» » SOMO: VITU VITATU ANAVYOVICHUKIA MUNGU



Na, Ev. Zachary John Bequeker
UNJILI HALISI MINISTRY
WhatsApp:
 +255 (0)625 966 236
+255 (0)758 590 489

Facebook: www.facebook.com/zachary.bequeker

Instagram: www.Instagram.com/zachary_bequeker/

"Kuna vitu sita anavyovichukia Bwana; Naam, viko saba vilivyo chukizo kwake: Macho ya kiburi, ulimi wa uongo, Na mikono imwagayo damu isiyo na hatia".         MITHALI 6:16-17

✍Leo tutaangalia vitu vitatu katika orodha hii katika MITHALI 6:17.

1. Macho ya kiburi
✍ Mtu mwenye macho ya kiburi hujiona yeye ndiye bora, wa thamani kuliko wengine.
✍Mtu huyu huwadharau wengine na kuwaona si kitu kwake na kusahau kuwa kila mmoja ni wa thamani kwa mwenziye na Mungu humpatia kila mmoja karama yake (WARUMI 12:6)Kufanya hivyo ni sawa na kumdharau Mungu kwa kuidharau hekima yake na mtu huyo huitwa mpumbavu (MITHALI 1:7)

✍Mtu mwenye macho ya kiburi(anayejiinua) hushushwa (ZABURI 18:27)

2. Ulimi wa Uongo
✍Yesu kristo amabaye ni Mungu anasema yeye ni kweli. YOHANA 14:6 "Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli,na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi."

✍Hivyo ni dhahiri kuwa Mungu wetu anachukia uongo. Mungu ni mkweli anachosema anatimiza hivyo kwa mtoto wa Mungu lazima kuwa mkweli.

✍Katika amri ya tisa inakataza kuwa mashahidi wa uongo, yaani tusiruhusu ndimi zetu kutetea uongo. 
Watu wamekuwa wakisema uongo na kusababisha watu wengine kufukuzwa  kazini au nyumbani, ndoa kuvurugika na hata wengine wamekuwa wakisema uongo kanisani juu ya mtu fulani na kusababisha wengine kufukuzwa na hata kufa kiroho.
 Chagua mwenyewe, useme uongo uwafurahishe wanadamu na uhatarishe roho yako au useme kweli uponye roho yako na uhatarishe usalama wako wa kimwili?

KUTOKA 20:16  "Usimshuhudie jirani yako uongo."

3. Mikono imwagayo damu isiyo na hatia
✍Kumwaga damu ni kuua na kuua ni dambi.

✍Kitendo hili hakiruhusiwi kumtendea binadamu yeyote. Sote tuliumbwa kwa sura na mfano wa Mungu MWANZO 1:26-27

✍Neno la Mungu linatukataza kuua KUTOKA 20:13 "usiue"

✍Ni Vyema tukatambua ni vitu vipi anavichukia Mungu ili tusimtende dhambi.

❤ Sharing is Caring

Share kadri uwezavyo ili wajifunze wengi zaidi

NJILI HALISI MINISTRY

Pakua App Ya Injili Halisi -Bofya Hapa Flower
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295

About INJILI HALISI MINISTRY

Zachary, most known as Zakacheka is the founder of the Injili Halisi Ministry. He is a member of Full Gospel Bible Fellowship Church.. He lives in Mwanza,Tanzania. 0621261295.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply