» » SOMO: MAMBO 10 YANAYOWEZA KUHARIBU UHUSIANO WETU NA MUNGU


WhatsApp: +255 (0)625 966 236
                     +255 (0)758 590 489
Facebook: Zachary John Bequeker
Instagram: zachary bequeker

Kuna mambo mengi ambayo yanaweza kumfanya mtu awe mbali na Mungu. Leo tutaangalia mambo 10 kama yafuatayo:-

1.Pesa
     Watu huwa wakitumia muda mwingi wakitafuta pesa kuliko kuutafuta USO wa Mungu, kwa kuomba na kusoma biblia.
MATHAYO 6:19-34
Sina maana ya kwamba uache kazi au uache kutafuta pesa, Bali tumfanye Mungu kuwa wa muhimu kuliko pesa.

2. Vyombo ya habari na Mitandao ya Kijamii
Internet, Magaeti,Tv, simu n.k tunapaswa tutumie kwa kiasi. Tusipokuwa makini tutajikuta muda wote tunautumia kwa kuchat, mtu ataanzia facebook, anaenda Instagram, baadaye Twitter kisha Snapchat, WhatsApp, Telegram, IMO, Wechat, Palmchat n.k hadi anakuja kumaliza kutembelea mitandao hiyo yote tayari siku imepita.
Mwingine yeye ni kuangalia runinga tu, anatoka chaneli hili anaenda ile au unakuta yeye ni mtu wa kubadili CD tu na hizi season ndio zimewamaliza kabisaaa.

Hebu tuwe na muda maalum wa kuwa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii pia.

3. Kanisa/Dini
Watu wengi huamini Dini kuliko kumwamini Yesu kristo aliye njia, kweli na uzima.
Nenda kanisani na uishi kwa kulifuata neno la Mungu na so mapokeo ya kanisa au Dini.

4. Mahusiano
Mahusiano yetu kati ya wazazi,ndugu,jamaa,wafadhili wetu, watoto,wafanyakazi wenzetu,wakuu wetu wa kazi, boyfriends/girlfriends ......hawa wote wanauwezo mkubwa wa kututenga au kupoza upendo wetu kati yetu na Mungu. Ni asili yetu wanadamu kuwa na Mahusiano, lakini tusiruhusu moja ya uhusiano huu kuwa kuwa na nguvu kuliko Mungu .
KUMBUKA: Mungu ametuagiza tupendane 1 YOHANA 3:11….Kwa hiyo tunapopendana,tunatimiza agizo la Mungu. Lazima tuhakikishe kwamba tunampa Mungu muda wa kutosha(ample time) kila siku.
Uhusiano wa girlfriends, boyfriends na wakuu  wetu wa kazi ni uhusiano hatari sana ambao una 100% za kutuweka mbali na Mungu wetu. Tuwe makini na wakuu wetu wa kazi na tusiwe na girlfriends au boyfriends kwani ni dhambi. 
WAEFESO 5:3 “Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo wote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu;”

5. Ratiba(Routine)
      Hakikisha unatenga muda wa kuwa na Mungu wetu.
Katika ratiba zetu lazima kuwepo na muda wa Kusoma neno na kuomba. Na mruhusu Mungu akuongoze.

6. Kazi zetu
Kazi zetu hutufanya kuwa mbali na Mungu. Kwa maana watu wengi huwa tunatumia muda mwingi kwa kazi na kumsahau Mungu. Wakati mwingine tunajikuta katika wakati mugumu tunapokuwa kazini. Tufanye kazi kwa bidii na tutenge muda wa kuwa na Mungu wetu pia.Tusiwe kama Martha Bali tuwe kama Mariam LUKA 10:38-42

7. Our hobbies
Our hobbies can consume a lot of time. 
Hobby ni jambo alipendalo mtu.
Hobbies zetu hutuchukulia muda mwingi sana.
Tunapaswa tuwe na kiasi katika hobby . 2 TIMOTHEO 4:5 "Bali wewe, uwe na kiasi katika mambo yote, vumilia mabaya, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiliza huduma yako."
Pia kuna hobbies zingine ambazo moja kwa moja ziko kinyume na mapenzi ya Mungu. Hivyo tunapaswa kuziacha mara moja katika Jina la Yesu, sema Amen kama umeelewa.

8. Kuhitaji baraka za Mungu kuliko  Mungu mwenyewe
Tuutafute kwanza ufalme wa Mungu  na hayo mengine yaani baraka tutazidishiwa. 
Tunapaswa tumtafute Mwenye vitu na siyo vitu. Tukimpata mwenye vitu tujue tumeshapata vitu. 
MATHAYO 6:33 "Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa."

9. Wachungaji wetu
Wachungaji nao wanaweza kututenga na Mungu. 
Wachungaji wengi huaminisha waumini kuwa wao Ndio wanajua kila kitu…….na sababu  hiyo husema hakuna haja ya kuhangaika kusoma Vitabu vya neno la Mungu tukiwa nyumbani. 
Hebu fikiri kwa MTU anayeenda kanisani mara moja kwa juma maana yake anailisha roho yake mara moja tu kwa siku saba.
 Je, unaweza kuishi juma zima kwa kula mlo mmoja tu kwa siku zote hizo? Hapana haiwezekani. Kama haiwezekani vivyo hivyo kwa Roho zetu ni ngumu kuishi kwa mlo mmoja tu kwa juma lote.
Hata kama umezingwa na shughuli jitahidi kupangilia ratiba yako ili baada ya Nazi uwe na muda wa Kusoma Biblià na kuomba.
KUMBUKA: Si wajibu wa wachungaji kutulisha kila tunachohitaji Kiroho Bali ni Wajibu wetu.

10. Sisi wenyewe
  Kwa asili tu wenye dhambi na tunapofuata asili yetu tuna kuwa mbali na Mungu.
Kwa sababu  hiyo nasi ni vyema tukaishi kwa kumfuata Mungu wala tusifuatishe matakwa ya miili yetu.(tamaa zetu wenyewe). Tujikane na tuishi ndani ya Kristo WARUMI 7:15-21
Tumruhusu Mungu aichunguze na kuitengeneza mioyo yetu. ZABURI 139:23-24.


• Ni Mimi EV. Zachary John Bequeker - Mwanza Tanzania.
Wasiliana nami: 
                          Barua pepe:Zacharybequeker@gmail.com
                           WhatsApp/IMO/Telegram/SMS/Direct call: +255625966236
Kwa masomo zaidi tembelea www.zakachekainjili.blogspot.com
    @INJILI HALISI MINISTRY2018

Pakua App Ya Injili Halisi -Bofya Hapa Flower
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295

About INJILI HALISI MINISTRY

Zachary, most known as Zakacheka is the founder of the Injili Halisi Ministry. He is a member of Full Gospel Bible Fellowship Church.. He lives in Mwanza,Tanzania. 0621261295.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply