» » SOMO: MIIBA NA MOTO KATIKA IMANI


MUNGU wetu  tunayemuabudu, HEKIMA yake kiutendaji iko juu sana. Wako watu wengi baada ya kuanza safari au katikati ya safari yao ya kwenda MBINGUNI hukutana na magumu na mazito kwa namna moja au nyingine. Kila msafiri kwa wakati wake hukutana na MIIBA hii na MOTO kwa namna tofauti.

Soma 1PETRO 4:12 "Wapenzi msione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu, unaowapata kama MOTO ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho"

Wengine wamekaa kwenye imani katika usafi na utakatifu miaka 5,miaka 10 au miaka 27 sasa hana MTOTO, pamoja na machozi miaka yote hiyo ni kama MUNGU hasikii. Wengine alitamani kupata MUME wa kiblia lakini anaona ni miaka imekatika na MZUNGUKO wa damu unaenda kukoma yaani kati ya miaka 45 hadi 50, maana yake uwezekano wa kuzaa ni kama unapungua.

Mwingine ni UGONJWA umeng'ang'ania katika mwili kwa miaka nenda miaka rudi anaona wengine wakishuhudia kuwa MUNGU kawaponya na yeye bado. Wengine ni hali ngumu kiuchumi kila kukicha afadhari hata jana maana ni mitihani na mazito. Wengine ni MIMBA kuharibika, changamoto katika NDOA, KAZINI, kwenye BIASHARA, MISIBA, AJARI, kutengwa, kusemwa vibaya na yanayofanana na hayo.

Soma: 2 WAKORINTHO 12:7-10 "Na makusudi nisipate kujivuna kupita kiasi, kwa wingi wa mafunuo hayo nalipewa MWIBA katika mwili, MJUMBE wa Shetani ili ANIPIGE, nisije NIKAJIVUNA kupita kiasi. Kwaajili ya kitu hicho nalimsihi BWANA mara tatu kwamba kinitoke; Naye akaniambia Neema yangu yakutosha;maana uweza wangu watimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa FURAHA nyingi, ili uweza wa KRISTO ukae juu yangu. Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na MISIBA na ADHA, na SHIDA, kwa ajili ya KRISTO. Maana niwapo DHAIFU ndipo nilipo na NGUVU."

Unapoyaona hayo hupaswi kunyong'onyea na kulalamika hata kuwaza kuacha WOKOVU, wakati kama huo ndipo Paulo anasema "basi nitajisifia UDHAIFU wangu kwa FURAHA nyingi."

Ni muhimu kufahamu kwamba kila msafiri wa kweli hakosi changamoto safarini labda kama wewe ni MSINDIKIZAJI. Tunajua vizuri kero na mahangaiko ya safarini pamoja na hatari zote haziwapati WASINDIKIZAJI.

Jambo la kuzingatia ni kwamba uyaonapo hayo hayamaanishi MUNGU amekuacha, wewe ni MBAYA kuliko wengine na yanayofanana na hayo bali kinyume chake MUNGU amekuamini kuwa JARIBU hilo unaliweza maana hawezi kuachilia jaribu ambalo linapita uwezo wako

Soma: 1WAKORINTHO 10:13 "Jaribu halikuwapata ninyi isipokuwa lililokawaida ya wanadamu, ila MUNGU ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita muwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.

Ni kweli dhambi inaweza kuleta majuto na mabaya yote lakini, jambo hilo likiwa ni dhambi DHAMIRI itakushuhudia kwamba ni kutokana na DHAMBI na baada ya KUTUBU kwa machozi na kuacha, jambo hilo hukoma mara moja. Lakini ukiwa ni MWIBA hata uombe mara 3 kama Paulo bado litasimama mpaka muda ulioamriwa ukamilike.

YESU anakupenda upeo, furaha yake ni kuona unahitimu katika kila jaribu au mtihani unaopitishwa. Baada ya kushinda kila jaribu na mtihani, uko UTUKUFU wa MUNGU unakusubiri. Yeye ashindaye atayarithi haya, UFUNUO WA YOHANA 21:7; sasa una shinda nini kama hayo hayapo?

Mtu yeyote asikuvunje moyo kwa magumu na mazito unayopitia, usikubari mtu akutenganishe na KRISTO kwa maneno yasiyo maana. SAFARI ya MBINGUNI ni ya mtu peke yake na MUNGU. Yeye aliyeanza safari moyoni mwako lazima aikamilishe ukiendelea kuwa MWAMINIFU.

MWISHO:
AYUBU 26:5-6 "Hata nitakapokufa sitajiondolea uelekevu wangu. Haki yangu naishika sana, wala sitaiacha;Moyo wangu hautanisuta wakati nikiwapo hai."

Watie moyo watakatifu wake, waambie MFALME wetu na BWANA wetu ndiye anayetawala juu mbinguni na duniani, anatuwazia mema YEREMIA 29:11, baada ya taabu za duniani hatimaye YESU atupendaye atatukaribisha kwake, HALELUYA!

Ni mimi Kaka Joseph M. Marwa.


Written by Zachary John Bequeker, Mwanza - Tanzania
+255625966236

Pakua App Ya Injili Halisi -Bofya Hapa Flower
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295

About INJILI HALISI MINISTRY

Zachary, most known as Zakacheka is the founder of the Injili Halisi Ministry. He is a member of Full Gospel Bible Fellowship Church.. He lives in Mwanza,Tanzania. 0621261295.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply