» » SOMO: NJIA YA YESU NA NJIA YA SHETANI


Kuna wakati tumewahi kusafiri na kufika mahali tusikopajua vyema, njia ikawa ni ngeni kwetu na tukajikuta tuko mahali penye njia mbili inatubidi tusimame kwa sababu hatuijui njia sahihi kuwa ni ipi. Kwa Kuogopa kukosea njia inatubidi tumuulize  mtu fulani atuonyeshe njia sahihi.

Maisha yetu hapa duniani ni kama safari. Kuna njia mbili tunazoweza kuzifuata maishani. Njia hizi ni njia ya Yesu na njia ya Shetani. 


Tunaweza kuichagua njia ya Yesu au njia ya Shetani. Inatupasa tuchague njia sahihi itakayotufikisha mahali sahihi kwa sababu maisha ni kama safari. Safari hii huanza pale tunapozaliwa na huisha pale tunapokufa. Watu wengine hufa wakiwa vijana, hawa wana safari fupi. Wengine hufa wakiwa wazee, hawa wana safari ndefu. Lakini siku moja sisi sote tutafika mwisho wa safari ile ya maisha.


Ni lazima uchague mwenyewe njia utakayoifuata kwani tumepewa uamuzi wa kuchagua.


MATHAYO 7:13-14 "Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.".    

 Njia ya kwanza hapa inatajwa kuwa ni pana na watu wengi wanaingia kwa njia ile lakini njia hii inaelekea kwenye mauti. Watu wengi hupitia njia ya Shetani bila ya kuifikiria.

Njia ya Shetani ni rahisi. Watu wengi wanaifuata njia hiyo. Shetani huwaruhusu watu watende wapendavyo katika njia yake


Njia ya Yesu si rahisi. Mlango wa njia ya Yesu ni mwembamba, ni watu wachache tu ndio waionao njia hiyo lakini inaelekea uzimani.


Kama uko katika kanisa ambalo kila kitu wao ni kawaida tu, kutenda dhambi ni rahisi tu; hakika hapo hauko salama bali unaelekea Upotevuni. Upotevuni maana yake unakuwa uko mbali na Mungu. Ni rahisi kwenda Upotevuni kwani ni sawa na kuendesha baiskeli kwenye mtelemko. Watu Wengi hufuata njia yao ya kuelekea mautini. Hatupaswi kuelekea kwenye    mauti ya milele! Hatupaswi kufuata njia ya Shetani.


Ili kuishika njia ya Yesu ni lazima kutubu dhambi zetu . Maandiko yanasema njia hii ni ngumu. Maana yake ni kwamba ni lazima tuyashinde majaribu na dhambi. Ni lazima tuishi maisha matakatifu. Njia hii si rahisi lakini imejaa furaha na inaelekea uzimani. Inatupeleka tuishi na Mungu milele tena yatupatia maisha mema sana. 


Kuna watu wengi katika njia ya shetani. Wanaelekea kwenye mauti ya milele. 


Tukifuata njia isiyofaa msituni, tunaweza kurudi. Hivyo nawe kama sasa umegundua kuwa hauko katika njia sahihi sasa yakupasa urudi na uifuate njia iliyo sahihi. Tunaweza kuona kama tunapoteza wakati mwingi; lakini tutafika tuendako. Kama ukisubiri hadi mwisho wa safari ambayo ni mauti ya milele huwezi kurudi kamwe. Tunaishi hapa duniani mara moja tu na baada ya kufa ndio mwisho wa safari yetu kama ni uzima wa milele au mauti ya milele. Kwa hiyo lazima tufanye maamuzi ya busara katika kuchagua njia.


Watu wengine husema kuwa watajaribu    njia ya Shetani kidogo halafu kisha wataenda kwa njia ya Yesu. Hapa pana hatari kubwa sana kwa sababu tumeona kwamba watu wengine hufa wakiwa wangali vijana. Hatujui tutafika mwisho wa safari yetu siku gani kwa sababu hiyo basi ni lazima tuhakikishe kwamba sasa tuko katika njia sahihi.


Kama unataka uzima wa milele; njia ni moja tu ambayo ni Yesu Kristo. Yesu anasema katika  YOHANA 14:6 "Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi."  Tunaifuata njia ya Yesu kwa kulifuata neno la Mungu kwa kuwa neno la Mungu ndiye Yesu mwenyewe na ndiye awezaye kutufikisha salama.


Je, unahitaji kuifuata njia sahihi? Fuatisha sala hii, sema " Bwana Yesu nimefahamu kwamba wewe ndiye njia ya uzima wa milele, nakuomba Bwana unisamehe maovu yangu yote nipe kibali cha kutembea katika njia yako ili nisipotee. Nisaidie niweze kuifuata njia yako katika maisha yangu yote katika jina la Yesu....Amen"


Je, umefuatisha sala hii? Kama ni ndiyo bonyeza neno hili<<<NDIYO>>>  


Ili udumu katika njia ya Yesu ni lazima kuhudhuria ibada,kuomba na kujifunza neno lake mara kwa mara. 


Sasa umeokoka jambo la kuzingatia tafuta kanisa linalohubiri kweli ya neno la Mungu bila kupindisha pindisha. Kwa msaada, maombi/maombezi na ushauri wasiliana nami WhatsApp kwa Simu namba +255-625-966-236 pia Nifuate facebook kwa jina la www.facebook.com/ZacharyJohnBequeker.


Ni mimi Mwinjilisti Zachary John Bequeker

INJILI HALISI MINISTRY
+255-625-966-236
+255-758-590-489

Share na wengine wajifunze


MUNGU AKUBARIKI!!!

Pakua App Ya Injili Halisi -Bofya Hapa Flower
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295

About INJILI HALISI MINISTRY

Zachary, most known as Zakacheka is the founder of the Injili Halisi Ministry. He is a member of Full Gospel Bible Fellowship Church.. He lives in Mwanza,Tanzania. 0621261295.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply