Nyakati tulizonazo za sasa ni za mwisho na ni nyakati za hatari. Watu wengi hawataki injili ya kweli bali injili ya kuwafariji tu na ndio maana wanapenda mafundisho wa uongo yanayoendana na tamaa zao wenyewe na si yanayoendana na maagizo ya Mungu. Hivyo basi ili kuwa salama ni lazima kuijenga imani yetu mahali palipo na injili ya kweli.
Baada ya kuokoka kila mmoja ana wajibu wa kuisimamia imani yake yeye mwenyewe pamoja na watu kukudhihaki na kukukejeli wewe cha kufanya ni kuzidi kuijenga imani yako.
YUDA 1:17-20 "Bali ninyi, wapenzi, yakumbukeni maneno yaliyonenwa zamani na mitume wa Bwana wetu Yesu Kristo, ya kwamba waliwaambia ya kuwa, Wakati wa mwisho watakuwako watu wenye kudhihaki, wakizifuata tamaa zao wenyewe za upotevu. Watu hao ndio waletao matengano, watu wa dunia hii tu, wasio na Roho. Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika Roho Mtakatifu,"
Tunafanywa imara kiimani na neno la Mungu. WAKOLOSAI 2:6-7 "Basi kama mlivyompokea Kristo Yesu, Bwana, enendeni vivyo hivyo katika yeye; wenye shina na wenye kujengwa katika yeye; mmefanywa imara kwa imani, kama mlivyofundishwa; mkizidi kutoa shukrani."
Baada ya kuokoka tunaanza kujenga imani zetu kwa neno la Mungu kwa kuhudhuria ibada, kujisomea biblià na kwa kusoma vitabu mbali mbali vya mafundisho ya neno la Mungu.
Kila mmoja hujenga kwa malighafi zake, wengi hujenga kwa neno laini la kufariji tu wao hawataki kukemewa, kuonywa wala kukaripiwa lakini wewe jenga imani yako kwa malighafi ngumu zitakazoifanya imani yako kuwa imara ambapo hata majaribu yakija hayawezi kuiangusha imani yako. Wewe ni Mwanafunzi, Mwanafunzi bora hakwepi, habagui vipindi darasani wala hachagui kwamba asome mada ipi na asisome ipi bali husoma zote kwa maana anajua inampasa kufanya hivyo ili aweze kushinda katika mitihani yake. Vivyo hivyo mtu aliyeokoka huwa anaingizwa katika majatibio (tests) ambayo yataimarisha kiroho chake. Hivyo na wewe usiwe mtu wa kubagua neno la Mungu kwamba hili ulitendee kazi na hili usilitendee hasha! haipaswi kuwa hivyo bali inapaswa kulitenda kila neno aliloliagiza Mungu na kwa kufanya hivyo utaona unakuwa mshindi katika Jina la Yesu.
1 WAKORINTHO 3:10-12 "Kwa kadiri ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi, kama mkuu wa wajenzi mwenye hekima, naliuweka msingi, na mtu mwingine anajenga juu yake. Lakini kila mtu na aangalie jinsi anavyojenga juu yake. Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani, Yesu Kristo. Lakini kama mtu akijenga juu ya msingi huo, dhahabu au fedha au mawe ya thamani, au miti au majani au manyasi, kazi ya kila mtu itakuwa dhahiri."
Pia soma 1 PETRO 4:12-16
Kama hujaokoka ni Vyema ukaokoka sasa sawa sawa na neno la Mungu katika WARUMI 10:10 "Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu."
Natumaini uko tayari kuokoka, sasa fuatisha maneno haya. Sema " Bwana Yesu nimejigundua kuwa sijajenga imani yangu kwako . Nakuomba unisamehe Bwana. Nipe uwezo wa kuyashinda majaribu ya ulimwengu huu wa sasa na uniwezeshe kulipenda neno lako na kuliishi bila kubagua katika Jina la Yesu...Amen!"
Je, umefuatisha sala hii? Kama ni ndiyo bonyeza neno hili<<<NDIYO>>>
Je, umefuatisha sala hii? Kama ni ndiyo bonyeza neno hili<<<NDIYO>>>
Sasa umeokoka jambo la kuzingatia tafuta kanisa linalohubiri kweli ya neno la Mungu bila kupindisha pindisha. Kwa msaada, maombi/maombezi na ushauri wasiliana nami WhatsApp kwa Simu namba +255-625-966-236 pia Nifuate facebook kwa jina la Zachary John Bequeker.
Ni mimi Mwinjilisti Zachary John Bequeker
MUNGU AKUBARIKI!!!
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295
No comments: