 tena msimdhulumu
mjane, wala yatima, wala mgeni, wala maskini; wala mtu awaye yote miongoni
mwenu asiwaze mabaya juu ya ndugu yake moyoni mwake. 11 Lakini hao
walikataa kusikiliza, wakageuza bega lao, wakaziba masikio yao ili wasisikie. 12
Naam, walifanya mioyo yao kuwa kama jiwe gumu, wasije wakaisikia sheria na
maneno ya Bwana wa majeshi, aliyoyapeleka kwa roho yake kwa mkono wa manabii wa
kwanza; kwa sababu hiyo ghadhabu kuu ikatoka kwa Bwana wa majeshi.”.
Hapa tunaona ghadhabu iliyowapata watu waliokataa kusikia
neno la Mungu.
Katika mwezi huu yeyote anayekataa kuisikia sauti ya
Mungu atanyang’anywa mamlaka yake na kupewa mtu mwingine. Mali zake na vitu
vyake vyote vitaharibiwa.
HAGAI 2:20-23
“20 Kisha neno la Bwana
likamjia Hagai mara ya pili, siku ya ishirini na nne ya mwezi, kusema, 21 Sema na Zerubabeli,
liwali wa Yuda, ukisema, Nitazitikisa mbingu na dunia; 22
nami nitakipindua kiti cha enzi cha falme, nami nitaziharibu nguvu za falme za
mataifa; nami nitayapindua magari, na hao wapandao ndani yake; farasi na hao wawapandao
wataanguka chini; kila mtu kwa upanga wa ndugu yake. 23 Katika siku ile, asema Bwana wa
majeshi, nitakutwaa wewe, Ee Zerubabeli, mtumishi wangu, mwana wa Shealtieli,
asema Bwana, nami nitakufanya kuwa kama pete yenye muhuri; kwa kuwa nimekuchagua,
asema Bwana wa majeshi.”
Katika mwezi huu ni uamuzi wako kubarikiwa au kulaaniwa
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295
No comments: