» » SOMO: NI NANI MWENYE HAKI?



Na Ev. Zachary John Bequeker

Mtu mwenye haki ni mtu anayeenda pamoja na Mungu (MWANZO 6:9) Kwa sababu Mungu ni Mungu mwenye haki (KUTOKA 9:27, ZABURI 145:17)

Haki hutoka mbinguni, maana yake mbinguni kumetawala haki na kama mtu yeyeote hapendi wala kutenda haki huyo hawezi kuingia mbinguni wala hawezi kumpendeza Mungu (ZABURI 85:11)

Kinyume cha haki ni uovu na kinyume cha mwenye haki ni mwovu yaani mwenye dhambi (MWANZO 18:23,  2 SAMWELI 1:10).


Mwenye haki ana ujasiri wa kusimama mbele za Mungu na ana hakika kwamba muda wowote akifa anaingia mbinguni lakini muovu hana ujasiri wa kusimama mbele za Mungu wala hawezi kuufurahia uwepo wake Mungu kwa sababu yeye ni mchafu na badala yake hatotaka kabisa kusikia habari za neno la Mungu kwa sababu linagusa maisha yake na kumfanya akose amani. (ZABURI 68:3 ZABURI 28:1).


Mwenye haki anapenda amani , na kwa kupenda amani anakuwa anampenda Yesu aliye mfalme wa amani. (ZABURI 85:10).


Mungu atawatenga wenye haki na waovu siku ile ya hukumu (MATHAYO 13: 43,49)  Mungu huwapenda wenye haki na atawaangamiza wasio haki yaani waovu (ZABURI 146:8 ,ZABURI 145:20, ZABURI 11:18,11).


Mungu hana haja ya kumtafuta mwenye haki kwa sababu mwenye haki kwa Mungu ni sawa na mvuvi aliyekwisha weka samaki kwenye mtumbwi halasu sasa anatupa nyavu mtumbwini ili awapate samaki hao badala yake mvuvi huyo atatupa nyavu mtoni, ziwani au baharini ilia pate wengine. Na ndivyo Mungu wetu alivyo. Yesu Kristo anakutafuta wewe mwenye dhambi ili upate kutubu LUKA 5:32 “Sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi, wapate kutubu.”



HITIMISHO: Mtu anaye hesabiwa kuwa ni mwenye haki ni yule anayeshika na kulifuata neno la Mungu. Sheria za Mungu ni maagizo yake yote atupatiayo kupitia neno lake.  EZEKIELI 18:9 “9 tena ikiwa amezifuata sheria zangu, na kuzishika hukumu zangu; mtu huyu ni mwenye haki; hakika ataishi, asema Bwana MUNGU.”


Huwezi kuwa na amani kama hutendi haki wala huwezi kuwa na haki kama humtaki mfalme wa amani yaani Yesu Kristo. ZABURI 85:10 “Fadhili na kweli zimekutana, Haki na amani zimehusiana.


Kumbuka kila kazi inastahili mshahara na mashahara wa dhambi ni mauti ya milele.Ni chaguo lako kwamba uendelee kutenda uovu au utubu ili uwe mwenye haki.

WARUMI 6:23 “3 Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti…..”


Mwenye uwezo wa kuwaokoa wanadamu na dhambi zao ni Yesu pekee. Mkubali Yesu leo.

MATHAYO 1:21 “Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao


INJILI HALISI MINISTRY

+255 625 966 236

+255 758 590 489

www.zakachekainjili.blogspot.com

Pakua App Ya Injili Halisi -Bofya Hapa Flower
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295

About INJILI HALISI MINISTRY

Zachary, most known as Zakacheka is the founder of the Injili Halisi Ministry. He is a member of Full Gospel Bible Fellowship Church.. He lives in Mwanza,Tanzania. 0621261295.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply