» » SOMO: MADHABAHU MBILI


»Tunapokuwepo kwenye kusanyiko liwe ni la ibada, maombi hata unaposoma Neno la Mungu au kuomba wewe mwenyewe tujue kuna madhabahu ya pili ambayo kazi yake ni kuyabomoa yale ya madhabahu ya kwanza.

»Ilivyo ni kwamba Mhubiri anaposimama katika madhabahu anahubiri pia katika ulimwengu wa roho anakuwepo mhubiri mwingine katika madhabahu nyingine mbele yako, kwa sababu hiyo mtu anaweza kuwepo tu kimwili lakini kiroho anakuwa katika madhabahu ya pili.

 »Kazi ya madhabahu ya pili ni kusahaulisha Neno, kufanya tusilisikie Neno na kulielewa, kufanya tusiyatende mapenzi ya Mungu.

 »Kuna madhabahu ya Mungu na madhabahu ya Shetani. Ile madhabahu ya pili ya Shetani ni sanamu, na kama tunasikiliza Kutoka kwayo hatuwezi kushinda na kwa kufanya hivyo tunashiriki ibada ya mashetani. Ibada ya mashetani inakutoa katika mpango wa Mungu.
Lazima kila ibada iwe na madhabahu. Mungu hataki sisi tushirikiane na mashetani kwa kufanya hivyo tunamtia Mungu wivu na kuwa kama tunapambana naye. Tumeambiwa tuikimbie ibada ya sanamu(1 WAKORINTHO 10:14-22).

 »Unaweza kuwa umekaa na mtu kiti kimoja kanisani lakini yeye asiwe pamoja na wewe hapo ila yuko mbali kabisa; muda huo anaweza kuwa sokoni akiulizia bidhaa , kazini au yumbani akiangalia chungu cha maharage yasiungue wakati yuko amekaa kanisani akisikiliza Neno.

 »Mtu anapokuwa amefunga kunakuwa na madhabahu ya pili ambayo ni ya kufungulia. Mtu huyo atakuwa anawaza "vitumbua vya kwa mama fulani ni vitamu kweli, lazima nitachukua hivyo kwa ajili ya kufungulia".

 »Mtu anaweza kuwa kwenye Maombi na wakati huohuo kuna madhabahu ya pili inayomfanya apange mipango, na wakati mwingine mipango ile huwa ni mizuri kweli kiasi kwamba mtu anaacha kuomba anakaa kupanga mipango na mbaya zaidi baada tu ya muda wa maombi kuisha hakuna cha utekelezaji wa mipango ile kwa sababu ilikuwa ni mipango Kutoka katika madhabahu nyingine.

 »Hata wewe unayesoma ujumbe huu ndani yako kuna madhabahu nyingine inakufanya uwaze kuishia hapa ili uwahi kusoma udaku, kataa madhabahu hiyo katika Jina la Yesu...sema Amen.

 »Mtu anaweza kuwa yuko kwenye ibada anasikiliza neno ,anaomba au anasoma bibliร  huku ana mambo yake mengine kichwani, na kazi hii inafanywa na madhabahu ya pili. »Ni lazima tushindane na mipango yote ya ibilisi isiweze kutuzuia kuomba, kusoma Neno, kufunga na kusikiliza Neno tukiwa kanisani au Nyumbani. Kama hatutashindana na madhabahu ya pili hatuwezi kushinda.

 »Siyo kila aliyeko ibadani anawaza ibada, mwingine anakuwa anawaza mambo ya nje kabisa " Hivi ule mlango nilifunga? Naona kama sijafunga? " Mwingine anawaza "Hivi ile mboga niliichemsha? Siitachacha na hela ya kununua mboga nyingine Sina".

 »Mungu anataka tusikilize Kutoka kwenye madhabahu yake tu aliyoijenga, hivyo nasi tujenge madhabahu ya Bwana ndani yetu tusijenge madhabahu ya ibilisi. Tunapojenga madhabahu ya Bwana tunashinda(KUTOKA 17:14-16). »Tuzibomoe madhabahu zote za kigeni tulizojenga ndani mwetu(WAAMUZI 2:1-5). »Shetani kazi yake ni kutuibia Neno la Mungu ili tusikue kiroho.

 »Ukiwa unasikiliza madhabahu ya pili utafanyiwa dhihaka kama walivyofanyiwa manabii wa Baali , ukiwa kwenye madhabahu ya Bwana unatamba kwelikweli, hivyo utaomba lolote kwa ujasiri na utajibiwa(2 WAFALME 18:21-40, 19:1-3). 

»Tunapoomba jambo lolote huku tuna madhabahu mbili Mungu hawezi kutujibu kwa sababu kutakuwa na shaka mioyoni mwetu"Sijui ni Mungu ametenda? au sijui ni nimepata kwa sababu nilimwendea yule mganga".

 »Eliya alipokuwa na madhabahu moja ya Bwana alikuwa na ujasiri sana na alifanya miujiza ya kupita kawaida, lakini alipoinua madhabahu ya pili ya Yezebeli moyoni mwake hofu ilimjaa.

 »Petro alizama baada ya kuruhusu madhabahu ya pili ya upepo na kuiacha kuiamini madhabahu ya Bwana iliyomwamuru atembee juu ya maji(MATHAYO 14:29-30).

 »Madhabahu ya Bwana inaushindi na Baraka na ndiyo tunayopaswa kuiangalia.

 »Shetani hujenga madhabahu kwa kutuletea matatizo ili tubaki tu kutafuta namna ya kutatua matatizo hayo na kushindwa kuyafanya yale tuliyoamriwa na Sauti ya Mungu ni ya utulivu lakini sauti ya Shetani ni ya kulazimisha watu waisikilize(1 WAFALME 19:9-14).

»Tuzivunje madhabahu zote za Shetani na tujenge madhabahu ya Bwana na kwa kufanya hivyo tunapata mpenyo wa mambo ya Rohoni na mwilini. »Hata katika kazi zetu, biashara zetu, ndoa au Masomo tusikubaliane na masauti ya madhabahu ya pili yanayotuambia kuwa hatuwezi kufanikiwa. Ukisikia masauti "wewe umekaa hapa siku zote hata bidhaa zako hazinunuliki ni lazima utafunga duka au muuzie bidhaa zote yule jirani yako wewe ufanye biashara nyingine, siunaona yeye anavyouza" ukisikia hivi sema mara moja "hapa hafungi duka mtu". Labda wewe ni mchuuzi sauti nyingine itasema " wewe umezungusha ndizi zako na hakuna hata wa kukuita WEWE NDIZI si urudi tu Nyumbani ukazile" ukisikia hivyo usinyong'onyee sema "lazima nauza tena naenda mtaa wa pili nauza zote". Umeenda hospitali wamesema mirija yako ya uzazi imeziba hivyo huwezi kupata mtoto na wewe umejenga madhabahu hiyo, Ibomoe sasa na sema "Naijulikane kwamba wewe ni Bwana ijibuye kwa moto na utashangaa mirija inazibuka unabeba ujauzito".

 Preached by Askofu Nathan Meshack

 Written by Zachary John Bequeker- Mwanza Tanzania +255-625-966-236

 Pia nifuate Facebook kwa Jina la Zachary John Bequeker

Tembelea:
www.zakachekainjili.blogspot.com

Kwa HABARI tembelea: www.zakacheka.blogspot.com

Pakua App Ya Injili Halisi -Bofya Hapa Flower
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295

About INJILI HALISI MINISTRY

Zachary, most known as Zakacheka is the founder of the Injili Halisi Ministry. He is a member of Full Gospel Bible Fellowship Church.. He lives in Mwanza,Tanzania. 0621261295.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply