ð Tunapaswa kuzifahamu mbinu za shetani ili
asaweze kujiinua juu yetu na kutukatisha tama.
(2 WAKORINTHO 2:11) .
Hatupaswi
kukata tama kwa sababu tukikata tama hatuwezi kuendelea na safari ya imani.
Mbinu kubwa anayoitumia shetani kuwazuia watoto wa Mungu kuendelea na
imani(wokovu) . Tunatakiw tumwombe Mungu atujaze maarifa ya mapenzi yake na
kutuwezesha kuyatenda. Tutashinda tukiwezeshwa na Bwana na tukimpendeza
kabisa(WAKOLOSAI 1:9-11).
Tusikubali kukatishwa tama, lazima Yesu asimame
upande wetu. Shetani anafahamu majira ya kuja BWANA YESU na kwa sababu hiyo
anatia bidii kuwakatisha tama watoto wa Mungu kuendelea na wokovu ikli waje
kuwa watu wakukataliwa na aende nao motoni ( UFUNUO 12:12).
Musa alituma watu
12 kwenda kuipeleleza KANAANI, wale 10 wote walikuwa na maneno ya kukatisha
tama isipokuwa wawili tu hawakuwa na maneno ya kukatisha tama, Kalebu
akawaambia TWAWEZA KUSHINDA BILA SHAKA (HESABU 13:17-34) Tunapofanya mambo yetu
lazima tuseme kuwa tunaweza bila shaka.
Kumbe katika maisha ya wokovu au tunapotaka
kufanya jambo lolote lenye mafanikio kiroho au kimwili tusipende kutafuta
kutiwa moyo, kwa sababu watia moyo huwa ni wachache hali wakatisha tama ndio
wengi na huwa na maneno yanayoonekana kama vile yana huruma kwetu. Kwa mfano,
mtu anaweza kukufuata na kuanza kulia akisema”rafiki yangu nakuhurumia, kwa
nini umeokoka? Hujui kuokoka ni kuchanganyikiwa! Na huoni tangu uokoke mambo
yako sasa hayaendi vizuri? Achana na wokovu” mwingine atasema “eheehe! Nakuona
tu, kila siku shule shule, hivi unadhani kwetu kuna wasomi? Wengi mno katika
ukoo wetu walijaribu kusoma lakini hawakuweza kufika popote, walichoambulia ni
mimba tu” , “ Wewe unadhani hapa biashara hiyo uliyoianzisha ya duka la vifaa
vya ujenzi ina soko! Hapa hamna labda
uende kijijini” Maneno hayo ukiyasikia ni kama vile yanahuruma ndani yake kumbe
si lolote wala si chochote bali yanakatisha tamaaa tu; na mara nyingi watu hao
nyuma yao huwa anazungumza Shetani moja kwa moja kama alivyozumgumza na Eva
kupitia kwa nyoka. Ni heri kukata tama nje kuliko kukata tama ndani. Ukisha
kata tama kinachofuata ni KILIO kama wana wa Israeli(HESABU 14:1).
Ni lazima
tuwe na maneno ya Ushindi.Mungu hawaachi kamwe watu wasio kata tama. Kukata tama ni ugonjwa mbaya kuliko UKIMWI.
Shetani hutumia mazingira tunayokuwa nayo kutukatisha tama. Pamoja na magumu
yote tunayoyapitia , tujipe moyo tutashinda kama YESU alivyoshinda(YOHANA
16:33) .
Dhiki, mateso, maudhi na hali ngumu
ya kimaisha hatuwezi luikweka tukiwa hapa duniani hadi Mungu aingilie
kati. Tusikubali kitu chochote kitutenge na Mungu (WARUMI 8:35-39).
Kuna roho za
tegemezi, ambapo pamoja na fursa zilizopo huwa tunashindwa kuzitumia. Tusipende
kuwategemea wanadamu kwa kila kitu, tujijengee mazingira ya kujisimamia sisi
wenyewe(YEREMIA 17:5-8). Shetani hutukatisha tamaa kwa kuzuia au kuchelewesha
majibu ya maombi yetu(DANIEL 10:11-14).
Mtu anapokuwa anatarajia kitu fulani
kinapocheleweshwa au kuchelewa mtu huyo huumia moyoni mwake(MITHALI 13:12).
Pamoja na majibu ya maombi yetu
kuchelewa tusikate tamaa.
Shetani hutumia magonjwa na watu wa karibu nasi kutukatisha tamaa , tukatae hali hiyo katika
jina la Yesu(AYUBU 2:7-10).
Shetani hutumia maneno ya watu kutukatisha tamaa
kiroho na hata kimwili; Maneno ya wakuu wa makuhani yalimvunja moyo Yuda na
matokeo yake akaishia kujinyonga. Watu tuliookoka tukatae namna yote ya
kukatishwa tamaa katika Jina la Yesu, Sema Ameeeen!
NI MIMI EV. ZACHARY JOHN BEQUEKER WA MWANZA TANZANIA. WASILIANA NAMI KWA WhatsApp +255625966236. PIA NIFUATE FACEBOOK KWA JINA HILOHILO.
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295
No comments: