» » SOMO: SHEHE KATIKA BIBLIÀ


Na Ev. Zachary John Bequeker
INJILI HALISI MINISTRY
+255 (0)625 966 236
+255 (0)758 590 489

➡Neno "Shehe" katika biblià halijatumika kwa maana iliyozoeleka au kufahamika kwa wengi kuwa ni Kiongozi wa dini ya kiislamu.

➡Katika Kiswahili Neno hili Shehe lina maana mbili.

➡Maana ya kwanza ni mtu mwenye elimu ya dini ya Uislamu, agh. huifundisha kwa watu wengine. Na maana ya pili ni mzee anayeheshimiwa kwa ajili ya busara yake na mashauri anayotoa.

➡Katika biblià, neno hili limetumika maana yake ikiwa inahusiana na ile ya pili. Kumbe hata waliotafsiri biblià bila shaka walitumia neno hilo kwa  maana hiyo ya pili.

➡Tuangalie sasa maana halisi ya neno hilo Shehe lilivyotumika katika biblià:-

🆕 1: Governor - Huyu ni Kiongozi wa serikali, mfano Mkuu wa Mkoa. 2 NYAKATI 1:12 "Sulemani akasema na Israeli wote, na maakida wa maelfu, na wa mamia, na waamuzi, na kila shehe wa Israeli wote, wakuu wa nyumba za mababa.
Then Solomon spake unto all Israel, to the captains of thousands and of hundreds, and to the judges, and to every governor in all Israel, the chief of the fathers."

🆕 2: Prince - Huyu ni Mkuu katika tawala za Kifalme. YOSHUA 17:4 "Nao wakakaribia mbele ya Eleazari, kuhani, na mbele ya Yoshua, mwana wa Nuni, na mbele ya mashehe, wakasema, Bwana alimwamuru Musa kutupa sisi urithi kati ya ndugu zetu; basi kwa kuiandama hiyo amri ya Bwana akawapa urithi kati ya ndugu za baba yao.
And they came near before Eleazar the priest, and before Joshua the son of Nun, and before the princes, saying, The LORD commanded Moses to give us an inheritance among our brethren. Therefore according to the commandment of the LORD he gave them an inheritance among the brethren of their father." Pia soma 1 NYAKATI 7:40

🆕 3: Ruler - Huyu ni mtu mwenye mamlaka juu ya nchi na watu   NEHEMIA 2:16 "Wala mashehe hawakujua nilikokwenda, wala nilivyotenda; wala sijawaambia Wayahudi, wala makuhani, wala wakuu, wala mashehe, wala watu wengine waliokuwa wakiifanya kazi hiyo.
And the rulers knew not whither I went, or what I did; neither had I as yet told it to the Jews, nor to the priests, nor to the nobles, nor to the rulers, nor to the rest that did the work." Pia soma (NEHEMIA 4:14,19; NEHEMIA 5:7,17; NEHEMIA 7:5; NEHEMIA 12:40; NEHEMIA 13:11;EZRA 9:2 )

🆕 4: Lord - Huyu ni mtu (Mwanamme) mwenye mamlaka katika eneo fulani.
YOSHUA 13:3 "kutoka Shihori, hicho kijito kilichokabili Misri, hata mpaka wa Ekroni upande wa kaskazini, nchi inayohesabiwa kuwa ni ya hao Wakanaani; mashehe matano wa hao Wafilisti; Wagaza, na Waashdodi, na Waashkeloni, na Wagiti, na Waekroni; tena Waavi,
From Sihor, which is before Egypt, even unto the borders of Ekron northward, which is counted to the Canaanite: five lords of the Philistines; the Gazathites, and the Ashdothites, the Eshkalonites, the Gittites, and the Ekronites; also the Avites:"
Pia soma (1 SAMWELI 5:8-11; 6:4-18; 7:7; 29:2,7).

🆕 5: Duke - Huyu ni mtu mwenye wadhifa mkubwa katika taifa au ni Kiongozi wa Taifa dogo lililo huru.
 YOSHUA 13:21 "na miji yote ya nchi tambarare, na ufalme wote wa Sihoni mfalme wa Waamori, aliyekuwa akitawala katika Heshboni, aliyepigwa na Musa pamoja na hao wakubwa wa Midiani, nao ni Evi, na Rekemu, na Suri, na Huri, na Reba, hao mashehe wa Sihoni, waliokuwa katika nchi hiyo.
And all the cities of the plain, and all the kingdom of Sihon king of the Amorites, which reigned in Heshbon, whom Moses smote with the princes of Midian, Evi, and Rekem, and Zur, and Hur, and Reba, which were dukes of Sihon, dwelling in the country."

Pia ni Mkuu wa mji au mtaa(jumbe) soma MWANZO 36:17,29 "Na hawa ni wana wa Reueli, mwanawe Esau; jumbe Nahathi, jumbe Zera, jumbe Shama, jumbe Miza. Hao ndio majumbe waliotoka kwa Reueli katika nchi ya Edomu. Hao ni wana wa Basemathi, mkewe Esau.
And these are the sons of Reuel Esau's son; duke Nahath, duke Zerah, duke Shammah, duke Mizzah: these are the dukes that came of Reuel in the land of Edom; these are the sons of Bashemath Esau's wife.......Hawa ndio majumbe waliotoka katika Wahori; jumbe Lotani, jumbe Shobali, jumbe Sibeoni, jumbe Ana,
These are the dukes that came of the Horites; duke Lotan, duke Shobal, duke Zibeon, duke Anah,".

➡Bila shaka mpaka hapa utakuwa umejifunza maana sahihi ya neno SHEHE lilivyotumika katika biblià.
Kwa mafundisho zaidi Tembelea:
www.zakachekainjili.blogspot.com

Ni mimi Ev Zachary John Bequeker
INJILI HALISI MINISTRY
+255 (0)758 590 489
+255 (0)625 966 236
EMAIL: zacharybequeker@gmail.com

Facebook: www.facebook.com/zachary.bequeker

Instagram: www.Instagram.com/zachary_bequeker/

Pakua App Ya Injili Halisi -Bofya Hapa Flower
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295

About INJILI HALISI MINISTRY

Zachary, most known as Zakacheka is the founder of the Injili Halisi Ministry. He is a member of Full Gospel Bible Fellowship Church.. He lives in Mwanza,Tanzania. 0621261295.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply