» » SOMO: TOFAUTI YA KUOKOKA NA KUUKULIA WOKOVU



Na Zachary John Bequeker


✍Kuokoka ni kuzaliwa mara ya pili (YOHANA 3:3-7; 1 PETRO 1:23) baada ya kulisikia neno na kuliamini kisha unamkiri Yesu kuwa Bwana(mtawala) na mwokozi wa maisha yako. Tunaliona hilo katika WARUMI 10:9-10 "Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu."

✍Baada ya mtu kuokoka anapaswa aishi maisha yanayompendeza Mungu yaani sawa sawa na Neno la Mungu na Neno hilo ndilo litakalomfanya kuwa Mtakatifu, Soma *YOHANA 17:17* "Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli."

✍Neno la Mungu ndilo linatufanya kuwa watakatifu na pasipo utakatifu hatuwezi kumwona , yaani kuingia Mbinguni (soma WAEBRANIA 12:14)

✍Mtoto anapozaliwa anahitaji maziwa ili akue Vyema vivyo hivyo hata baada ya mtu kuokoka (kuzaliwa mara ya pili) anapaswa ajifunze Neno la Mungu ambalo linaitwa Maziwa yasiyoghoshiwa 1 PETRO 2:2 Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu;"

✍Kumbe, kama ukizaliwa mara ya pili halafu ukabaki mahali pasipohubiriwa Neno la Mungu lisiloghoshiwa (yaani lisilochakachuliwa) ni sawa na bure.

✍Hii ndio tofauti ya kuokoka na kuukulia wokovu. Unapookoka unazaliwa mara ya pili na kuukulia wokovu unalelewa chini ya walezi watakao kupatia lishe bora.

Wasiliana nami kwa +255625 966 236/ +255 758 590 489 / +255 673 590 489
JE, HUJAOKOKA UNAHITAJI WOKOVU? BONYEZA NENO HILI <<<<<NDIYO>>>> Download App ya Neno la Mungu hapa ====> INJILI HALISI

Pakua App Ya Injili Halisi -Bofya Hapa Flower
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295

About INJILI HALISI MINISTRY

Zachary, most known as Zakacheka is the founder of the Injili Halisi Ministry. He is a member of Full Gospel Bible Fellowship Church.. He lives in Mwanza,Tanzania. 0621261295.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply