By Ev. Zachary John Bequeker +255625966236
Kaini alikuwa ni mtoto wa kwanza (MWANZO 4:1), akifuatiwa na ndugu zake Habili(MWANZO 4:2) na Sethi (MWANZO 4:25) Hawa walikuwa ni kizazi cha kwanza, ingawa watoto waliotajwa ni watatu tu, Adamu alikuwa na watoto wengine wake na waume (MWANZO5:4).Mwanahistoria wa Kiyahudi aliandika kuwa kama walivyosema wazee wa kale Adamu alikuwa na watoto 56, wa kiume 33 na wa kike 23. Biblia haituambii walikuwa watoto wangapi lakini kwa kuangalia umri wa maisha ya Adamu miaka 930 (MWANZO 5:5) tunakubaliana kuwa walikuwa ni watoto wengi. Kumbuka kuwa Adamu na Hawa waliambiwa wazae wakaongezeke (MWANZO 1:28).
Adamu alimzaa Sethi akiwa na miaka 130 akaishi miaka 800 mingine ndipo akafa (MWANZO 5:4). Mwanamke aliambiwa atazidishiwa uchungu (MWANZO 3:16).
»Kuna madai kuwa Kaini baada ya kumuua ndugu yake Habili alitoka na kwenda Nodi na ndiko alikompata mwanamke/mke wake (MWANZO 4:17) na kusema kuwa kipindi hicho Nodi ilikuwa na watu walioishi tangu zamani (pre adamic human/pre adamiam)kabla ya Adamu kuwepo na kudai kuwa aliyeolewa na Kaini ni moja ya watu hao(Pre adamic human / pre adamism). Wengine husema alikuwa ni moja ya malaika walioasi.
»Biblia iko wazi sana kuwa mtu wa kwanza ni Adamu(MWANZO 1:26), Adamu anaitwa mtu wa kwanza ( 1 WAKORINTHO 15:45). Kabla ya Adamu kuumbwa hakukuwa na mtu duniani(MWANZO 2:5-8) Mungu alipomuumba Adamu akaona yuko peke yake, Mungu akamfanyia wanyama na ndege lakini hawakufanana naye (MWANZO 2:18-20) ndipo akamfanyia Hawa"Eve" mama wa viumbe vyote (MWANZO 3:20).
Hivyo ni vyema tukatambua kuwa hao watu wanaodaiwa kuwepo " pre adamic humans" hawakuwepo kwa sababu hata kabla Mungu kuumba dunia inaoneaha hakukuwa na watu (MWANZO 1:1-2).
»Tunaposoma neno " MKE" kwa lugha ya kiebrania ni "ishshah" linamaanisha WOMAN/ WIFE /FEMALE yaani MWANAMKE/MKE. Mwanamke ni yule aliyetokana na Adamu (MWANZO 2:23).
»Kumbe tunaona kuwa Kaini Hakuna pre adamic human / pre adamism bali alioa mwanamke aliyetokana na Adamu mwenyewe.
»Hivyo nasi, bila shaka Kaini alimuoa dada yake au mtoto wa ndugu yake.
Zamani ilikuwa si kosa kaka na dada kuoana. Abraham alimuoa dada yake, Sara (MWANZO 20:12), Amramu, baba yake Musa alimuoa shangazi yake(KUTOKA 6:20), Yakobo alioa binti za mjomba wake (MWANZO 29:1-35). Miaka 400 baadaye Mungu akabadili utaratibu, akazuia dada na kaka kuona (MAMBO YA WALAWI 18:6-18).
»NOTE: Biblia inaposema " akamjua MKE" haimaanishi "akaoa" bali ni kushiriki tendo la ndoa MWANZO 4:17). Mariamu alikuwa hajamjua mume lakini tayari alikuwa ameposwa na Yusufu(LUKA 1:34).
»Hivyo basi , Kaini alipoondoka kuelekea Nodi alikuwa na MKE wake na alipoondoka aliwaacha ndugu wengine wengi waliotaka kumpiga baada ya yeye kumuua Habili(MWANZO 4:15).
NAAMINI UNABARIKIWA SANA NA MASOMO HAYA. NI MIMI EV. ZACHARY JOHN BEQUEKER - MWANZA +255625966236.
NIFUATE FACEBOOK KWA JINA HILOHILO
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295
No comments: