»UCHAWI ni kufanya tendo la kushirikiana na pepo au majini au mashetani hawa na kuwatumia ili kuwadhuru watu wengine.
»Kazi ya Shetani ni kuchinja, kuua , kuharibu na kuibiba chochote chema tulichonacho (YOHANA 10:10).
»Pepo hawa hawaonekani kwa macho ya kawaida na tena wanaweza kupenya na kufanya makao ndani ya kiungo cha mwanadamu hata kilicho kidogo sana kama mshipa na kukiharibu.
»USHIRIKINA ni ushirikiano na MASHETANI katika kukamilisha kazi zao mbaya.
»Mtu anaweza kufanya mambo ya kushangaza yasiyo ya kawaida au asili(SUPERNATURAL) kwa kutumia nguvu za giza za Shetani au uchawi kama Simoni mchawi (MATENDO YA MITUME 8:9-11).
»Kwa kutumia nguvu za kichawi mtu anaweza KUMLAANI mtu nakupatwa na madhara. Mfano, mtu anaweza kumlaani mtu aliyemwibia fedha zake na kupatwa na madhara mpaka wakati atakapokiri kuzichukua na kuzirudisha kama alivyotendewa MIKA (WAAMUZI 17:1-2). Laana inaweza kuathiri familia nzima, ukoo na hata kizazi hadi kizazi.
»Wachawi walikuwepo tangu zamani. Kabla ya Yesu Kristo, tangu zamani za Farao wa Misri na nyakati zinazofuata wanatajwa wachawi wengi(KUTOKA 7:11; YOSHUA 13:22; 1 SAMWELI 28:9; 2 WAFALME 21:1-2,6; ISAYA 19:3; ISAYA 57:3; DANIELI 2:2; DANIELI 5:7).
»Hata baada ya Yesu Kristo, nyakati za kanisa la kwanza wachawi waliendelea kuwepo. Kulikuwepo mchawi aliyeitwa Simoni aliyekuwa akifanya uchawi katika taifa la Wasamaria(MATENDO 8:9-11). Mchawi mwingine anayetanjwa ni Bar-Yesu au Elima (MATENDO 13:6-8).
» Mungu aliweka sheria kwa lengo la kuwaondosha nyakati hizo (KUTOKA 22:18; MAMBO YA WALAWI 20:27) na akaeleza jinsi watu wake wasivyopaswa KULOGA au kufanya ushirikina na MASHETANI maana hayo ni MACHUKIZO KWA BWANA(MAMBO YA WALAWI 19:26; KUMBUKUMBU LA TORATI 18:9-14).
»Watu wengi kwa kujifanya wako juu kiroho hukana kwamba hakuna uchawi kabisa na kufikiri kwamba kufanya hivyo ndiyo kuishikilia imani ya Ukristo.
»Kuwepo kwa uchawi ni jambo lisilopaswa kukanushwa na Mwanafunzi yeyote wa biblià .
Kwa sababu kuwepo kwa uchawi kunatajwa wazi sana katika biblià .
»Hivyo kulogwa ni jambo lililohalisi.
»Mtu aliyeokoka uchawi hauna nguvu kwake kwa sababu yeye ni Yakobo tena ni Israeli (HESABU 23:22-23) pia Mtu aliye OKOKA ana mamlaka ya kupambana na Wachawi na kuwashinda (LUKA 10:19).
JE, WACHAWI WANAKUSUMBUA?
Bila shaka bado hujaokoka, na hata kama umeokoka bado unasitasita lakini leo amua kuokoka kikwelikweli wala usiwe na michanganyo tena na mamlaka ya Ki-Mungu dhidi ya nguvu za shetani itakuwa juu yako.
JE, WEWE NI MCHAWI? Wachawi wote sehemu yao ni katika moto wa milele na milele alioandaliwa Shetani na hao wote wanaomsaidia kazi zake. Hebu achana na uchawi OKOKA sasa.
Fuatisha sala hii sasa iliupokee mamlaka ya Mungu na uwezo wa kuachana na dhambi ya uchawi. Sema " Bwana Yesu, ahsante kwa Neno lako, hakika mimi Sina uwezo wa kuzishinda nguvu za giza nahitaji uniwezeshe, Bwana Yesu futa Jina langu kwenye vitabu vya hukumu na uliandike katika kitabu cha uzima, nipe uwezo dhidi ya nguvu za giza, niwezeshe kuushinda uchawi , siutaki uchawi kuanzia sasa. Ahsante Yesu kwa kunipa nguvu za kuushinda uchawi katika Jina la Yesu... Amen".
Tafuta kanisa linalohubiri kweli ya neno la Mungu ili uzidi kujifunza zaidi.
Kwa msaada zaidi wasiliana nami Zachary John Bequeker kwa WhatsApp/Telegram/IMO/Piga Simu/SMS kwa +255 625966236.
Pia Nifuate Facebook kwa Jina hilo hilo. Barikiwa!
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295
No comments: