» » NINI MAANA YA MKRISTO KIBIBLIA?



> Si kila anayejiita MKRISTO ni MKRISTO wa kweli. Si kila adhaaniwaye kuwa ni MKRISTO basi ni MKRISTO halisi.

Neno MKRISTO linatokana na neno KRISTO. Na Kristo ndiye Kiongozi wa Ukristo.
Kwa hiyo Mkristo inamaanisha ni mfuasi wa Krsito , ni mtu anayemfuata Kristo. Kwa hiyo kama sisi ni wakristo tunapaswa kumfuata kristo.

Ukisoma katika Matendo ya Mitume 11:26 utaona watu wanaotajwa kuwa ni WAKRISTO.

"hata alipokwisha kumwona akamleta Antiokia. Ikawa kwa muda wa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. Na wanafunzi waliitwa Wakristo kwanza hapo Antiokia."
WAKRISTO ni wanafunzi wa Kristo. WAKRISTO ni watu wanaojifunza mafundisho ya Yesu Kristo.

Unapoutaja Ukristo unamtaja Kristo na unapojitambulisha kuwa wewe ni MKRISTO umemtambulisha Kristo.
Kama hutaki kuhubiriwa au kuhubiri juu ya kristo wewe ni mwongo wala wewe si MKRISTO.
Mkristo anafurahi kuhubiriwa na kumhubiri Kristo.

KWA MAFUNDISHO TEMBELEA
🔗zakachekainjili.blogspot.com
💕 Sharing is Caring💓

Pakua App Ya Injili Halisi -Bofya Hapa Flower
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295

About INJILI HALISI MINISTRY

Zachary, most known as Zakacheka is the founder of the Injili Halisi Ministry. He is a member of Full Gospel Bible Fellowship Church.. He lives in Mwanza,Tanzania. 0621261295.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply