» » SOMO: MTU MWENYE AKILI NI YUPI?




Na Ev. Zachary John Bequeker


Biblia inatuambia kinyume cha mtu mwenye akili ni mpumbavu. Na mpumbavu ni mtu ambaye anasema moyoni mwake kuwa hakuna Mungu.


ZABURI 14:1 “1 Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema.”


Mpumbavu ni kafiri na kafiri humkana Yesu Kristo kama tunavyoona katika YUDA 1:4 “Kwa maana kuna watu waliojiingiza kwa siri, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo.”


Mpumbavu humtukana Mungu.
ZABURI 74:22 “Ee Mungu, usimame, ujitetee mwenyewe, Ukumbuke unavyotukanwa na mpumbavu mchana kutwa.”


Mtu mpumbavu hufikiri hata kuwapo hai kwake ni kwa nguvu zake, mali zake na akili zake tu wala si Mungu.

ZABURI 92:5-6 “5 Ee Bwana, jinsi yalivyo makuu matendo yako! Mawazo yako ni mafumbo makubwa. 6 Mtu mjinga hayatambui hayo, Wala mpumbavu hayafahamu”


Kama nilivyosema kuwa kinyume cha mtu mwenye akili ni mpumbavu, na kinyume cha mpumbavu ni mtu mwenye akili yaani hekima.


MWANZO 41:39 “Farao akamwambia Yusufu, Kwa kuwa Mungu amekufahamisha hayo yote, hapana mwenye akili na hekima kama wewe.”

 Mtu mwenye akili ni mtu amtafutaye Mungu.


ZABURI 14:2 “2 Toka mbinguni Bwana aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye Mungu.”


Mwenye akili anamtafuta na Mungu na Mungu hawezi kumuacha mtu huyo.

ZABURI 9:10 “10 Nao wakujuao jina lako wakutumaini Wewe, Maana Wewe, Bwana hukuwaacha wakutafutao.”


Mpumbavu hupotea kwa sababu hamtafuti Mungu, ukimtafuta Mungu, yeye hukuongoza katika njia iliyo sahihi.


ZABURI 49:10 “Naam, ataliona, hata wenye hekima hufa; Mpumbavu na mjinga hupotea pamoja, Na kuwaachia wengine mali zao”


Mpumbavu hajui kitu kwa sababu hataki kutafuta, yaaani kumtafuta Mungu.

MITHALI 9:13 “Mwanamke mpumbavu hupiga kelele, Ni mjinga, hajui kitu.”


Mtu mwenye akili hulifuata neno la Mungu na mpumbavu hawezi kuyapokea wala kuyafuata maneno ya Mungu MITHALI 10:8 “Aliye na akili moyoni mwake atapokea agizo; Bali mpumbavu mwenye maneno mengi ataanguka.” Na kwa namna hiyo ni lazima atapotea kwa sababu amelikataa neno la Mungu ambalo ndio njia na taa ya mwanadamu. ZABURI 119:105 “Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu.”


HITIMISHO: Mtu mwenye akili ni yule amtafutaye Mungu, huyapokea maagizo ya Mungu yaani neno la Mungu na kulitenda na kwa namna hiyo haawezi akapotea na kuangamizwakwa sababu huyafuta maarifa ya Mungu. Anaye yakataa maneno ya Mungu amemkataa Mungu mwenyewe. HOSEA 4:6 “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe…” 

Je, unataka kuwa mwenye akili au mpumbavu? Chaguo ni lako.


INJILI HALISI MINISTRY

+255 625 966 236

+255 758 590 489

www.zakachekainjili.blogspot.com

Pakua App Ya Injili Halisi -Bofya Hapa Flower
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295

About INJILI HALISI MINISTRY

Zachary, most known as Zakacheka is the founder of the Injili Halisi Ministry. He is a member of Full Gospel Bible Fellowship Church.. He lives in Mwanza,Tanzania. 0621261295.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply