» » SOMO: KUCHUKIA UTUKUFU NA KUIDHARAU AIBU


WAEBRANIA 11:24-26 "Kwa imani Musa alipokuwa mtu mzima alikataa kuitwa mwana wa binti Farao; akaona ni bora kupata mateso pamoja na watu wa MUNGU, kuliko kujifurahisha katika dhambi kwa kitambo; akihesabu ya kuwa kushutumiwa kwake KRISTO ni UTAJIRI kuliko hazina zote za Misri; kwa kuwa aliyatazamia hayo malipo."

Mara nyingi na ndivyo ilivyo kuhubiri injili ni kulibeba Jina la YESU kulipeleka kwa ulimwengu ambao siku zote una uadui juu ya MUNGU. Kuionea haya (AIBU) injili ni kumuonea haya YESU mwenyewe WARUMI 1:15, MARKO 8:38; hivyo yeye naye ana ahidi kumuonea haya mtu huyo siku ya kufunuliwa kwake.

Unapowahubiri watu kuacha dhambi au unapoishi maisha yaliyo mbali na dhambi; mara nyingi ni kuamsha hisia za uadui katika jamii inayotuzunguka, zinazoweza kupelekea kupewa majina ya hovyo mengi; kwasababu dhamiri zao zinawahukumu watakurushia maneno na kukuita majina ya ajabu kama vile:

Amechanganyikiwa, Amerukwa na akili, Mweu, Maskini, Mshamba, Mtumwa, Anajifanya Mtakatifu sana, Mwendawazimu, Mjinga, Amekosa kazi, Anatafuta sadaka, Mtaabishaji, Msumbufu, Anayepigia watu kelele, Mzee wa ndoto, Mjanja mjanja, Nabii wa uongo n.k Soma MARKO 3:21-28

Lengo la majina hayo yote ni kukuvunja moyo ili ikiwezekana usiwe na ujasiri tena hata mwisho uone aibu. Kinachofanyika katika ulimwengu wa roho adui hutumia watu, ustaarabu au vitu ili kututoa kwenye lengo.

Kamwe watakatifu waliotutangulia hawakukubali ukombozi juu ya hilo, hawakutaka faraja wala lolote la kuwapumzisha wasiibebe aibu. Maana kwao ilikuwa heshima kubwa sana kudharauliwa kwaajili ya hilo Jina, WAEBRANIA 12:35b "Lakini wengine waliumizwa vibaya na kuuawa, wasikubali ukombozi ili wapate ufufuo ulio bora". Iwe ni chuoni au shule unayosoma, au sehemu ya biashara, au mtaani; itakupasa kuibeba AIBU na kukubali KUDHARAULIKA lakini KRISTO atukuzwe katika jamii inayokuzunguka

Utukufu na thawabu zinamgoja kila mmoja ambaye halegei wala hakati tamaa juu ya kulibeba Jina hili kuu sana la KRISTO katikati ya kizazi cha uzinzi na zinaa. Kunyamaza ni kuogopa AIBU, UFUNUO WA YOHANA 21:8 na itahesabika ni kutaka utukufu na heshima kabla ya muhura wako.

UFUNUO WA YOHANA 14:13b "Heri wafu wafao katika BWANA tangu sasa wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao." Sasa unaanzaje kupumzika hata kabla ya kumaliza kazi? Siyo wakati wa kupumzika tuendelee kuibeba AIBU na KUDHARAULIWA kwa ajili ya JINA la YESU.

MWISHO:
Nafasi ya kufanya vizuri na kuendelea kupeleka vifaa mbinguni bado tunayo, kila siku MUNGU anayotupa ni mtaji wa kutisha tuitumie vizuri, ili mwisho BWANA atusifu maana sifa za kusifiwa na wanadamu hazina thawabu bali tukisifiwa na KRISTO oooh ni heshima MILELE. 2 WAKORINTHO 10:18 "Maana mtu mwenye kukubaliwa si yeye ajisifuye, bali yeye asifiwaye na BWANA.". Tukiyasahau yale ya zamani tuliyokwisha yatenda, bali tutende upya kama vile hatujawai kutenda. Heri mtumwa yule ambaye BWANA wake atakapokuja atamkuta anagawa POSHO, LUKA 12:42.

Amani, amani, amani kwako wewe uliyempa YESU maisha. Na wewe ambaye bado haujafanya maamuzi chukua hatua tubu na kuacha uovu, kisha anza kwenda mahali inapohubiriwa injili isiyotiwa maji ili ukulie wokovu, KARIBU!

Ni Mimi Kaka Joseph M. Marwa.


Written by Zachary John Bequeker, Mwanza - Tanzania
+255625966236

Pakua App Ya Injili Halisi -Bofya Hapa Flower
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295

About INJILI HALISI MINISTRY

Zachary, most known as Zakacheka is the founder of the Injili Halisi Ministry. He is a member of Full Gospel Bible Fellowship Church.. He lives in Mwanza,Tanzania. 0621261295.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply