MHUBIRI: ASKOFU NATHAN MESHACK
MAHALI: FGBF MWANZA 21.01.2018
MWANDISHI: Zachary John Bequeker
Askofu Nathan Meshack na mkewe Susan Meshack
=>Mungu anawajua walio wake ( 2 TIMOTHEO 2:19).
Waitwao ni wengi wateule ni wachache (MATHAYO 22:14), Wakati
wote mtu wa Mungu jiweke katika kundi la wateule ambao wameyatoa maisha yao kwa
Bwana Yesu, ambao wanahesabu dunia hii kuwa kama mavi na kuona si kitu cha
kushikamana nacho (WAFILIPI 3:8).
Waitwao wengi wako kwenye majengo ya ibada wala hawalijui
neno la Bwana na hawajadhamiria kwenda mbinguni. Haakuna faida ya kuhudhuria
ibada halafu ukaikosa mbingu.
Wateule wako tayari kwa lolote lile mpaka wamuone Bwana.
Walioteuliwa(wateule) wakati wote huwa wako katika kundi
maalum. Hivyo wateule wanakuwa wana uhakika wa kwenda mbinguni .
Hatupaswi kuishi maisha ya unafiki, kwani wanafiki
hawatamwona Mungu .
Mteule anakuwa wakati wote anajilinda ili asimchukize yeye
aliyemteua.
Ni bora kujulikana na Mungu kuliko kujulikana na wanadamu.
Ukijulikana na Mungu unakuwa na nafasi nzuri kuliko kujulikana na wanadamu .
ukijulikana na Mungu yeye(Mungu) anachukua mizigo, matatizo na mambo mengine
yanayokuwa kati yako.
Watu hufanya dhambi kwa sababu hawajajulikanI na Mungu hivyo hawatambuliki kwake kwa sababu ya
dhambi zao (ISAYA 59:2).
Mtu anayejulikana na Mungu hawezi kufanya dhambi kwa sababu
anajua Mungu anamuona wakati wote na mahali popote anapokuwa kwa sababu Mungu
amemchora katika vitanga vyake, mtu huyu anapoomba lolote kwa Mungu husikiwa na
kujibiwa (ISAYA 49:14-19).
Ishara ya kumtambua mtu anayejulikana na Bwana ameachana na
uovu(2 TIMOTHEO 2:19).Maovu hayatakiwi kuonekana kwa watu wa Mungu.Masengenyo,wivu,uasherati,uzinzi,wivu,chuki,uchawi,fitina,uzushi,uadui,ugomvi,ulevi,
na mambo mengine yanayofanana na hayo ni matendo ya mwili(uasi) (WAGALATIA
5:19-21).
Usikae na kufurahia kuwepo tu kanisani hali hujulikani na
Mungu; Lazima wakati wote ulenge kujulikana na Mungu, Mungu akikujua hata
mashetani yanakujua. Paulo alijulikana na Mungu na mashetani pia yalimfahamu
kuw asi mtu wa mchezo(MATENDO YA MITUME 19:15).
Tunatakiwa kuwa watu tulio dhamiria kwenda mbinguni.
Ukiona maisha ya wokovu ni magumu kwako fahamu kwamba
hujaokoka. Kama hujaacha dhambi/maovu halafu unalitaja jina la Bwana kwa
kufanya hivyo unalitaja jina la Bwana bure.
Unapoasi unakuwa dhihaka mbele za adui yako, Mungu huwaachia
adui zetu watupige(KUTOKA 32:25-35).
Kama hujaacha maovu wewe hauko upande wa Bwana. Aliyeupande
wa Bwana hatendi yaliyo machukizo mbele za Mungu. Tunapokuwa kinyume cha Bwana
tunapatilizwa.
Walio upande wa Bwana wakati wote wanalenga kumpendeza Mungu
na si kuwapendeza wanadamu. Tunapaswa tuone fahari juu ya Bwana na si vitu
vingine kwa maaana vitu vingine hupotea(1 WAKORINTHO 1:31).
Roho zinazopenda kwenda mbinguni zinapenda neon la Mungu
lisiloghoshiwa. Roho hiyo inapolisikia neon hulifurahia. Mtu ambaye hajaokoka
hukwaza na neno la Mungu.
Mtu anayejulikana na Mungu hana maneno mengi, kwani kwenye
maneno mengi hapakosi uovu(MITHALI 10:19). Tuyatumie maneno hayo kuhubiri
injili na si kujibariki wenyewe na kuwasema wengine kwa ubaya. Kilicho kinyume
na Mungu tukiweke pembeni. Tunapaswa tuwe wamoja wala mafarakano yasionekane
kati yetu (1 WAKORINTHO 1:10-13).
Hatupaswi kuwa na makundi katika nyumba ya
Mungu sote tu watoto wa baba mmoja(YOHANA 1:12-13) Yesu na Baba ni wamoja hivyo
nasi ni vyema tukawa wamoja (YOHANA 10:30). Lazima tumpendezeshe Mungu wakati
wote na si kua na hofu ya Mungu ya kipindi. Tusipende kutenda makosa kwa sababu
kila kosa lina ujira/mshahara wake(WAEBRANIA 1:1-3)
Safari ya kwenda mbinguni haihitaji kusukumwasukumwa kwani
ni kwa faida yetu wenyewe.
Hakuna amani ya Bwana kwa watenda dhambi, dawa ni KUTUBU ili
upate neema ya kushi maisha yanayompendeza Mungu na kutazamia kuingia mbinguni
Je, unajijua bado hujajulikana na Bwana? Unajua bado dhambi zinakusumbua,
sasa ni wakati wa kupokea uwezo wa kushinda dhambi. Tunashinda dhambi kwa
kufanyika watoto wa Mungu(YOHANA 1:12). Fuatisha maneno haya ili upokee wokovu…Sema
“ Mungu Baba, nasema ahsante kwa neno lako, nimegundua kuwa mimi sikupendezi
wewe bali nimekuwa mtu wakuwapendeza wanadamu . Sasa nakuja kwako nikihitaji
ondoleo la dhambi, nisamehe makosa yangu na unipe uwezo wa kushinda dhambi ili
nikupendeze wewe wakati wote katika jina la Yesu Amen.
Written by Zachary John Bequeker - Mwanza +255625966236
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295
No comments: