Na Mwinjilisti Zachary John Bequeker
+255625966236/+255758590489
Jumapili ya matawi
itakuwa ni lini 2019?
Jumapili ya matawi mwaka huu itakuwa ni Aprili 14, 2019.
Kwa nini Jumapili ya
Matawi ni Muhimu kwetu?
Jumapili ya Matawi ni ishara ya wiki takatifu, inawakilisha
siku ambayo Yesu aliingia Yerusalemu kwa shangwe na ushindi mkuu akiwa amepanda
punda akiwa na kusanyiko kubwa la watu waliokuwa wakimsifu kwa shangwe nyingi
sana. (MATHAYO 21:1-11)
Ni wiki ya kabla ya kufa na kufufuka kwake, na matukio ya
siku hiyo hukumbukwa katika ibada maalumu ya Jumapili ya matawi.
Kwanini tunaiita
Jumapili ya matawi?
Wakristo husherehekea kufufuka kwa Yesu Kristo siku ya
Pasaka.
Jina la Jumapili ya matawi linatokana na matawi ya mitende
ambayo watu walitandaza chini naye Yesu akapita juu yake akiwa amempanda punda
kuingia Yerusalemu.
Matawi ya mitende ni alama ya amani na ushindi.
Yesu alipofika katika
mji mtakatifu wa Yerusalemu watu walitandaza matawi ya mitende na mavazi
chini kwa kumheshimu yeye(Yesu).
Ilitabiriwa katika agano la kale kwamba watu watamtambua
Masihi akiwa amempanda mwanapunda akiingia Yerusalemu na watatandika matawi ya
mitende.
ZEKARIA 9:9 “ Furahi sana, Ee binti Sayuni; Piga kelele, Ee
binti Yerusalemu; Tazama, mfalme wako anakuja kwako; Ni mwenye haki, naye ana
wokovu; Ni mnyenyekevu, amepanda punda, Naam, mwana-punda, mtoto wa punda.”
HII NI INJILI HALISI MINISTRY, KWA MAWASILIANO +255 621 261 295
No comments: