» » SOMO: JE, MTU ALIYEOKOKA ANAWEZA KULOGWA?


»Mtu aliyetubu dhambi kwa kumanisha kuziacha na kumpokea Bwana Yesu atawale maisha yake, huyu ni mtoto wa Mungu (YOHANA 1:12).

»Watu waliookoka(watoto wa Mungu) ni TAIFA TAKATIFU, ni Yakobo na ni Israeli.

»Nyakati za  biblià wachawi waliloga wengi kwa kutumia uchawi. Waligeuza maji kuwa damu (KUTOKA 7:20-22). Wachawi walikuwa na uwezo wa kuleta vyura katika nchi (KUTOKA 8:5-7) na mengine mengi.

»Mungu alisema HAKIKA HAPANA UCHAWI wowote ule au UGANGA unaoweza kuwadhuru watoto wake yaani Yakobo au Israeli kwa maana yeye Baba yao (Mungu) ana nguvu kama nguvu za nyati (HESABU 23:22-23). Hata kwetu leo watu tuliookoka, ni hivyo hivyo kwa sababu sisi ni watoto wa Mungu.

»Hakuna uchawi wowote au uganga unaoweza kutudhuru au kutubabaisha na kushindana na nguvu za Mungu wetu.

»Mtu aliyeokoka amepewa mamlaka dhidi ya wachawi wote, hivyo hawawezi kumloga (LUKA 10:19).

»Mtakatifu wa Bwana ana ulinzi ambao ni wa hali ya juu ( maximum security) ulinzi huu huondoka mara tu mtu huyo anapotenda dhambi na hivyo kuwapa nafasi wachawi kumloga. Kumbe basi mtu aliyeokoka HAWEZI KULOGWA kama ataishi maisha ya UTAKATIFU lakini akitenda dhambi tayari kunauwezekano wa yeye kulogwa (ZABURI 34:7).

⚫Kama unataka kuzidi kuimarika kiroho, tafadhali endelea kutembelea tovuti hii kujifunza mengi. 

Ni mimi Mwinjilisti Zachary John Bequeker, Mwanza - Tanzania
»Kama una maswali na maoni, Wasiliana nami WhatsApp +255625966236 au Nifuate Facebook kwa Jina hilo hilo.

Pakua App Ya Injili Halisi -Bofya Hapa Flower
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295

About INJILI HALISI MINISTRY

Zachary, most known as Zakacheka is the founder of the Injili Halisi Ministry. He is a member of Full Gospel Bible Fellowship Church.. He lives in Mwanza,Tanzania. 0621261295.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply