» » AINA MBILI ZA KONDOO


»Kuna aina mbili za kondoo; ambao ni kondoo wa Yesu na Kondoo vipofu waliopotea.

1: KONDOO WA YESU
»Hawa ni watu waliookoka na huishi na kuongozwa na Yesu mwenyewe ambaye ndiye Neno (YOHANA 1:1; YOHANA 17:17).

»Hawa wanapolisikia Neno hulichunguza ili kujua kama ndivyo lilivyo kama walivyokuwa watu wa Beroya (MATENDO 17:10-11).

»Kondoo wa Yesu huisikia sauti ya Mchungaji mwema na humfuata vile atakavyo (YOHANA 10:26-27) na kwa sababu hiyo basi wao huenenda katika njia nzuri na hawawezi wakapotelea mwituni mbwa mwitu wakawala kwa sababu wako mikononi mwa Mchungaji mwema Yesu ambaye alikuwa tayari kuutoa uhai wake kwa ajili ya watu wake (YOHANA 10:11,14).

»Kondoo hawa humpendeza Mungu upeo kwa sababu hulisikia Neno la Mungu na kulitenda kama lisemavyo na si maongozi ya viongozi wa dini. Yesu anaposema "hawatapotea" maana yake hawatatupwa katika giza yaani Motoni ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno (MATHAYO 8:12; MATHAYO 22:13;MATHAYO 25:30).

»KUMBE basi, mtu aliyekatika kundi hili ni bora kuliko kundi jingine kwa sababu yeye analifuata Neno la Mungu mia kwa mia ambalo ndiye Yesu mwenyewe na mtu haiingii mbinguni isipokuwa kwa kumfuata Yesu aliye njia, na kweli, na uzima (YOHANA 14:6). Tunamfuata Yesu na kufanywa Watakatifu kwa kusikia kweli ya Neno la Mungu ambalo ndilo Neno la Mungu yaani Yesu mwenyewe (YOHANA 17:17). Hivyo basi kuishi maisha ya utakatifu ns kuingia mbinguni ni lazima kwa sababu ya kulitii Neno la Mungu na si maongozi ya wachungaji, dini au mapokeo (WAEBRANIA 12:14).

2: KONDOO VIPOFU WALIOPOTEA

»Kundi hili ni tofauti kabisa kabisa na kundi la kwanza. Kondoo hawa huongozwa na wachungaji vipofu ambao wao wenyewe hawajui waendako  kwa sababu hiyo basi wote hutumbukia shimoni (MATHAYO 15:14; LUKA 39-40).

» Watu hawa humheshimu Mungu kwa midomo(maneno) yao ila mioyo yao iko mbali na Mungu kwa sababu hawalifuati Neno la Mungu bali mapokeo ya viongozi wao wa dini (MATHAYO 15:7-9).



»Kondoo vipofu waliopotea huwa wako gizani, hawana nuru ya wokovu ambayo ni kweli ya Neno la Mungu kwa sababu mungu wa dunia hii ambaye ni shetani huwa amewaweka chini ya amri zake na hawawezi kulielewa Neno la Mungu hata ukitaka kuwafundisha wanaweza kukupiga hedi (2 WAKORINTHO 4:4).

» Hawapendi makaripio na maongozi ya Mchungaji mwema Yesu bali hutaka maongozi yao wenyewe.

»Watu hawa hupendelea kusikia maneno laini yadanganyayo na si maneno ya uzima (ISAYA 30:9-10).
Maneno laini hayo ndiyo miujiza na kutabiriwa.

»Watu hawa hupenda kupokea miujiza bila kufikiri kuwa inatokana na Mungu au Shetani.

»Wahubiri wengi wamewafanya watu kuwa kondoo vipofu waliopotea kwa kushindwa kuwaambia ukweli wa Neno la Mungu aidha wakihofia kukosa waumini kwa sababu waumini wenyewe hawataki kweli au kwa kuwa wao wenyewe ni vipofu wakiongozwa na Shetani (YEREMIA 50:6) 

»Hawa hupokea kila kitu wanachoambiwa na wahubiri; wakiambiwa kula nyasi wanakula, wakiambiwa kukanyagwa ili wapokee upako wanakanyangwa, wakiambiwa wanunue mafuta au sabuni ya upako wao ni sawa,  wakiambiwa wavue nguo za ndani ziombewe kwao sawa, wakishikwa matiti na sehemu za siri wanapoombewa wao ni sawa, wakitomaswa na kubusiwa au kunyonywa ulimi ili wapokee upako wao kila kitu twende kazi,   wakiambiwa maji ya mto ule aliobatiziwa Yesu yana upako wao ni sawa, wewe Yesu alibatizwa miaka 2,000 (elfu mbili) iliyopita ina maana mpaka leo maji ni yaleyale? Mto huo umegandisha maji kama ya kwenye ndoo? Hebu funguka. Haya mara mchanga wa kaburi la Yesu, hivi Yesu walimzika wapi kwanza na hilo kaburi kama wangekuwa wanachota mchanga miaka yote hiyo si lingekuwa limeisha? Na utasikia wana sema " Oooh, man of God" wewe acha ujinga; huyo ni man of Gold siyo man of God. Sasa ni hivi , kwa Habari ya maji, sabuni, nguo au vitambaa, ukiniambia nilete vyangu uombeee it's OK na siyo vyako wewe uniuzie mimi najua unavitoa wapi?

»Yesu mwenye upendo alikuja kwa ajili yetu ili kutuokoa (MATHAYO 15:24) Na amawatuma watumishikuwasaidia watu walioko gizani hivyo ndugu yangu usinichukie (MATHAYO 10:6).

»Yesu ameweka Neno hili ndani yangu ili kututoa katika giza na kutuongoza katika nuru yaani njia ya amani iendayo uzimani, mbinguni (LUKA 1:77-79).

»Wote tulikuwa gizani lakini Yesu wa Upendo akatuweka nuruni (MATHAYO 4:16).

»Tunaingia mbinguni kwa kulifuata Neno la Mungu na si vinginevyo.


Ni mimi Mwinjilisti Zachary John Bequeker wa Mwanza - Tanzania.

Wasiliana nami WhatsApp/SMS/Telegram/IMO/Piga Simu kwa +255-625966236.  

Pia Nifuate Facebook kwa Jina hilo.

Share na wengine wajifunze.

Endelea kutembelea blog hii kujifunza zaidi.

Pakua App Ya Injili Halisi -Bofya Hapa Flower
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295

About INJILI HALISI MINISTRY

Zachary, most known as Zakacheka is the founder of the Injili Halisi Ministry. He is a member of Full Gospel Bible Fellowship Church.. He lives in Mwanza,Tanzania. 0621261295.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply