» » USIOGOPE KWA UNACHOKIONA


Zaburi 37:17-19 “Maana mikono ya wasio haki itavunjika, Bali Bwana huwategemeza wenye haki. Hawataaibika wakati wa ubaya, Na siku za njaa watashiba.”
Huu ni unabii mkubwa sana kwa watu wa Mungu ambao unatimia mbele yetu. Mungu amehidi ahadi nyingi kwa watu wamwaminio hasa.
Mungu anasema “huwategemeza wenye haki” ambapo dhahiri anaonesha kwamba Mungu ni mwaminifu hutimiza ahadi.
Haijalishi ni mambo gani yanatokea duniani, Haijalishi ni habari zipi za kuogofya zinazokujia, jinsi gani dunia inavyoyumba --- watu wa Mungu hawataogopa kamwe. Mungu atatenda sawasawa na kuamini kwetu akitimiza neno lake. Tutapitia magumu na kuhangaika lakini Bwana atajitukuza kwetu, atasimama na kututetea.
Wakristo wanapita katika magumu mengi siku hata siku lakini Bwana atatenda miujiza wakati ambapo akili za kibinadamu zinakosa majibu.
Dada yangu, unaona umri umeenda hujaolewa; rafiki zako wanaolewa kila mwaka lakini wewe bado upo inafikia hatua unakata tamaa kwa kile unachokiona, nakwambia usiyumbishwe na kile unachokiona katika jina la Yesu.
Uko katika ndoa kwa muda mrefu hujapata mtoto hadi wifi zako na mama mkwe wana kudhihaki, nakwambia usikate tama, Mungu aliyempa Sara mtoto ndiye atakayekupa na wewe, Mungu aliyempa Hana mtoto atakupa na wewe, Mungu huyo huyo aliyempa Elisabeti mtoto atakupa na wewe katika jina la Bwana sema Amen kama una amini.
Goliathi kwa kumtazama alikuwa ni mkuu wala hakuna ambaye angeweza kumshambulia. Hata Goliathi mwenyewe alipomuona Daudi akamdharau, akacheeeeka akishangaa, “Hata Mfilisti alipotazama huku na huku, akamwona Daudi akamdharau; kwa kuwa ni kijana tu mwekundu, tena ana sura nzuri. Mfilisti akamwambia Daudi, Je! Mimi ni mbwa hata umenijia kwa fimbo? Mfilisti akamlaani Daudi kwa miungu yake. Mfilisti akamwambia Daudi, Njoo huku kwangu; nyama yako nitawapa ndege wa angani na wanyama wa mwituni. Ndipo Daudi akamwambia yule Mfilisti, Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la Bwana wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana”

HITIMISHO: Jambo kubwa hapa ni kuweka imani yako kwa Mungu asilimia 100%. Mungu hawezi kukuacha uaibike kamwe kwani ukiaibika wewe ameaibika na Yeye, hivyo ni lazima atakupigania. kuna mambo mema mengi ambayo Mungu ameweka kwa ajili yako, Mwamini yeye naye atatenda katika jina la Yesu.

KWA MAFUNDISHO TEMBELEA;
💕 Sharing is Caring💓

Pakua App Ya Injili Halisi -Bofya Hapa Flower
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295

About INJILI HALISI MINISTRY

Zachary, most known as Zakacheka is the founder of the Injili Halisi Ministry. He is a member of Full Gospel Bible Fellowship Church.. He lives in Mwanza,Tanzania. 0621261295.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply