Mwinjilisti Zachary John Bequeker - +255-625-966-236
Sara alikuwa mkewe Ibrahimu. Abrahamu aliambiwa na Mungu atoke katika nchi ya jamaa zake na nyumba ya baba yake waliokuwa wakiabudu miungu. Pindi anatoka huko alikuwa na umri wa miaka 75, akatoka na mkewe Sara (MWANZO 12:1-7).
Abrahamu alimdai Mungu mtoto atakayekuwa mrithi wake (MWANZO 15:1-7). Mungu alimuahidi Ibrahimu atampa mtoto akiwa na umri wa miaka 75 lakini ahadi ilitimia na kupata mtoto akiwa na umri wa miaka 100. Ahadi hiyo ilichukua miaka 25 ndipo ikatimia (MWANZO 21:1-7).
UAMINIFU ambao kwa lugha ya asili huitwa "PISTOS" huwa haupimwi kwa tukio moja au kwa muda mfupi bali kwa matukio kadhaa na kwa muda mrefu sana. Huwezi kusema mtu huyu ni mwaminifu kwa kuwa naye siku mbili, tatu au kadhaa bali utamwamini mtu baada ya majaribio mengi. Mwaminifu ni mtu ambaye hakuna kitu chochote kinachoweza kumyumbisha kutimiza kile anachotakiwa kukitimiza. Mungu anapoitwa MWAMINIFU maana yake anachosema ni lazima atakitimiza tu (HESABU 23:19). Hivyo basi ahadi zote za Mungu zilizomo ndani ya neno lake ni lazima kutimia kwake yeye aliyeahidiwa akiwa na imani juu ya hilo. Ibrahimu ilifikia mahali akaona ile ahadi inachelewa akazaa na kijakazi wake.
Ili kuona uaminifu wa Mungu ukitimia ni lazima nasi tuwe waaminifu, tupatane naye katika uaminifu kwani Mungu hawezi akawa mwaminifu kwetu kama sisi si waaminifu.
IMANI NI LAZIMA IENDANE NA SUBIRA
Wanaobarikiwa ni wale wanao subiri kama Ayubu (YAKOBO 5:11).
Nasi tunapomwomba Mungu tuwe waaminifu tukingoja majibu hata kama ni kwa muda mrefu tunapaswa kusubiri tukijua kuwa ni lazima atatenda kama alivyosema kwani UAMINIFU WETU UNAPIMWA KATIKA KUSUBIRI
YUSUFU naye alikuwa mwaminifu akiamini kuwa ahadi ya Mungu lazima itimie pamoja na kwamba alipita katika mambo magumu kwa muda mrefu.
Mungu anataka tushike amri zake na kuwa waaminifu hata tukiwa katika utumwa wa aina yoyote ile. Pamoja na kwamba kutakuwa na magumu na mapito ya kila aina tusinung'unike, tusihuzunike, tusisononeke wala kufadhaika bali tuzidi kuliishi neno la Mungu tukiamini BARAKA za Mungu kwetu za mwilini na za rohoni ni lazima zije.
Ni mimi Mwinjilisti Zachary John Bequeker
INJILI HALISI MINISTRY
+255-625-966-236
+255-758-590-489
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295
No comments: